Hii inaonekna kwamba sio muaminifu na hautaki kumpa mungu nafasi yake.
Hiyo ni Rushwa tena ya kizamani sana.Na ninakuomba kwa faida yako ya humu duniani na mbele ya Mungu ondoa fikra hizo.
We unasema utampa mtu pesa nono kwanini usianze biashara ndogondogo kwa pesa hiyo.
Na ninani amekuambia walioajiriwa ndio wanamaisha mazuri.
Naimani mungu ndio aliekupa hicho kiasi cha pesa cha hongo,na tambua kwamba mungu amekujaalia hizo pesa kwa malengo maalum na hekma zake na sio kama ilivyo dhamira yako.
Amini mungu,weka juhudi utafanikiwa na usikimbilie katika njia za kumuudhi mungu kwa style hiyo.
Na inaonekana kwamba unaulimbukeni wa ajira za utumwa na sio kujituma mwenyewe.
Na Pia wewe mpaka hapo sio muaminifu,maana umeshindwa kumuamini mungu wako mwenyewe kwa kufanya juhudi na subira na kujituma binafsi,utashindwaje kumuibia hata muajiri wako au kusuka mpango wa Ujambazi kwa muajiri.
Kuwa makini,Life is how you make it.