Kazi kwenu- tanzania railways | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi kwenu- tanzania railways

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Abunwasi, Oct 3, 2012.

 1. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Salam toka kenya ni kwamba baada ya re-structuring shirika la reli la kenya limepata faida ya Ksh 1.2b na wanaimani kuwa faida zaidi itapatikani katika siku zijazo. Sasa basi tuliowapa dhamana ya kuendesha shirika letu la TRL badala ya visingizio visivyokwisha hebu nendeni kwa ndugu zenu kenya wawaambie siri ya mafanikio yao. Vilevile siyo vibaya kuanza kushughulikia kinganisho mlicho kiacha kati ya reli ya kenya na tanzania kwani ninaamini ni biashara nzuri tu kama ilivyokuwa miaka ileee.
   
 2. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hawa sikivu sijui kama wamekusikia sawasawa,
  Ni vizuri kujifunza kwa wenzetu kwani mabadiliko ni lazima, hayakwepeki.
   
 3. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Watanzania hatuna utamaduni wa kuiga maendeleo labda ingekuwa ufisadi 2ngeiga
   
 4. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tunakimbizana New York kufyeka kodi. Tutapata wapi muda wa kuiga ya reli? Na kama tutaiga malori ya mtoto wetu yatapataje biashara? Nyie watanzania ni wajinga wa kutupwa. Baba, mama, na mtoto wanawafaidi kwa kuuwa system nzima inayowafaidi wanyonge wenu. Ni bora mfe wate, ila kilaza mmoja na familia yake wafaidi. Mtaamka lini? Kodi mnayokatwa ni mara tano ya wakenya. Maendeleo mlio nayo ni mara zero ya wakenya. Ulishaona nchi ambayo haina reli wala ndege za uhakika? Kama mnashindwa kiasi hicho mbona ndege ya raisi wenu inaruka angani kila siku kukimbilia US? Mbona matrack ya mkewe na mwanaye yanamiliki vibarabara uchwara mlivyo navyo? Ni kwa nini hamuwezi kumili reli ambazo zingesafirisha mizigo na abiria kote nchini kwa bei nafuu kabisa? Kodi senu mnazotoa zinafanya nini kwa manufaa ya umma? Wakenya tuliuwana, lakini tumekaa chini tukaamua kufanya mabadiliko. Je nyie woga wenu utawafikisha wapi?
   
Loading...