Kauli ya rais kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya rais kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kibagata, Oct 14, 2012.

 1. K

  Kibagata JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 773
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Kauli aliyoitoa Mkuu wa kaya leo kuwa YULE MTOTO KUKOJOLEA MSAAFU NI KOSA KUBWA SANA. hili ni kosa kama KIIMANI AU KISHERIA na kama ni kiimani then kwa KATIBA IPI maake kauli ya Mkuu wa nchi mara nyingi iendane na sheria za nchi na kikatiba. Kwa hali ya kawaida ni kosa kuingiza imani katika kuongoza nchi. NCHI SI MAHAKAMA YA KADHI kutoa kauli kama hiyo. TUJADILI
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Sitaki kujadili mambo ya JK ...soo mean
   
 3. F

  Fursa Pesa JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 2,324
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  kukojolea vitabu vitakatifu ni kosa kubwa,ila inapotokea mtoto kuikojolea si kosa kwa mtoto bali ni kwa mzazi/mlezi wake.katika hili kuna mapungufu ya utunzaji wa vitu katika kaya zetu hasa biblia,masaafu.na wakati mwingine biblia ama msaafu huo kutumika kwa wazazi/walezi katika siku maalum tu na si vinginevyo,hii unjengea mtoto kudhalaudhalau tu vitabu hivi na pengine anapovichukua mzazi/mlezi umtizama tu.kwa wale ambao ni waumini wa kweli hakuna hata kipande kimoja katika vitabu vyao kitaharibika,lakini kwa wale ambao si waumini wa kweli hii kuchoma vitabu hivi itaendelea tu.rai yangu kwa ndugu zangu wote yatupasa kutunza vitabu vyetu na kuvisoma mara kwa mara.
   
 4. Kiba

  Kiba JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 453
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hakika miongoni mwa mbulula ambao sijadiligi wala siangali picha yake ni jamaa. embu aweke wazi kifungu ?
   
 5. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Kibongo bongo, baba mzazi wa mtoto aliyekojolewa anakua celebrit, sitashangaa clouds na earadio wakampa airtime, kama yule aliyeangika mashairi ya bongo fleva.
   
 6. O-man

  O-man JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 318
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kwa mimi binafsi, kitendo hiki sikukipenda. Kibaya zaidi namfahamu baba yake. Ni mtu mwenye heshima na ni mnyenyekevu kwa marika yote. Namuomba Mungu aendelee kumuongoza katika shughuli zake za kila siku na kwa hili linalomkabili sasa. Asimhukumu mtoto kwa jazba ila kwa maono na mafundisho sahihi.
   
 7. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo mtoa mada , kama hili umeliona si kosa hadi tulijadili , for another hand ungependa huyo mtoto tumpongeze?
   
 8. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inawezekana Halipo kwenye katiba kama unavyotaka wewe, Lakini jambo lolote lile (dogo au kubwa , kwakutenda au kuzungumza) ambalo linaloweza kupelekea kuvuruga kwa amani ni KOSA KUBWA ..
   
 9. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mi sina muda wa kumsikiliza kilaza Dhaifu.
   
 10. m

  majege Senior Member

  #10
  Oct 14, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35

  Kwanza nikupongeze mleta uzi huu.
  Kwa upande wangu nilitegemea mkuu wa kaya angekuwa na maneno mengi tu ya kuongea kama mkuu wa nchi kwani imemchukua muda wa kutosha kwa yeye kutafakari, kushauriwa na kujipanga kutoa kauli madhubuti kama mkuu wa nchi. cha ajabu kauli aliyotoa ni kama mtu aliye kurupushwa kutoka usingizini na amesahau kuwa yeye ni kiongozi mkuu wa nchi au kama mtu wa mtaani tu kama hao wahuni walioshiriki kuchoma makanisa na kuleta vurugu zilizotokea.
  Naomba niende mbali kidogo, Jk anataka kutuaminisha kwamba kuwa kiongozi mkuu wa taifa huhitaji kuwa na uwezo wa ziada wa akili, maono na ushauri na badala yake tuone kwamba haina shida mtu yoyote anaweza kuwa raisi.

  Haiingii akilini mtu kukosa kutoa kauli au kalipio katika hili unless yeye kawatuma kufanya yaliyo tokea.

  Kiapo chake kama Raisi ni kulinda katiba na sheria za nchi kwa gharama yoyote kitu ambacho no tafuti na kauli nyepesi isiyo na uzito na maono kama aliyotoa yeye.

  La mwisho naomba wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari mtusaidie watanzania kwani tunakoenda siko. mtengeneze agenda ya pamoja ya kunusuru amani inayotaka kutoweka tu kwa sababu ya kuwa na jamii inayoshabikia uharamia/Maovu kwani viongozi wetu wamelewa madaraka na kusahau wajibu wao kwa jamii na kujihisi kuwa wao siyo waathirika wa janga hili.
   
 11. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mtoto kakosea!!! Lakini ukweli unabaki... Je huyo mtoto mdogo (under 18) alijua imani na miiko ya waislamu????? Nani alimfundisha? Kisaikolojia huo unaitwa umri wa kudadisi (the age of curiosity) na ni sehemu ya mtoto yeyote kukua!! Tunaye rais goigoi, hoi, mdini, mwendawazimu na mpumbavu!!!!! Nina hasira ... nasubiri ban!!!!! Potelea mbali!!!
   
 12. k

  kapongoliso JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,136
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Mkuu wa nchi ameonyesha udhaifu mkubwa katika kushughulikia suala la Waislam kuharibu makanisa kule Mbagala. Eti anawaambia wakristu wasilipize kisasi. Waislamu walilipiza kisasi kwa tatizo alilofanya mtoto, hawakukatazwa ila wakristo ndo wanakatazwa. Rais mwenye ndimi mbili (double standard).Anasema mtoto alifanya kosa kubwa kunajisi korani, kwani huyo mtoto anajua korani nini? Mkulu anafikiri nchi hii wote wanatakiwa wawe waislam. Haya makkanisa kule Zakheim yalihusika nini na matukio ya Kizuiani? Huyo mkulu ni mdini namba one na kila siku amekuwa anatetea waislam kwa kila ujinga wanaotenda. Wanadharau polisi pale kidongo chekundu, jamaa akuwaonya, wakaandamana hadi mambo ya ndani akawakataza polisi wasiwapige kwa sababu sio CDM, wakadai waliokataa sensa waachiwe bila masharti, kweli ikawa hivyo, leo wameharibu makanisa jamaa anchekacheka tu, wameahiddi kwenda NECTA, wanachekewa tu. Akiambiwa dhaifu, goigoi, mbaguzi, anakasirika. Kumpeleka yule dogo mahakamani ni kujidhalilisha tu, tumeona wakina kamuhanda wanauua kule Nyololo wapo mitaani, watu wanaiba hadi serikali yake imefilisika, hawajapelekwa mahakamani. Unashupalia kesi ya kitoto(minor) ili upate umaarufu kwa waislamu mdini mkubwa.
   
 13. s

  structuralist JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,209
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Kwanza na declare imani yangu thabiti ya uisalam. Unafikiri angekuwa raisi mkrisito angeunga mkono hicho kitendo? Pili naunga mkono kitendo cha rais kukemea kitendo cha huyo dogo kukojolea msahafu kwasababu hilo jambo halikubaliki. Yani wewe ulikuwa unataka raisi ashangilie? Au ampongeze? Ingekuwa kitabu cha imani yako kimekojolewa na rais akatoa hilo tamko ungechukia? Rais alipaswa kukemea hicho kitendo na hatakama isingekuwa msahafu bado angelazimika kufanya hivyo. Ishu ya tatu ni kwamba raisi alikemea tabia ya kuwa na jaziba na kuchoma makanisa,mbona hilo husemi? Binafsi nalaani kabisa kitendo cha kukojolea msahafu lakini pia kwa dhati kabisa na laani kitendo cha kuchoma moto makanisa kwani hili si sawa na halikubaliki hata kidogo. Naomba tuache ushabiki usio na tija kili mtu aheshimu imani ya mwenzake bila kuweka vichocheo vya chuki. Hatuhitaji kulea vijana wasio heshimu vitabu vya imani nyingine na watu wasio heshimu nyumba za ibada za watu wengine.
   
Loading...