Kazi na Bata ni kauli mbiu inayomnyima usingizi Dr Bashiru

mogulnoise

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
2,434
5,535
Ni kweli kauli mbiu ya Kazi na Bata imekuwa mwiba wa koo kwa CCM

Lumumba kuna waka Moto barua za kuwaita wale Wazee zimekwama, Makamba kasema amechoka wamwite Mzee wa Kazi na Bata hashikiki huku comred akiwa anapiga jalamba msituni

Hakika Bashiru na yule mnunua binadamu viti havikaliki wakiangalia ule ujambazi wa serikali za mitaa waliofanya huku wananchi wakiwasusia huku Mzee wa Kazi na Bata anapasua ngome , hali ni mbaya Lumumba kuliko tujuavyo

CC Mzee tupa tupa
 
Kaulimbiu yoyote duniani huambatana na kuuwa saikolojia ya kitu furani.. KAZI na Bata ni Tamu lakini inauwa saikolojia nyingi ambazo RAIS mbunifu inabidi asema vijana wameamua Kula MAISHA na kuendelea kutengeneza Hela za Manyoka kama nilivyosoma jamiiforum... Ukitaka ujue KAZI na Bata inauwa stress gani ungana na Mie:

1: stress ya kujenga kichwa (Elimu)

2: stress ya kujenga nyumba (walijenga hawatakiwi kuzijudge)

3. Kujenga maeneo ya Kula bata mathalani (Clubs, Casino, shopping malls, Maziwa sehemu zenye ukame n.k) -- Yawezekana miradi YENYE ni milioni 100, Kwa 💯 Tu

4.Kuwa na Usalama wa chakula (food security). N.k

5. Malipo ya hela ya assurance Kwa wote la sivyo mambo yangu hatakiwi kikuathiri

La sivyo ni kama kilimo Kwanza ukawa kaulimbiu 😁😁😁😁
 
Wewe nawe acha kuzingua! Kila uzi unaweka hii mi maandishi yako! Kwani huna kitu kingine cha kuchangia?
 
Ni kweli kauli mbiu ya Kazi na Bata imekuwa mwiba wa koo kwa CCM

Lumumba kuna waka Moto barua za kuwaita wale Wazee zimekwama, Makamba kasema amechoka wamwite Mzee wa Kazi na Bata hashikiki huku comred akiwa anapiga jalamba msituni

Hakika Bashiru na yule mnunua binadamu viti havikaliki wakiangalia ule ujambazi wa serikali za mitaa waliofanya huku wananchi wakiwasusia huku Mzee wa Kazi na Bata anapasua ngome , hali ni mbaya Lumumba kuliko tujuavyo

CC Mzee tupa tupa
Siyo Bashiru tu ila kila mtanzania mzalendo anaipenda nchi yake lazima ashangazwe na kauli ya kijinga namna hii! Nchi yetu ni miongoni mwa nchi maskini kabisa dunia halafu badala ya kuwahimiza watu wafanye kazi kwa bidii zote unawaambie eti kazi na bata? Ujinga ulioje! Zitto anajua watanzania wengi ni wavivu ndiyo maana anaingia na slogan ya namna hii ili kuwavutia. Nchi yetu siyo nchi ya kazi na bata hata kidogo ila inabidi iwe ya kazi na kazi.
 
Mkuu nchi yetu Ni tajiri-by jpm
 
Mkuu nchi yetu Ni tajiri-by jpm
Kwani ni uongo? Huna habari tuna raslimali nyingi sana na tunahitajika kufanya kazi ya ziada ili tuigeuze hiyo raslimali ili itufae? Tuna ardhi yenye rutuba na maji tele. Tuna madini ya kila aina. Ni uvivu wetu tu ndiyo unatufanya tuishi kifukara. Ndiyo maana mjinga yeyote anayesema tunahitaji kazi na bata hatufai.
 
Ni uvivu wetu tu ndiyo unatufanya tuishi kifukara
Uvivu wa kuiondoa CCM mandarakani inayoshindwa tafuta masoko ya mazao yanaozea kwa wakulima, inauza madini nje kwa bei chee, inashindwa tagaza vivutio vya utalii, inashidwa kuweka mazingira bora kwa wafanyabiashara, inashindwa kutoa elimu bora kwa watu wake ili waweze kujiajiri, inateka na kuuwa watu wenye akili na mapenzi mema ya nchi, nk nk.....
 
Nikiona mtu nayedhani CCM ikiondoka basi maisha yatabadilika huwa namwonea huruma sana. Tatizo letu ni zaidi ya CCM. Hizo nchi nyingine za Afrika zenye utajiri lakini bado ni maskini zinataliwa na CCM?
 
CCM sio jina, ni fikra na matendo, huko kwingine kuna CCM yenye jina lingine.........
 
Ahaa. Goli linahamishwa polepole. Kumbe hata Chadema inaweza kuwa CCM yenye jina jingine! Sasa kinachokufanya usikubaluane na mimi kuwa taizo siyo CCM bali ni sisi waafrika ni nini?
 
Nikiona mtu nayedhani CCM ikiondoka basi maisha yatabadilika huwa namwonea huruma sana. Tatizo letu ni zaidi ya CCM. Hizo nchi nyingine za Afrika zenye utajiri lakini bado ni maskini zinataliwa na CCM?

Mkuu naomba niufanye mjadala uwe mrefu kidogo halafu twende kwa hoja na huyo jamaa..

Ni vyema tumuulize anafikiri kwanini CCM ndio chanzo au moja ya chanzo cha umasikini wa watanzania??..

Kwanini pia unafikiri CCM sio moja ya chanzo au chanzo kikuu cha umasikini wa Watanzania?? Je kama sio CCM tatizo ni nini???
 
Siyo Bashiru tu ila kila mtanzania mzalendo anaipenda nchi yake lazima ashangazwe na kauli ya kijinga namna hii! Nchi yetu ni miongoni mwa nchi maskini kabisa dunia halafu badala ya kuwahimiza watu wafanye kazi kwa bidii zote unawaambie eti kazi na bata? Ujinga ulioje! Zitto anajua watanzania wengi ni wavivu ndiyo maana anaingia na slogan ya namna hii ili kuwavutia. Nchi yetu siyo nchi ya kazi na bata hata kidogo ila inabidi iwe ya kazi na kazi.
Mkuu umasikini wa nn?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom