Ulichosema ni kweli kabisa,ukiacha benki,kwa sasa kazi zinauzwa. Kinachokuja kuiua Tanzania ktk ajira ni RECRUITMENT AGENCIES. Kazi zote zinafichwa huko na kudokoa moja moja kwa bei wanayoitaka wao. Mkuu hapa graduates tegemea kuumia. Juzi nlipigiwa cm mtu wa Tra anadai kuna kazi ila kupoza Boss ni 2mil,nlipowaeleza rafiki zangu wanasema eti ndo fasheni. Kuna rafiki yangu aliitwa akaambiwa kuwa shortlisted laki,sawa mshahara mkubwa ila je usiposhinda interview? Nakuakikishia kama una ela kazi unapata,unaweza kusign mkataba hata usiku sa2 wenye tarehe ya siku inayofuata. Siku hizi graduates wanaiita 'Initial Investment'. Kumbuka walio makazini hawataki kusikia maneno aya ila ukweli utabaki kuwa ukweli! Ivi una habari kuna wanafunzi wamehitimu Nov.ila kwa kuwa na Initial capital sasa ni wakurungezi,hapa sitaji majina,wala tusiseme cha GPA,experience,wala akili,mimi nawajua mwanzo mwisho na nimeishi nao ila kwa kuwa na chochote wako na nyadhifa kubwa ambazo najua kama zngetangazwa wangeandika 'experience 15yrs anda above' ila mbele ya ela wako mbali. Yan wawili wao wamepewa hadi nyumba,gari na salary gross over 3mil. Huu ni ufisadi na ubaguzi ambao matajiri wanauita bahati ya mtu,ila wanyonge wanauita upendeleo! Ila alienacho ataongezewa,waliobaki mdogo mdogo tutafika.