Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
TPDC walilalama zoezi la zabuni za vitalu vya gesi asilia liliingiliwa na Waziri husika Muhongo kinyume na sheria ya manunuzi.
Huyu katibu mkuu aliyetumbuliwa alikuwa msimamo mmoja na TPDC kuwa sheria ya manunuzi iheshimiwe na Muhongo aache kuingilia.
Muhongo ana kampuni ya kichina anayotaka ipewe ugali huo na sasa wapinzani wake wameanza kung'olewa kuwapisha wateule wapya watakaohakikisha wachina wanalamba asali!
Ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ni matumizi mabaya ya madaraka na yanaashiria harufu kali ya ufisadi.
Uongozi mzima wa TPDC sitashangaa ukitumbuliwa ili kupisha madudu haya ya hawa walaji.
Huyu Muhongo pamoja na kugubikwa na kashfa kibao leo anaonekana ni jembe sasa nimeanza kujua sababu kumbe ni kulinda Milo ya wakubwa serikalini.
Halafu hawa hawa wanatumbua wasiyo na hatia kumbe wao ndiyo wanapaswa kutumbuliwa!