Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi UVCCM, Mohamed Kawaida ameeleza kuwa anazo taarifa za baadhi ya asasi za kiraia na vyama vya siasa vinavyowapeleka Vijana wa Kitanzania kwenye mafunzo nje ya nchi ili kuwaandaa kuja kuwa sababu ya machafuko na vurugu ndani ya nchi, akieleza kuwa siku sio nyingi atawataja wahusika ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Mohamed Kawaida ameyaeleza hayo wakati akizungumza na wananchi wa Bukombe Mkoani Geita, akieleza kuwa ni jukumu la Vijana kuzilinda tunu za Taifa ambazo ni amani, umoja na mshikamano hasa wakati huu ambapo Taifa linajiandaa na uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Ninayo orodha ya hizo asasi za kiraia, ninayo orodha ya hivyo vyama vya siasa, ninayo orodha ya hizo Ngo's zinazotuma vijana kutaka kuharibu amani ya nchi yetu. Wakiendelea nitawataja hadharani ili serikali ichukue hatua dhidi yao." Amesema Kawaida.
Kwa upande mwingine katika hotuba yake, ameeleza kuwa UVCCM imejipanga kuhamasisha vijana kuipenda nchi yao na kushiriki kikamilifu katika ushiriki wa uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu, akisisitiza umuhimu wa amani na utulivu kwa maslahi ya maendeleo ya Taifa letu