Kauli ya Nikki wa Pili juu ya muziki wa bongo

SBAKARI

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
355
289
NIKK WA PILI ASEMA WEUSI HAWAUI MUZIKI, AWAHUSISHA ASLAY NA DIAMOND PLATNUMZ .

Msanii wa muziki kutoka Kundi la Weusi, Nikki wa Pili amesema anasikitishwa na propaganda za wasanii wenzake pamoja na mashabiki wanaodai kuwa wanaharibu muziki kwa kutoa nyimbo mara kwa mara .

Mkali huyo wa 'quality time' ameeleza hayo na kuwataka watanzania washeherekee pale msanii anapotoa hits nyingi ndani ya kipindi kifupi na sio kumwambia anaua muziki .

"Cha kwanza niseme nasikitishwa na feedback kwasababu kama weusi wanaweza kupiga hits tano ndani ya miezi miwili katika diversity yani ukisikiliza 'Luck me' ni tofauti na 'Nuru' ni tofauti na 'Quality Time' ni tofauti na 'Madaraka ya Kulevya' ni tofauti na 'Dude' ni tofauti na 'Kataa leta' ndani ya miezi mitatu watu wanaweza kufanya kitu kama hicho nilifikiri kwamba ingepokelewa kama Mwanafunzi aliyepata 'A' saba, nilifikiri watu wataangalia katika ukubwa huo watu wataangalia Art kwamba imewezekanaje hawa watu wameweza kupiga sound sita tofauti floo, melody, ubunifu, content tofauti katika kila nyimbo nilifikiri watu watasheherekea Art" alisema @nikkwapili .

"kama kawaida ya watanzania wanapindisha ukweli kwahiyo kitu kikubwa kwenye hiyo sanaa haizungumzwi watu wanazungumza ooh weusi wanatoa nyimbo wanaua nyimbo zao ongelea creativity unaacha kuongelea big point unaongelea kuua, unawezaje kuua hits..? Eeh! Kuna wasanii wangapi mwaka huu wametoa hata nyimbo nne mpaka sasa hazijasikika, hao je wameua nyimbo zao au? Hiyo hoja kwangu naona haina mashiko"ameongeza .

Katika hatua nyingine Nikk wa pili amesema "kama dogo @Aslayisihaka amepiga hits 3 ndio vitu vya kuongea huyu mtoto mdogo anapiga hits 3 ndani ya miezi miwili ndio vitu vya kusifia @diamondplatnumz ametoa ngoma 3 video kubwa ndio vitu vya kuongea namna Artist alivyowekeza video kubwa 3 ndani ya miezi miwili ndio vitu vya kusifia tusilete politics tusivunje mioyo watu wanaofanya kazi"
[HASHTAG]#letitshinenewz[/HASHTAG]
 
Manyimbo ya weusi yote mabaya. Mziki ukiwa mzuri utapendwa tu mbona zamani mlikuwa mnatoa nyimbo nyingi na zote zinapendwa unalazimishaje watu wapende kisichowavutia... Niki kubalini mziki wenu umeisha watu awawaelewi.
 
yaan kauli yako inaonyesha jins gani umetoa mtima nyongo
 
Kwa maoni yangu naona wanaokosoa wako sawa, unajua muziki ni kama chakula, ukila sana cha aina moja kinakinai hivyo kama mnataka kuendelea kusurvive wapeni gap mashabiki wenu wale kwa kujinafasi, kutoa nyimbo mara kwa mara inaweza hisiwa ni dalili ya kutojiamini, huyo Diamond unayemtolea mfano nyimbo zake hazifanyi vizuri kivile, Aslay namuelewa kwanini anafanya hivyo, ni kwavile anahitaji kujitengenezea himaya yake kama solo artist, yaani ukimwita kwenye show awe na nyimbo za kutosha zinazofahamika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapo mwishon nimekuelewa sana
 
Yatoeni tu as long as yanawaingizia pesa maana sisidhani kama lengo ni kuwafurahisha mashabiki bila nyie ku make pesa.
Yatoeni tu maana muda wenu ukipita yaliyibaki studio hakuna atakaye taka kuyasikiliza.
Toa ngoma watu waenjoy tengeneza pesa
 
hahahaha
 
Nikki nae saa zingine sijui anakuaje!! Anakuwa kama vile hajui maana ya hit song!!
 
Back
Top Bottom