Kauli ya Rais wa China kuhusu kinachoendelea Libya

Dumelambegu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,052
257
Rais wa Jamhuri ya Watu wa China amepinga mashambulizi yanayofanywa na nchi za magharibi nchini Libya kwa kisingizio cha kudhibiti a 'non fly zone'. Amesema makubaliano yaliyofikiwa na UN kuhusu Libya yalilenga kuepusha mauaji zaidi ya raia wasio na hatia lakini majeshi ya nchi magharibi yanafanya kinyume.

Chanzo cha Habari: Aljazeera.
 
Huyu rais wa china hana jipya,maana alikuwa na uwezo wa kutumia kura ya veto kupinga uvamizi....
 
China siyo nchi ya kidemokrasia. Ni nchi ya kibabe, sera zao ni kuvuna kilichowaleta katika nchi bila kuangalia kama wananchi wanaathirika vipi na hiyo pesa au misaada wanayotoa katika nchi husika. Mfano mzuri ni Sudan, wakati wanavuna mafuta na kutoa misaada ya silaha za kivita kwa serikali ili iue wananchi wake wao kwao ni chereko tu. Kwa hiyo china kuna uwezekano ikaja kulipuka kama Misri au Tunisia.
 
China siyo nchi ya kidemokrasia. Ni nchi ya kibabe, sera zao ni kuvuna kilichowaleta katika nchi bila kuangalia kama wananchi wanaathirika vipi na hiyo pesa au misaada wanayotoa katika nchi husika. Mfano mzuri ni Sudan, wakati wanavuna mafuta na kutoa misaada ya silaha za kivita kwa serikali ili iue wananchi wake wao kwao ni chereko tu. Kwa hiyo china kuna uwezekano ikaja kulipuka kama Misri au Tunisia.

We unafuata propaganda za Magharibi, Ili nchi kulipuka hutokana na raia kutokuridhika na hali ya maisha, Wachina wanajitahidi katika kuboresha mazingira ya wananchi wake kujichumia, huo uhuru ambao unasema haupo ni kelele za magharibi tu, wachina wa kawaida wanaishi kwa uhuru walioridhika nao na wanawachukia sana wamarekani kisera na wanajua migogoro yote inayotokea ulimwenguni kuna mkono wa Marekani. Ila wanapenda kwenda US kusoma, wanapenda bidhaa zao n.k.
Kiufupi tu hakuna mchina mwenye akili ya kuandamana, kila mtu yuko bize kutafuta mshiko,na serikali inamuwezesha, hivyo haoni sababu ya kulumbana na serikali, isipokuwa kwenye majimbo yanayokaliwa na waislam, maana kama walivyo waislama wa bongo nao wanahisi kuachwa nyuma.
Hakuna nchi ambayo imethibiti public security kama China, na wananchi wanaamnini sana polisi,kitu kidogo tu wanaita polisi. Kwa hiyo kutokea ya Tunisia ni ndoto ya mchana wanayoiota US na Ulaya.
Turudi kwenye suala ya Libya,hata mimi naona ni unafiki kutoa kauli wakati ulikuwa na uwezo wa ku-veto, Lakini hasara za kuveto zingekuwa kubwa kiasi gani ukizingatia mataifa ya waarabu wamekubali,na haijulikani upepo utaendaje, anyway, No-fly zone sawa naikubali lakini kuna azimio jingine la UN kuhusu silaha kuingia Libya,sasa tunaona nofly zone inakuwa kuattack majeshi ya serikali ili kusafisha njia kwa waasi, halafu wanaenda mbali zaidi kufkiria kuapa waasi silaha, huko siyoi kukiuka azimio la UN la marufuku ya silaha kuingia Libya?.Kutumia kisingizio cha "all necessary means to protect civilians" kuhalalisha kutoa silaha kwa waasi si sahihi hata kidogo. Naona maazimio ya UN yanakuwa mazuri kama yanawafaidisha mataifa ya Magharibi, lakini yakiwageuka wao yanakuwa mabaya na yanatolewa tafsiri tofauti.

Ndiyo maana nchi kama North Korea inamiliki nuke kama njia ya kujikinga, kama si hivyo labda ingeshaundiwa zengwe na kushambuliwa.

NB: Simuungi mkono Ghadafi,naunga mkono njia za mazungumzo kama suluhu. That means for the moment a cease fire is needed.
 
Jamani mechi ya Yanga na Azam ilikuwaje? Na India na Pakstan kwenye cricket vipi?
 
Back
Top Bottom