Kauli ya naibu spika kuhusu kitendo cha wabunge wa upinzani kususia mijadala ya bunge la bajeti huku wakiendelea kupokea posho
Naibu spika wa bunge, Dk Tulia Ackson leo ametoa mwongozo uliombwa na mbunge wa Nkasi kaskazini, Ally Keissy na waziri wa katiba na sheria, Dk Harisson George Mwakyembe waliotaka kujua kama ni alali kwa wabunge wa kambi ya upinzani kuendelea kulipwa posho wakati wanaingia bungeni asubuhi wanasaini na kuondoka, ilihali wanalipwa posho na mishahara.
Na hii kauli ya naibu spika kuhusu mwongozo huo:
Kutokana na uamuzi uliowahi kutolewa na bunge hili wa tarehe 27 Aprili, 2016 kuhusu mwongozo wa spika unaofanana na ulioombwa na waheshimiwa wabunge hao wawili, ambao uliombwa na mhe. Hussein mohamed Bashe (mb) ambaye aliuliza kuhusu usahihi wa wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kulipwa posho na mishahara wakati hawashiriki na kutimiza wajibu wao wa kuchangia kwenye mjadala wa bunge la bajeti. Katika kujibu mwongozo wa mhe. Bashe kiti kilinukuu ibara ya 73 ya katiba inayosema:-
“73. Wabunge wote wa aina zote watashika madaraka yao kwa mujibu wa katiba hii na watalipwa mshahara, posho na malipo mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na bunge”.
Kiti kiliendelea kutoa uamuzi wake kama ifuatavyo:-
“masharti ya kazi ya mbunge yameeleza kwamba mbunge anastahili kulipwa mshahara kwa kila mwezi. Aidha, masharti hayo yametoa ufafanuzi kuwa “mbunge anapohudhuria vikao vya bunge na kamati zake atalipwa posho ya vikao kwa kiwango kitakachowekwa na serikali kwa kuzingatia sheria ya fedha za umma na kanuni zake na masharti ya kanuni za bunge kuhusu vikao.
Malipo ya mshahara kwa mbunge ni suala la kikatiba na sheria. Malipo hayo hulipwa kwa mbunge kutokana na kazi yake ya ubunge kama ilivyotajwa katika ibara ya 73 ya katiba.
Malipo ya posho kwa mbunge yameanzishwa kwa mujibu wa katiba na pia yamewekwa katika sheria ya uendeshaji bunge, sura ya 115 chini ya kifungu cha 19. Utaratibu unaotakiwa kuzingatiwa umefafanuliwa kwenye waraka wa rais wenye masharti ya kazi ya mbunge yaliyoanza kutumika tarehe 25 Oktoba, 2010 na marekebisho yake ya tarehe 11 Juni, 2012 ambayo kwa pamoja yanaeleza kwamba, mbunge anapohudhuria vikao vya bunge na kamati zake atalipwa posho ya vikao kwa kiwango kitakachowekwa kwa kuzingatia sheria ya fedha, kanuni zake na masharti ya kanuni za bunge kuhusu vikao”.
Kwa kuwa mbunge anatakiwa kulipwa mshahara au posho kutokana na kuhudhuria na kushiriki katika mijadala bungeni, na kwa kuwa wabunge ni wawakilishi wa wananchi katika kuisimamia serikali, kutohudhuria bungeni na kususia kutoa mchango wake wa mawazo ni kushindwa kutimiza wajibu wake huo wa kibunge. Pia si sahihi wala halali kwa mbunge kupokea posho na mshahara bila ya kufanya kazi.
Kama kiti kilivyoamua katika uamuzi nilioutaja, vitendo hivi vya kutoka ukumbini makusudi baada ya kujisajili havikubaliki.
Nazidi kusisitiza kuwa ipo haja ya siku zijazo kurekebisha sheria tulizonazo ili kukabiliana na hali ya namna hii na kuweka utaratibu mahsusi utakaowezesha kila mbunge kulipwa posho baada ya kutekeleza majukumu yake ipasavyo na sio kuandika kuhudhuria katika mkutano na vikao pekee
Huo ndio mwongozo wangu.
Chanzo: Mwananchi
Maoni yangu: Sikutegemea kama waziri wa katiba na sheria angeomba mwongozo kama huu kwa jambo ambalo lipo kisheria na kikatiba