Kauli zao zinapoteza matumaini mengi ya wengi

Tonytz

Senior Member
Jul 18, 2022
159
1,142
Kwanza nianze Kwa kumshukuru Mungu Kwa uzima na afya anayonijalia SIKU zote.

Pia nawashukuru JF Kwa kuweza jukwaa hili ili kuibua na kuendeleza mawazo yaliyokosa pa kusema.

Wahenga walisema kuwa uyaone. Msemo mwepesi lakini uliobeba majonzi Kwa wale tunaoyaona sasa.

Kwanini wanaendelea kudahili walimu wa masomo ya Sanaa ikiwa wanasema tupo wengi au tumetosheleza mashuleni. Kisiasa ndiyo, lakini kiuhalisia hapana.

Leo natamani kusema wazi kuwa, mioyo ya wengi wanaohitimu vyuo Kwa masomo ya Sanaa imekufa na kupondeka sana. Hivi ni kweli walimu wa Sanaa( Arts) wapo wengi mashuleni? Nulizana nawe mdau wa jukwaa hili.

Huku mtaani WAZAZI WA wahitimu wa ualimu Kwa masomo ya Sanaa tumevunjika moyo kabis na kauli za wanasiasa katika Serikali yetu pendwa, Kwa kauli ya kusema hatuwezi kuajiri walimu wa Sanaa kwa kuwa wapo wengi, hivi mnafahamu maumivu na mateso wanayopotia WAZAZI ambao walipambana kwa shida na ugumu kusomesha watoto zao?

WAZAZI wengine Wamepata hata magonjwa makubwa kwa kuhangaikia masomo ya watoto wao kwenye kuwalipia ada, Leo hii kijana au Binti anaambiwa ajira kipaumbele Kwa waliosoma sayansi. Usawa unazingatiwaje hapo?

Nafikiri ifike kipindi Serikali iamue kuacha kudahili wanafunzi katika masomo hayo,ili kuondoa sintofahamu za wenye matumaini. Lakini ikumbukwe nchi haijengwi na wanasayansi tu, Kila mwenye taaluma Fulani anashiriki katika kujenga nchi.

Ukija katika uhalisia mashuleni walimu wa hayo masomo ya Sanaa ni wachache sana,waliopo wanazidiwa na mzigo mzito,hii ni mfano halisi kabisa,kwani Kuna shule ya msingi hapa jirani kwetu walimu wachache Kwa masomo yote. Lakini je nini dhima hasa ya kuona walimu wa masomo ya Sanaa kama hawahitajiki Kwa sasa?

Kwa kuwa mfumo wetu wa elimu haumtengenezi mwanafunzi kujiajiri,ni budi Serikali ambaye ndiye mwajiri wa kundi kubwa kulitazama suala hili Kwa kina.

Walimu wa masomo haya ya Sanaa Wana matumaini na ndito zao, hivyo zisikatishwe Kwa kauli za kisiasa ambazo zinapelekea kuonekana walimu wa Sanaa kama ni ziada tu katika jamii? Au ndiyo tuamini msemo kuwa " aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa"

Kwa kuhitimisha naomba serikali ikiwezekana waache kudahili walimu kwenye kada ya ualimu wa Sanaa ili pengine kusimamia diri ya kisiasa iliyopo.
 
Ulitaka upewe jibu gani? Mlaumuni Mwendazake si aliwaambia anajenga SGR na kununua ndege Ili mpande au?

Tena mkamuita ana Maono,imekuaje tena? Samia yeye anajiri wake.
 
TATIZO watoto wao hawajasomea kozi hizo. Watoto wa maskini ndio wamejazana huko. Kwa sasa kumsomesha mtoto kozi ambazo hawezi kujikwamua mwenyewe ni ujuha.

Kuna kozi hazistaili kuendelea kudaili kwa sasa ila hawawezi kukukwambia maana nao wanataka pesa.

JANGA LINGINE NI KOZI ZA AFYA ZA D-4
 
Mwalimu analilia ajira akipata akipangiwa buhigwe anaanza kutafuta uhamisho arudi dar au karibu na dar ndo maana utakuta wanajazana mjini wakipangiwa vijijini wanakimbia kwa style hyo hatuwezi ku solve tatizo la ajira na uhaba wa walimu kwa ujumla.
 
Kwa wahitimu wa sekondari wanaokwenda kusomea fani ya ualimu chuo kikuu miaka hii, wanahitaji maombi kwa kweli.
 
Hakika ndugu, familia duni ndizo zinazoteketea. Naomba kura Yako mkuu na Mungu akubariki
 
Mwalimu analilia ajira akipata akipangiwa buhigwe anaanza kutafuta uhamisho arudi dar au karibu na dar ndo maana utakuta wanajazana mjini wakipangiwa vijijini wanakimbia kwa style hyo hatuwezi ku solve tatizo la ajira na uhaba wa walimu kwa ujumla.
Ni kweli,tatizo ni mitazamo tu kibinadamu tunayokuwa nayo miongoni mwetu. Umenena sahihi sana mkuu. Naomba kura Yako mkuu na Mungu akubariki sana
 
Kwa wahitimu wa sekondari wanaokwenda kusomea fani ya ualimu chuo kikuu miaka hii, wanahitaji maombi kwa kweli.
Mungu ni mwema tu ndugu. Na Mapito tu ya kimfumo. Naomba kura Yako ndugu yangu. Na Mungu akubariki
 
Kwanza nianze Kwa kumshukuru Mungu Kwa uzima na afya anayonijalia SIKU zote.

Pia nawashukuru JF Kwa kuweza jukwaa hili ili kuibua na kuendeleza mawazo yaliyokosa pa kusema.

Wahenga walisema kuwa uyaone. Msemo mwepesi lakini uliobeba majonzi Kwa wale tunaoyaona sasa.

Kwanini wanaendelea kudahili walimu wa masomo ya Sanaa ikiwa wanasema tupo wengi au tumetosheleza mashuleni. Kisiasa ndiyo, lakini kiuhalisia hapana.

Leo natamani kusema wazi kuwa, mioyo ya wengi wanaohitimu vyuo Kwa masomo ya Sanaa imekufa na kupondeka sana. Hivi ni kweli walimu wa Sanaa( Arts) wapo wengi mashuleni? Nulizana nawe mdau wa jukwaa hili.

Huku mtaani WAZAZI WA wahitimu wa ualimu Kwa masomo ya Sanaa tumevunjika moyo kabis na kauli za wanasiasa katika Serikali yetu pendwa, Kwa kauli ya kusema hatuwezi kuajiri walimu wa Sanaa kwa kuwa wapo wengi, hivi mnafahamu maumivu na mateso wanayopotia WAZAZI ambao walipambana kwa shida na ugumu kusomesha watoto zao?

WAZAZI wengine Wamepata hata magonjwa makubwa kwa kuhangaikia masomo ya watoto wao kwenye kuwalipia ada, Leo hii kijana au Binti anaambiwa ajira kipaumbele Kwa waliosoma sayansi. Usawa unazingatiwaje hapo?

Nafikiri ifike kipindi Serikali iamue kuacha kudahili wanafunzi katika masomo hayo,ili kuondoa sintofahamu za wenye matumaini. Lakini ikumbukwe nchi haijengwi na wanasayansi tu, Kila mwenye taaluma Fulani anashiriki katika kujenga nchi.

Ukija katika uhalisia mashuleni walimu wa hayo masomo ya Sanaa ni wachache sana,waliopo wanazidiwa na mzigo mzito,hii ni mfano halisi kabisa,kwani Kuna shule ya msingi hapa jirani kwetu walimu wachache Kwa masomo yote. Lakini je nini dhima hasa ya kuona walimu wa masomo ya Sanaa kama hawahitajiki Kwa sasa?

Kwa kuwa mfumo wetu wa elimu haumtengenezi mwanafunzi kujiajiri,ni budi Serikali ambaye ndiye mwajiri wa kundi kubwa kulitazama suala hili Kwa kina.

Walimu wa masomo haya ya Sanaa Wana matumaini na ndito zao, hivyo zisikatishwe Kwa kauli za kisiasa ambazo zinapelekea kuonekana walimu wa Sanaa kama ni ziada tu katika jamii? Au ndiyo tuamini msemo kuwa " aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa"

Kwa kuhitimisha naomba serikali ikiwezekana waache kudahili walimu kwenye kada ya ualimu wa Sanaa ili pengine kusimamia diri ya kisiasa iliyopo.
Inaumiza sanaaaa
 
Safi sana mkuu
 
Back
Top Bottom