Kaya 343 Kinondoni zagomea Sensa Dar es Salaam

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,903
32,312
Wanabodi,

Mratibu wa Sensa Wilaya ya Kinondoni Ando Mwankunga, amesema watu wanaoishi katika kaya zaidi ya 243 wiliyani humo wamekataa kuhesabiwa.

Alisema watu zaidi ya 40 waligoma kuhesabiwa, na kuongeza kuwa kuongeza kuwa kata ya Msingani kaya 21 zimegoma, kata ya Makurumla ina kaya 95 wamegoma, kata ya Mbweni kuna kaya 15 wamegoma, kata ya Msasani kuna kaya 45 wamegoma.

SOURE; Mwananchi Septemba 4 2012
 
hii ni dalili kuwa wananchi hawana utii na serikali ya ccm, hata tuliohesabiwa tumefanya hivyo ili data zitumike kwa serikali ijayo ya 2015 wakati ccm ikiwa upinzani.
 
Taarifa njema kabisa hii! na itakuwa fundisho kwa serikali sikivu!!

Kereng'ende 40 hawawezi kusukuma helikopta. Pamoja na kutoipenda serikali ya CCM, sensa ni kwa maendeleo ya Taifa. Hata tutakapochukua madaraka 2015, tutahitaji takwimu hizi kupata pa kuanzia ukuzingatia hali itakuwa ni mbaya.

Kinachonishangaza ni kuona kuwa kuna watu wenye kufikiria kwa viungo vya kukalia kiasi wanaona hili ni jambo la kufurahisha. Yule mwenyewe aliyewaambia mgome, AMEHESABIWA
 
Kama umeshahesabiwa si usubiri uletewe maendeleo mkuu tatizo liko wapi!!!
 
Kwa ujumla zoezi la sensa mwaka 2012 limeshindikana ingawa serikali ya ccm imeongeza neno "changamoto"
 
Tatizo halipo kwenye kutohesabiwa tu,bali hata kwa waliohesabiwa data zimechakachuliwa.Mfano kwangu karani alimkuta wife akamuuliza maswali 3 out of 62;jina,kazi na umri.Kwa jirani aliwakosa akaacha maagizo wakija waache majina tu,keshoyake asubuhi atayapitia i.e swali 1 out of 62... HIYO NDIYO SENSA!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wnaogomiea sensa mi naona hawana akili naomba mnisahihishe kama nakosea
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom