Nakumbuka kauli ya baba wa taifa kuwa Ikulu ni mzigo na wale wote wenye ndoto ya uraisi wajiandae kutawala nchi ktk mazingira magumu zaidi ya haya ya leo kwani watu sasa wanajua kudai haki zao na si kudanganywa na kuburuzwa.
Mwisho nasema uongozi si kutoa ahadi,si kufunya uzinduzi,si kufanya ziara zisizo na tija,sio kutoa hotuba majukwaani na kwenye makongamano na wala si kuhudhuria mikutano tu au kutaka vyeo na ummaarufu bali uongozi au kutaka uongozi ni mtu kusukumwa na dhamira ya kweli juu ya matatizo,shida,maradhi,umasikini,ujinga na mambo mengine yanayosumbua taifa kwa nia ya kuyaondoa kabisa au kuyapunguza kwa kadri kiongozi anavyoweza.
Viongozi wa leo wengi hawasukumwi na mambo kama hayo bali husukumwa na ubinafsi na tama ya madaraka kwa faida yao na familia zao tu na ndio maana wanashindwa kutimiza majukumu yao kama viongozi wa kitaifa.
Matokeo ya viongozi kama hawa ni wananchi kuteseka na kuishia kulalamika na inakuwa kila siku afadhali ya jana.
Watanzania tusipobadilika ktk kufanya maamuzi kwenye sanduku la kura tutaendelea kulia na kusaga meno mpaka siku Yesu atakaporudi.