Kawambwa ni Mzigo kwa Taifa...

Nilimdharau tangu aliposhindwa kumfukuza "mkuu wa shule ya sekondari Ndada" kwa vitendo vyake vya kijinga na kufukuza wanafunzi 20 kwasababu eti wanaomba sehemu ya kufanya ibada? ..

Hana maana kabisa.
 
Kawambwa analazimishwa na Baba Mwanaasha tu Kuingia kwenye Siasa ili kuibeba Bagamoyo,
but nafikiri hata yeye 1)Haipendi Siasa,
2)Haiwezi Siasa.
Ni waziri pekee ambae nina uhakika wa 101% kama CCM wakirudi 2015 (Mungu aepushie mbali) hatokuwepo kwenye cabinet.
 
Mimi huwa nashindwa kabisa kuelewa kwanini huyu mtu huwa anapewa uongozi. Hana uwezo.
 
Huyu jamaa was a good lecturer at FOE ya enzi hizo kabla ya COET. Kwanini asiachane na siasa akaenda kufanya kazi anayoiweza? Kwani lazima kuwa mwanasiasa?
 
Nilimdharau tangu aliposhindwa kumfukuza "mkuu wa shule ya sekondari Ndada" kwa vitendo vyake vya kijinga na kufukuza wanafunzi 20 kwasababu eti wanaomba sehemu ya kufanya ibada? ..

Hana maana kabisa.
kwako wewe angewarudisha wale wanafunzi waliofanya fujo na kujenga msikiti ndanda ndiyo angekuwa waziri mzuri hata kama maendeleo ya elimu yakiwa duni tz?
 
kwako wewe angewarudisha wale wanafunzi waliofanya fujo na kujenga msikiti ndanda ndiyo angekuwa waziri mzuri hata kama maendeleo ya elimu yakiwa duni tz?

Alitakiwa kumfukuza irresponsible civil servant (mwalimu anayeendekeza UDINI) kwa kuwasumbua wanafunzi wanaotaka kufanya ibada kwa chuki zake, by the way wanafunzi hawakuleta fujo... ndio maana wako tayari shuleni.
 
Ni kweli wakuu JK alione hili amtoe haraka iwezekanavyo
 
..nadhani mfumo wetu wa elimu umeoza na kumlaumu Waziri Dr.Kawamba kutokana na matokeo mabaya ni kumuonea tu.

..ila waziri naye anawajibika kutueleza anachukua hatua gani kuhakikisha kwamba aibu hii ya matokeo mabovu haitokei tena.

..nadhani waziri wa mwisho mwenye uchungu na elimu ya nchi hii alikuwa ni JACKSON MAKWETA. wengine wote waliomfuatia sielewi walichokifanya.
 
Hivi chanzo cha matokeo mabaya serikali haifahamu? wala siyo Kawambwa ila madai na mishahara midogo kwa walimu ni tatizo kubwa.
 
Kimsingi mimi namlaumu sa baba R1 kwa kushindwa kuwachukulia hatua wazembe kama hawa wanaosababisha serikali yote ionekane kuwa janga la taifa.Hapo awali nilikuwa namlaumu kuwa utendaji wake ni mmbivu kumbe nlikuwa nakosea badala yake ni kwamba ameshindwa kuwasimamia, kuwaongoza na kuwawajibisha wateule; hapa nafikiri kwa kuhofia kuwa chama hakitamwelewa kumbe ndo anaua chama!!!???...
 
Mimi Kawambwa simshutumu ila huyo anayewapa maisha ndo wakumpa shutuma(Kikwete) kwani sianatoa nyazifa kirafiki acha wamuaibishe na kuturudisha nyuma kimaisha.
 
GreatThinkers,

Shukuru Kawambwa ni kwa sasa ni waziri wa Elimu.
Matokeo ya form4 yaliyo tangazwa mwaka jana 2011, 11% ndio waliopata kati Div (1-3) waliobaki walikuwa Div 4 na Totally Failures.

Katika 11% ya waliofaulu, 9percent ni private na 2% ni Government.
Matokeo kama hayo pia 2012 pia tumeyaona. Je huyu anafanya nini hapo wizarani-Serikalini watoto wetu wanasoma kweli au wanatupiga changa la macho angali watoto wao wanasoma International School of Tanganyika?
Je migomo ya vyuo vikuu imeisha, St Kayumba wanapata mkopo sasa?

Si Mara ya kwanza-kabla ya kuhamishiwa wizara ya Elimu alikuwa wizara ya Miundombinu awamu hii hii ya nne-Moja ya madudu aliyofanya na kusimamia ni ujenzi wa barabara ya Kilwa-DSM pamoja na Mandela-DSM. Zote zilikuwa chini ya kiwango na baadaye alipohamishwa Magufuri alizikataa na kazi imebidi kurudiwa barabara yote ya Kilwa. Huyo ndiye Kawambwa.

Hapo awali JK alipoanza Urais Kawambwa huyu huyu alikuwa wizara ya mawasiliano lakini hasa aliwekwa ili dili za mkongo wa mawasiliano aweze kula dili kama ambavyo alishindwa ktk miradi ya Barabara na sasa anakomaa na ujenzi wa chuo kikuu kipya cha Afya.
Mimi kwa maoni yangu bila kumuonea mtu wivu wala nini

Kawambwa hafai

Huyu aondoke kwani anakula hela za bure za walalahoi(kodi zetu)si bora tuka jengee shule na kununulia
vifaa kama madawati,vitabu
 
katika mawaziri ambao waweza kuwa hawajui wajibu wao ni pamoja na Kawambwa, huyu jamaa anaonekna kupewa uwaziri ni udau na urafiki maana naona hata waziri msaidizi wake anaonekana kusikika zaidi
 
Back
Top Bottom