Kauli ya Serikali dhidi ya TANESCO ni siasa za uongo Tanzania

dkn

Senior Member
Oct 7, 2010
139
42
Watanzania tunapenda kusikiliza uongo wa serikali ya CCM kwa miaka 50 sasa, utaona jinsi issue ya umeme ilivyowekwa kisiasa mpaka inafika mwisho tunazidi kudanganywa… Waziri anasema tusherekee hata dakika moja kero ya umeme imeisha..leo anasema gesi ni mradi wa mtu binafsi wakati anasema serikali imetumia billion kwenye huu mradi. Angalia mfululizo wa statement za Waziri na Tanesco, MTANZANIA CHUKUA HATUA KUTOCHAGUA SERIKALI NA VIONGOZI WASIO NA UCHUNGU NA TANZANIA BALI MASLAHI BINAFSI.

August 6: Umeme wa gesi sasa kuanza mwezi ujao
Umeme wa gesi sasa kuanza mwezi ujao - Biashara | Mwananchi

Akizungumza juzi wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa bomba hilo na mitambo ya umeme wa Kinyerezi, Simbachawene alisema bomba hilo limekamilika na liko kwenye hatua ya majaribio.

Septemba 17: Tanesco yaahidi umeme wa uhakika wiki hii
Tanesco yaahidi umeme wa uhakika wiki hii - Kitaifa | Mwananchi

Akizungumza mjini Dar es Salaam, jana, Msemaji wa Tanesco, Adrian Severin alisema kazi ya kuunga bomba la gesi kwenye mitambo ya kufua umeme ya Ubungo iliyoanza Julai 7, mwaka huu, ilikamilika juzi kama ilivyopangwa.

Septemba 19: Serikali kushusha bei ya umeme Oktoba
Serikali kushusha bei ya umeme Oktoba - Kitaifa | Mwananchi

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alisema hayo, Dar es Salaam, jana wakati akikagua mradi wa bomba la gesi na kuwashwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Ubungo II na Kinyerezi I.

“Jambo hili ni kubwa na la kihistoria kwa nchi hii kwa kitendo cha kuanza kutumuia umeme wa gesi, tulipaswa kusimama hata kwa dakika tatu kusherekea mafanikio haya kupitia mradi kubwa wa serilkai uliogharimu dola za Marekani 1.22 bilioni”, alisema Simbachawene

Mradi wa kufua umeme kwa Gesi umekamilika nchini na ndani ya mwezi Setemba na Oktoba mwaka huu mitambo yote yenye uwezo wa kuzalisha megawati 335 itakuwa imewashwa na hivyo kuondoa tatizo la umeme hapa nchini. Waziri huyo anasema Septemba 17 pekee waliptisha gesi katika bomba lenye ujazo wa futi 20 milioni na kwamba bomba hilo lina uwezo wa kupitisha futi za ujazo 784 milioni na kwamba ghadi Desemba mwaka huu bomba hilo litakuwa limepitisha futu 130 milioni za gesi, sawa na wastani wa ujazo wa futi 20 milioni kwa siku.

Septemba 25: Tanesco yatoa sababu kukatika umeme mara kwa mara
Tanesco yatoa sababu kukatika umeme mara kwa mara - Kitaifa | Mwananchi

Meneja Mahusiano wa shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO) Adrian Severin amesema tatizo la kukatika kwa umeme litaisha Oktoba mwaka huu baada ya bomba la gesi kujaa baa 52.

Tatizo hili la kukatika kwa umeme litakuwa kwenye mikoa ambayo Gridi ya taifa imepepita hivyo tulianza kuzalisha megawati 90 na tunaendelea kupandisha kiwango taratibu ili kufikia megawati 335 mwishoni mwa Oktoba mwaka huu

Oktoba 9: Tanzania closing hydropower plants
Tanzania closing hydropower plants - BBC News

The closing of the hydropower dams was beyond the government's control, said Badra Masoud, head of communication at the ministry.
"We cannot do anything because of the changes in environment - we are not getting enough rain."
Ms Masoud said more people farming upstream from the dams was not helping the situation, as this reduced the flow of water.
"We are trying to convince Tanzanians not to farm upstream," she said.
According to Tanzania's private Citizen paper, the state-owned power company, Tanesco, has already shut down its major Mtera hydropower plant, which can generate 80 MW.
The country consumes 870 MW but it only currently generates 105 MW, the paper says.

Oktoba 10: Tanesco yazima mitambo ya kuzalisha umeme bwawa la Mtera.
:: Tanesco Yazima Mitambo Ya Kuzalisha Umeme Bwawa La Mtera

Meneja wa Tanesco kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera mhandisi Abdallah Ikwasa amewaambia waandishi wa habari waliotembelea kituo hicho kujionea hali halisi ya uzalishaji umeme kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kupungua kwa kina cha maji katika Bwawa hilo hata baada ya kituo hicho kulazimika kuzalisha umeme chini ya mita za ujazo zinazoruhusiwa kitaalam.

HABARI SIYO GESI TENA, SASA NI HAKUNA MVUA NA MTERA IMEKAUKA...TUMESAHAU GESI TUNAANZA KUWA NA HURUMA NA SERIKALI KWELI HAKUNA MVUA.

ALIYENUNUA KIWIRA KINYEMELA KAKOSA DEAL LA KUUZIA UMEME TANESCO NA WATAHAKIKISHA INAKUFA KAMA GENERAL TYRES NA VIWANDA VINGINE ANA ANADIRIKI KUITA WATANZANIA MALOFA
 
Mkuu dkn, naomba hako kalike kamoja nilikokugongea ukazidishe mara million moja na Mungu akubatiki sana maana kitu ulichotuwekea hapa nilikuwa naktafakari lakini wewe umekileta na data za kutosheleza.
Katika ufuatiliaji wangu wa hili swala nahisi kuna vichaa either kati ya sisi tunaosililiza hizi habari au wanaotueleza!

Hii nchi tukubaliande na mgombea urais wa TLP kuwa kuna kitu kikubwa kitatokea sooner; maana hata Mtera maji yameisha lakini kuna ya akiba kidogo yamdebaki lakini waliopewa madaraka wameishiwa akili zote hata za akiba hakuna!
 
mlikomalia prof. mhongo aondoke kisa watu wanataka kuafanya udalali wa vitalu vya gesi haya ndio matokeo yake

Namkubali Prof. Mhongo kwa utendaji sema siasa ya Tanzania bila kusema uongo serikali ndani ya CCM huendi mahali na yeye alikuwa smart na mtu wa facts pia hakuwa na kipawa cha kuongea na watu wa kawaida..yuko academic sana. Kaingizwa chaka na wenye serikali kwenye rushwa na kapoteza sifa nzuri aliyokuwa nayo kiutendaji sehemu alizokuwa.
 
Mkuu dkn, naomba hako kalike kamoja nilikokugongea ukazidishe mara million moja na Mungu akubatiki sana maana kitu ulichotuwekea hapa nilikuwa naktafakari lakini wewe umekileta na data za kutosheleza.
Katika ufuatiliaji wangu wa hili swala nahisi kuna vichaa either kati ya sisi tunaosililiza hizi habari au wanaotueleza!

Hii nchi tukubaliande na mgombea urais wa TLP kuwa kuna kitu kikubwa kitatokea sooner; maana hata Mtera maji yameisha lakini kuna ya akiba kidogo yamdebaki lakini waliopewa madaraka wameishiwa akili zote hata za akiba hakuna!

Mkuu hili ni shamba la bibi kweli haingii akilini Waziri anasema haya tarehe 19 Septemba hata mwezi haujaisha serikali itashusha bei ya umeme, leo tunaambiwa hakuna umeme tatizo mvua. Gesi tungeambiwa suala la kiufundi lakini umeshasema majaribio yamefanyika na gesi inafika sawa sasa uongo umefika mwisho
 
Mkuu hili ni shamba la bibi kweli haingii akilini Waziri anasema haya tarehe 19 Septemba hata mwezi haujaisha serikali itashusha bei ya umeme, leo tunaambiwa hakuna umeme tatizo mvua. Gesi tungeambiwa suala la kiufundi lakini umeshasema majaribio yamefanyika na gesi inafika sawa sasa uongo umefika mwisho

Wakuu mimi nadhani haya yote yanatokea ili andiko litimie yaaani "CCM IONDOKE COME OCTOBER 25TH". Nyani akitaka kufa miti yote huteleza siku hiyo. Nadhani Mungu anaruhusu haya yote yatokeee ili watz wajue kwamba n muda wa kuipumzisha hiki chama cha zamani.
 
Unajuwa hii nchi inaendeshwa kisanii, tarehe 6 February 2007 siku ya jumanne Dr shein alitembelea mtera name akasema mwisho was kutegemea mvua imekaribia ifikapo mwaka 2012 Tanzania hatokuwa tegemezi kwa uzalishaji was maji yaani mabwawa, leo mwaka 2015 tunazalisha megawatts 108 kati ya 800. Inasikitisha sana,lini tutakuwa ni nchi yenye kujifunza na makosa na kusimamia kauli tunayotoa? Hii ni kauli yake kipindi hicho
-Endapo mikakati hiyo itafanikiwa, ndani ya miaka mitano ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete, Tanzania
itaweza kupata megawati 928 za umeme karibu mara mbili ya umeme unaohitajika nchini.
Sasa leo hii tunayo 108.
 
Christmas ikifika hata hiyo mitambo itakuwa imezimwa.

Inabidi wapunguze bei mishumaa na mafuta ya taa.
 
Halafu eti yanakuja mazee yaliyosemwa yanasubiri kufa yanatudanganya tuendelee kuiamini ccm? Butiku na genge lako lile nyoko mtuache RAIA tuamue kwa Uhuru, awamu yenu ilishapita sasa ni zamu ya vijana kuamua hatima yao, nyie kwa vile mnasubiri kufa kaeni pembeni hii ngoma tuicheze wenyewe!!
 
Nchi itarudi kwenye uchumi wa kuni na mkaa .uchumi wa gesi hautamkwi tena,je ni mwanzo au mwisho wa hadithi za serikali ya ccm?
 
Namkubali Prof. Mhongo kwa utendaji sema siasa ya Tanzania bila kusema uongo serikali ndani ya CCM huendi mahali na yeye alikuwa smart na mtu wa facts pia hakuwa na kipawa cha kuongea na watu wa kawaida..yuko academic sana. Kaingizwa chaka na wenye serikali kwenye rushwa na kapoteza sifa nzuri aliyokuwa nayo kiutendaji sehemu alizokuwa.
Unadhan angekuwepo mabwawa yabgejaa maji?chini ya Muhongo umeme tuliujosa pia,hata wakat wa eskro saga tuliukosa
 
Poor simbachawene,unatumika vibaya sana,kauli zako zako tu zinaonyesha huna maamuzi yoyote na wizara uliyo kabidhiwa,mara mradi ni wa serikali mara mradi ni wa watu binafsi,hizi week mbili ziishe tu tuwakate muwe historia,lowassa will overhaul tanesco yote na kupitia mikataba ya kipumbavu mliyoingia,
 
kila siku mgao ,biashar nyingi town znategmea umem.. sas maendleo yataptikan vip kw hali hii ,kam umeshindwa kaz we wajibika t kiroh safi.
 
Eeehh subirini mipango ya jopo lililoundwa kupendekeza mapendekezo kwa mgombea urais ambaye ameshajua atashinda ila hajui akifika ikulu atafanya nini hadi asome hayo mapendekezo akremu then aunde tena jopo baraza la kutekeleza na pia aunde na baraza la ufuatiliaji baraza la kusimamia na kuhakiki utekelezaji naiona serikali ya mipangoo inakuja
 
naomba mungu maji yakauke kabisa tuingie giza nchi nzima ili tufanye maamuzi sahihi
 
LB7 njooni mujibu facts hapa kama kweli nyinyi ni wazalendo. Nina uhakika hapa hamuwezi tia miguu maana mmekalia majungu tu na unafiki. Mae.....
 
Back
Top Bottom