Kauli ya Rais Kikwete isipotoshwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya Rais Kikwete isipotoshwe

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ntemi Kazwile, Aug 11, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mhariri wa HabariLeo amekuja na mpya baada ya kuacha kazi yake ya kuutumikia umma wa Watanzania (wanaolipa mshahara wake) na kujivika ukada wa CCM kumtetea JK. Mimi niliisikiliza kwa ufasaha hotuba ya Kikwete na alikuwa wazi kabisa kuwa wafanyakazi na Tucta hawambabaishi na alienda mbali zaidi kwa kuwatishia uhai wao wale wote ambao wangevunja amri ya serikali ya kutogoma akitoa mifano ya jinsi serikali ilivyoweza kuwaua wale waliojihusisha na migomo ambayo serikali iliita haramu.. vipi leo hii anaanza kuyameza maneno yake? Anatumia vyombo vya habari vya serikali kumtetea ili kuwalaghai wafanyakazi? tunasema mwaka huu ng'o! Mlitulaghai na vyombo vyenu fake mwaka 2005 safari hii tafuteni mbinu nyingine
   
 2. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hao HabariLeo si waganga njaa tu!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Pamoja na ukada wa CCM wa huyo mhariri, safari hii CCM watajirajie kujibeba -- tena kikwelikweli. Naona itaki\uwa kama usemi ule unaosema siku ya nyani ikifika basi kila mti huteleza. Hiki kijarida cha kufungia mandazi na akina mama-lishe (sitanii kabisa hapa) hakiwezi kutuvuruga sote tunatoka kujikomboa kutoka makucha ya mafisadi.
   
 4. B

  BENSON MSEMWA Member

  #4
  Aug 11, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tena alienda mbali zaidi na kuwaita wanafiki,waongo,wazindaki,wafitini,
  mbona jk atajibeba mwaka huu na tucta hakuna kulegeza kamba ni mwaka wa mabadiliko
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Watatafuta pa kushikilia wasipaone!...Mi naomba tshirts za "SIHITAJI KURA ZA WAFANYAKAZI" zije huku mkoani watu wazivae hadi siku ya uchaguzi!
  Wameona maji ya shingo wanaanza kutubembeleza:smile-big:..Hatudanganyiki!
   
 6. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #6
  Aug 12, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Huyu Mhariri wa Habari Leo,sometimes I think he is lacking in profound meditation. Ile hotuba aliyotoa JK Diamond Jubilee Hall kwa wazee wa Dar es Salaam ilikuwa speech kali ingawa hakusema kwamba anataka kumuua mtu yoyote. Lakin kama nilivyoandika pale kwanza,kwamba ''it was a Stalinistic speech'' na kwamba wafanyakazi wangegoma,wakuu wao wangeitwa Cenrtal Police Station to sign a confession that they were instigated by Foreign Counter-Revolutionary powers.
  What I did not like about that speech ni jinsi yule Mkuu wa Mkoa,William Lukuvi alivyokuwa anashabikia wakati JK anazungumza,kama vile yeye ndiye aliyemchochea JK kusema maneno yale yote. Halafu what was surprising about that speech ni jinsi ambavyo kesho yake,baada ya kutoa ile hotuba kuwafokea wafanyakazi,jinsi JK alivyokuwa fawning,sycophantic,obsequious,alipokuwa anaongea na dignitaries waliokuja katika World Economic Forum for Africa. Imekuwa kama vile JK ana dual personality,vigumu kuamini huyu anaongea hivi leo,ndiye aliyeongea vile jana.
  Lakini yale mambo yameongewa zamani na sasa I think the bitterness has passed,na ule mgomo,I don't know what happenned to it,naona kama vile ule mgomo umeyayuka. Lakini wafanyakazi wanaweza kuelezwa maneno yale yale John the Baptist aliyowaambia askari,kwamba waridhike na mshahara wao,wasiwe na tamaa.
   
 7. T

  Taso JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  repetitive
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Rais Kikwete alitakiwa kusema hivi:

  mwenzetu akatoka kwenye script na kusema kura za kina hazitaki!!!
   
 9. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Semeni polepole lakini fanyeni kwa nguvu sana kuandika NO kumpa kura. Mbona yeye yuko kimya tunasikia wapambe tu? Yeye kakubali kwamba yasemwayo ndiyo yaliyosemwa na alisema yuko tayari kwa lolote. Sasa kupiga makelele maana yake nini kama sio mnaogopa fimbo yake? Mnyimeni kama alivyoomba, wapeni wanaozitaka kura zenu! Mbona mnambembeleza kumpa kura hizo? Alishajua anazo kura za kumtosha kuendelea kukaa jengo kuu lile hata bila kura za wafanyakazi milioni tatu, wake zao na waume zao, watoto wao wapwa zao shangazi zao marafiki , wachumba, washenga, maconcubine, nyumba ndogondogo na kubwakubwa.......... alijua network ya mfanyakazi na impact katika kura zao.

  Kama wafanyakazi kweli mnao umoja na wala hamkutaka kumchomekea Mgaya na tucta yake, basi mnyimeni kura JK na waambieni ndugu zenu, jamaa zenu na marafiki zenu woooote kabisa wasimpe kura kwa kuwa watu hao wanaathirika pia kutokana na kuathirika kwako mfanyakazi. Kampeni ya maana ni kuwakumbusha hao jamaa zenu wasisahau kumnyima kura.

  Kadiri mnavyolalamika inaashiria kushindwa kwenu katika kuainisha dharau mnazopewa na viongozi wenu na kukubali yaishe kwa kuwa mnaamini kwamba hamna jinsi ili kuishi mpaka JK peke yake afurahie kuiona kwenu kesho. Nyie mnategemea wapambe wake waseme nini, si ni mkakati wa kufuta matapishi? Threads zingine zimeonyesha kwamba huyu bwana hawezi kutafakari na kujibu mambo yanayohitaji akili nyingi papo hapo, mpaka avute nzoke kutoka wapambe wake. Pale alipokuwa anasema hakuwa anasoma kwenye nzoke, mengi aliyaongea ya kwake mwenyewe kutoka ndani kabisa ya moyo wake. Hayo ndiyo yenye maana yanayomuonyesha rangi yake ya kweli ya asili. Utajua kwamba hajapewa mkoba na wapambe utakapoona anapoongea ana kigugumizi mara kwa mara.

  hata mahakamani waendesha mashitaka wanatumia mbinu ya kukuchokoza ukasirike halafu uyaseme kwa hasira maneno yaliyomo moyoni mwako na ndipo watajua ukweli wa kile wanachokitafuta kutoka kwako. Simple psychology.
   
 10. F

  Froida JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mbali zaidi alikwenda kama Amiri Jeshi Mkuu alikuwepo Mkuu wa Majeshi ya Tanzania,Mwamunyange,Mkuu wa jeshi La Polisi Saidi Mwema na Mkuu wa Jeshi La Magereza,alikuwa anatangaza vita na wafanyakazi,lazima aadhibiwe kwa Kitendo hatarishi kama hicho huwezi kutishia watu na kutaka wafyate midomo wanapoidai haki zao wakiwa hawajavunja sheria yeyote ya nchi na wakiwa wakitimiza waajibu wao kikatiba,TUCTA tuko nyuma yenu kwa lolote mtakalosema
   
Loading...