Kauli ya Serekali yashangaza wananchi wa Bagamoyo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Bagamoyo. Zaidi ya kaya 900 zinazozungukwa na shamba la mradi mkubwa wa kilimo cha miwa wilayani Bagamoyo (Eco Energy) wamesema wamepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kusitishwa kwa mradi huo iliyotolewa bungeni na Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa, wakisema hawajalipwa fidia na hawajui hatima yao.

Katibu wa Kamati ya HakiArdhi ya Bagamoyo (Bagamoyo Land Right Task Force), Jumanne Salumu amesema kwa niaba ya wananchi yao kuwa kabla ya kusitishwa mradi huo, Serikali ilipaswa iwashirikishe na kutoa maelekezo ya umikili wa ardhi hiyo unakuwa wa nani baada ya mradi kusitishwa.

Wamesema kitendo cha Serikali kusitisha mradi bila ya kuwashirikisha ni kuwaacha hewani na kuibua mgogoro.

Waziri Mkuu alitoa taarifa hiyo wakati akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Freeman Mboye alilouliza Mei 19 kutaka kujua sababu zinazosababisha Serikali kushindwa kuweka jitihada za makusudi katika kuhakikisha mradi huo wa miwa unatekelezwa kikamilifu kwa lengo la kupunguza au kuondoa tatizo la uhaba wa sukari nchini.

Katika majibu yake, Majaliwa alisema Serikali imeamua kusitisha mradi huo kwa sababu ungetumia sehemu kubwa ya maji ya Mto Wami hivyo kuathiri ustawi wa Hifadhi ya Saadan na wanyama wenyewe.
 
Kwa kweli kama Rahisi tunaye! Hivi hana washauri au hashauriki? Mbona Mbona kauli tata kila siku? Hakuna kitu ana toa suluhisho sahihi an nini? A shida gani?
 
Yaani hata watumishi sasa wako makini na vyombo vya habari maana matamko yanatoka bila wahusika kujua.
Ukitaka kujua kesho yako lazima uwe karibu na Chombo cha habari
 
Back
Top Bottom