Kauli ya Mwapachu Kuhusu Lowassa

Kauli ya Mwapachu Kuhusu Lowassa

Bukanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2010
Posts
2,857
Reaction score
1,937
Ndugu zangu,

Nimekuwa kimya kwa muda mrefu katika mabadilishano ya fikra kwenye mtandao huu ambao kwa hakika, kwa maoni yangu, haubidi kuwa ni wa fikra pevu zisizo shawishika na misimamo ya 'kimalaya ya siasa'. Kama tutaserereka katika msingi huu, basi ni bora Chambi ukafunga virago na kusitish huu mtandao. Nimesoma mabadilishano na mabishano ya fikra kuhusu hali ya siasa nchini mwetu na hususan baada ya Mhe Lowassa kuamua kujiunga na Chadema na kuwa mwakilishi wa UKAWA katika kinyang'ariro cha nafasi ya Urais wa Jamhuri yetu ya Muungano. Sijui nyie wenzangu mmesimama au mmesimamia wapi katika suala hili.

Naomba niseme mwanzoni kabisa kwamba nchi yetu hii leo imefikia mahali ambapo wasomo, wanazuoni kama sisi katika mtandao huu, Hatuna budi kujitokeza na kuhesabika tunamuunga nani mkono katika uchaguzi ujao wa Rais wa Tanzania. Tuwe wakweli na siyo kuendelea kuegemea katika kificho cha 'uhuru' wa wanazuoni katika kutoa maomi na fikra kama vile sisi si wapiga kura au wananchi wanaothamini umuhimu kuhusu uongozi wa nchi yetu. Wakati huo umepitwa na hali halisi ya itikadi na maana muhimu ya uongozi wa Taifa.

Sasa, Mimi binafsi, namuuunga mkono Edward Ngoyai Lowassa. Yako mengi ambayo kazuliwa huyu ndugu yetu; tunaambiwa tangu 1995 wakati Mwalimi Juluis Nyerere alipo tamka kwamba 'huyu kijana ninalo file lake; ana utajiri usiyoelezeka. Ana nyumba kadhaa.' Lakini huyo huyo Baba wa Taifa alimpenda sana Edward na kumpa madaraka ndani ya CCM na baraza la mawaziri. Kama Edward alikwa 'corrupt' swali ni kwaninini Baba wa Taifa hakumchukulia hatua za kisiasa na kisheria? Kwanini aseme hayo aliyoyasema mwaka 1995 wakati Edward Lowassa alikuwa akiongoza kupendwa dani ya CCM, ngazi zote na akitarajiwa ndiye angependekezwa kuw mgombea wa Urais? Jamani, wanazuoni, lazima mtafakari historia na hali halisi ilivyokuwa. Mhe Jakaya Kikwete hakuwa 'the favourite' candidate in 1995. Na Mwalimu alimtaka Ben Mkapa wakati ule awe Rais. Ilibidi Lowassa atoswe ki namna!

Mimi namfahamu Edward. Ninyi mnaujua huo utajiri wake au basi akitoa michango hapa na pale ni pesa zake? Kati yenu mna utajiri zaidi ya Edward. Edward alivumilia na kumsaidia mwenzake (nasita sasa hivi kutumia neno 'rafiki') Jakaya ashinde uteuzi wa mgombea wa CCM hapo 2005. Aliamua hivyo baada ya makubaliano ya 1995. Wapo wengi wa Tanzania waliyojitolea muhanda, wa hali na mali kuungana na Edward kumwezesha Jakaya Kikwete kuwa Rais 2005. Kati yao, ndiyo wamekuwa karibu na Edward katika kinyang'anyiro cha majuzi Dodoma. Imani yao ilikuwa kwamba pamoja na mkanganyiko wa Februari 2008 wa Richmond ambao hauna mashiko yoyote ya ufisadi kwa maana ya rushwa, Rais Kikwete angemfungulia mlango mwenzake Edward kuwa mgombea wa CCM. Badala yake Edward bado akajengewa mzengwe wa utajiri kama Baba wa Taifa alivyofanya 1995. Hivi leo tukichambua nani kati yetu ni tajiri zaidi ya Lowassa tutakuwa na viongozi wanao kidhi mategemeo yetu?

Kuhusu hili swala la Richmond: Hivi baada ya taarifa ya Tume ya Bunge ya Dr Mwakyembe, Serikali litoa majibu. Mbona kwenye tuhum aza Bunge kuhusu Tegeta Escrow imekuwapo taarifa toka kwa Chief Secretary kuhusu suala hilo? Nani aliyejaribu kutoa maelezo ambayo yangemfungisha Lowassa au kumkomboa kwa kitendo chahe cha kujiuzuru kisiasa? Badala yake, wanazuoni wenzangu ambao sidhani kama tunazo facts za kutosha tuanaendelea kumshutumu Lowassa na kuwmona kama vile ni corrupt na kiongozi asiyefaa. It is not fair.

Mimi simlaumu Lowassa kujitoa CCM. Ni haki yake na kajieleza vipasavyo kuhusu maamuzi yake. Je, ni uamuzi wa uroho kuhusu U-Rais? Jamani, wanazuoni, hivi kweli tumefia hatua ya kumwona mtu ana uroho wa Urais? Ili awe au afanye nini ambacho sisi tufunge macho, na siyo tu kutoona, bali pia kuto chukua hatua? Ikifikia hapo, basi hatuna Taifa tena!!

Taifa letu limebahatika kufika hapa lilipofika mwaka huu. Wengi hatukutarajia kwamba yale ambayo tumekuwa tukitafakari na hata kusalia ghafla yameibuka. Sidhani na siamini kwamba ramani ya siasa ya Jamhuri yetu itabaki ilivyo ifikapo Desemba 2015. Ni ishara ya kheri na mwelekeo mwafaka kwa demokrasia ya Taifa letu.Naamini kwa dhati kabisa kwamba Edward Lowassa atakuwa kiongozi ambaye atasaidia ramani hii kuwa na muono mpya.

JV Mwapachu.

Culled From Wanazuoni
 
Wana zuoni lazima ifike wakati tuwe wawazi na wakweli, kwa hali hii ya sasa Lowasa ndo Rais
 
Atutolee unafiki wake hapa.Anaweweseka baada ya kuona fursa ya kupata cheo imekatwa.Hana jipya huyu.Tanga mjini imedorora na alishindwa hata kusapoti kuleta miradi ya maendeleo wakati nduguye alipokuwa mbunge.Alibweteka tu Ulaya.Hii yote ni kutapatapa baada ya kutoswa na JK
 
Mwapachu ni nani?

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Amb. Juma Mwapachu - Resume [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]

CURRICULUM VITAE OF
AMBASSADOR JUMA VOLTER MWAPACHU
LLB; DIP. International Law; D.Lit; FCMI.


1. PERSONAL DETAILS
Date of Birth : 27 September, 1942
Place of Birth : Mwanza, Tanzania
Marital Status : Married
2. EDUCATIONAL HISTORY
1949 – 1958: Several Primary Schools in Mwanza, Mbeya and Dar-es-Salaam, Tanzania
1959 – 1962: Tabora Boys Secondary School, Tanzania
(O' Levels)
Became Queen's Scout in 1961

1963 – 1964: St. Michael's and St. George's School and Mkwawa High School, Iringa Tanzania.
(A' Levels). Groria Scholae for 1964

1965 – 1969: University of East Africa (at the University College, Dar-es-Salaam) Tanzania.
Obtained a Bachelor of Laws Degree in March 1969

1977 – 1978: Indian Academy of International Law and Diplomacy, New Delhi, India.
Obtained a Post Graduate Diploma in International Law, International Institutions and Diplomacy.

November 2005: Conferred with a Doctor of Literature Degree (Honoris Causa) by the University of Dar-es-Salaam, Tanzania.


3. PROFESSIONAL MEMBERSHIPS
: Fellow, Chartered Management Institute, UK since 1981
: Fellow, Academy of Political Science, USA
: Member, Society for International Development (SID) since 1983: sits on the International Council and is Member of its from 2000

4. CURRENT POSITION: Secretary General, East African Community from April 2006 to present

5. PREVIOUS POSITION: Tanzania Ambassador to France with accreditations to Spain, Portugal, Tunisia, Morocco and Algeria, from July 2002 – April 2006

6. PROFESSIONAL EXPERIENCE
April 1969 – Sept.1969
: First Tanzania Graduate to join the Tanzania Police Force (Asst. Supt. of Police) then reverted to Attorney General's Chambers, Government of Tanzania, (State Attorney)

: Subsequently seconded to the National Bank of Commerce as Assistant Legal Secretary
Oct. 1969 – August 1973
: National Bank of Commerce (Under State Ownership) Held the following positions:

- Assistant Legal Secretary in the Legal and Trustee Department
- Personnel manger heading the Personnel Division of the Bank
- Chief Manpower Manager responsible for all personnel functions (manpower planning, recruitment and salary administration) of the Bank

Sept. 1973 – April 1976
: District Development Director, Government of Tanzania.
(Under the Decentralization Programme introduced in July 1972)

May 1976 – July 1980
: Ministry of Foreign Affairs, Government of Tanzania: Principal Foreign Service Officer

Aug. 1976 – March 1977
: Minister Counsellor and Deputy Head of Mission, Tanzania Embassy, Addis Ababa, Ethiopia

April 1977 – March 1980
: Minister Counsellor, Deputy Head of Mission and Head of Chancery, Tanzania High Commission, New Delhi, India

April – July 1980
: Acting Director, Information, Research and Policy Planning Division in the Ministry of Foreign Affairs

Aug. 1980 – Dec 1982
: Coopers and Lybrand Associates Limited, Tanzania (now PriceWaterhouse Coopers)

1988 – 1996
: Director, Board of Directors of Juthalal Velji Ltd (holding Company of JV Group)

1997 – Present
: Chairman, RJH Investments and Management Services Ltd, (Investment and Management Consultant) Tanzania

1997 – Present
: Director and Shareholder, Rickshaw Travels Limited, Tanzania

1998 – 2002
: Director, Board of Directors of East African Breweries Limited, Kenya

1998 – Present
: Director, Board of Directors Heritage Insurance (Tanzania) Limited

2000 – Present
: Director and Shareholder, Maersk (Tanzania) Limited


7. POSITIONS HELD IN TANZANIA NATIONAL PRIVATE SECTOR INSTITUTIONS AND CIVIL SOCIETY

1980 – 1984: Member of the National Management Committee of Tanzania Red Cross Society

1984 – 1990: Elected the Founding Secretary General of the Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA)

1991 – July 2002: President, Tanzania Chapter of the Society for International Development (SID)

June 1991 – April 1996: Elected Member of the Founding Governing Council of the Confederation of Tanzania Industries (CTI)

8. MEMBERSHIPS IN TANZANIA PRESIDENTIAL COMMISSION OF ENQUIRY

1989 – 1991: Member, Presidential Commission of Enquiry into Public Revenues, Taxation and Expenditure (MTEI Commission)

1991 – 1992: Member, Presidential Commission of Enquiry on One Party or Multi-Party Political System for Tanzania (NYALALI Commission)

1993 – 1994: Member, Presidential Commission to Review the Structure and Expenditure of the Government (KOLIMBA and later MRAMBA Commission)

1996 – 1998: Member of Team of Experts responsible for crafting the Tanzania Development Vision 2025

9. BOARD POSITIONS HELD IN TANZANIA PRIVATE SECTOR COMPANIES

July 2002: As President of Society for International Development (SID) Tanzania Chapter played host to the 23[SUP]rd[/SUP] SID International Congress in Dar-es-Salaam, Tanzania

1988 – 2003: President of Convocation, University of Dar-es-Salaam. As President of the University of Dar-es-Salaam Convocation, have been responsible for spearheading the holding of several key National Symposia between 1991 and 2003 covering the following topics:

- The Crisis of Social Delivery in Tanzania
- The Role of Intellectuals in the Democratization Process
- The Multi-dimensional Crisis of Education in Tanzania
- The Crisis of Multi-party Democracy in Tanzania
- Why is Tanzania Still Poor 40 years after Independence?

1990 – 2002: Vice Chair, University of Dar-es-Salaam Governing Council


10. POSITIONS HELD IN PUBLIC SECTOR INSTITUTIONS

May 1973: Member of the National Committee established by the National Union of Tanzania Workers (NUTA) to recommend an Income and Wages Policy for Tanzania

1985 – 1988: Member, National Planning and Consultative Council established by the Government, representing the Private Sector

1984 – 2002: Member of the Board of Directors, Board of External Trade, Tanzania. Vice Chair of the Board from 1988 to 2002

1986 – 1993: Member, Board of Directors, Tanzania Investment Bank

1988 – 1992: Member, Boards of Directors, Tanzania Audit Corporation

1992 – August, 1995: Chair, Board of Directors, Tanzania Railways Corporation

1994 – July 2002: Chair, Board of Directors, Tanzania Investment Bank

1998 – July 2002: Member, Board of Directors, Tanzania Standard Newspapers Limited, the Government Media Institution that publishes the Daily and Sunday News

2000 – July 2002: Member, Board of Directors of the Business Registration and Licensing Agency (an Executive Agency of the Government)

Feb. 2000 – July 2002: Commissioner in the Presidential Parastatal Sector Reform Commission (institution charged with the responsibility of managing and supervising restructuring and privatization of State owned enterprises)

11. PUBLICATIONS
: Published and edited four books including recent book: 'Confronting New Realities: Reflections on Tanzania's Radical Transformation'.
 
Chadema ishauzwa, sasa ni team Edo. Dr. Slaa kafukuzwa kama mpangaji asiyelipa kodi!!!

Wavivu wa kufikiri kama wewe wakiwa vijana, utu uzima ukiwafika hugeuka wachawi! Kama ndugu yangu uko kwenye utu uzima, kaa chonjo, usinga'e Shinyanga! kuna watu wanawashambulia watuhumiwa!
 
Sijaelewa hizo sentensi. Zinakinzana.

Ndugu zangu,

Lakini huyo huyo Baba wa Taifa alimpenda sana Edward na kumpa madaraka ndani ya CCM na baraza la mawaziri....

Badala yake Edward bado akajengewa mzengwe wa utajiri kama Baba wa Taifa alivyofanya 1995.

JV Mwapachu.

Culled From Wanazuoni
 
Ndugu zangu,

Nimekuwa kimya kwa muda mrefu katika mabadilishano ya fikra kwenye mtandao huu ambao kwa hakika, kwa maoni yangu, haubidi kuwa ni wa fikra pevu zisizo shawishika na misimamo ya 'kimalaya ya siasa'. Kama tutaserereka katika msingi huu, basi ni bora Chambi ukafunga virago na kusitish huu mtandao. Nimesoma mabadilishano na mabishano ya fikra kuhusu hali ya siasa nchini mwetu na hususan baada ya Mhe Lowassa kuamua kujiunga na Chadema na kuwa mwakilishi wa UKAWA katika kinyang'ariro cha nafasi ya Urais wa Jamhuri yetu ya Muungano. Sijui nyie wenzangu mmesimama au mmesimamia wapi katika suala hili.

Naomba niseme mwanzoni kabisa kwamba nchi yetu hii leo imefikia mahali ambapo wasomo, wanazuoni kama sisi katika mtandao huu, Hatuna budi kujitokeza na kuhesabika tunamuunga nani mkono katika uchaguzi ujao wa Rais wa Tanzania. Tuwe wakweli na siyo kuendelea kuegemea katika kificho cha 'uhuru' wa wanazuoni katika kutoa maomi na fikra kama vile sisi si wapiga kura au wananchi wanaothamini umuhimu kuhusu uongozi wa nchi yetu. Wakati huo umepitwa na hali halisi ya itikadi na maana muhimu ya uongozi wa Taifa.

Sasa, Mimi binafsi, namuuunga mkono Edward Ngoyai Lowassa. Yako mengi ambayo kazuliwa huyu ndugu yetu; tunaambiwa tangu 1995 wakati Mwalimi Juluis Nyerere alipo tamka kwamba 'huyu kijana ninalo file lake; ana utajiri usiyoelezeka. Ana nyumba kadhaa.' Lakini huyo huyo Baba wa Taifa alimpenda sana Edward na kumpa madaraka ndani ya CCM na baraza la mawaziri. Kama Edward alikwa 'corrupt' swali ni kwaninini Baba wa Taifa hakumchukulia hatua za kisiasa na kisheria? Kwanini aseme hayo aliyoyasema mwaka 1995 wakati Edward Lowassa alikuwa akiongoza kupendwa dani ya CCM, ngazi zote na akitarajiwa ndiye angependekezwa kuw mgombea wa Urais? Jamani, wanazuoni, lazima mtafakari historia na hali halisi ilivyokuwa. Mhe Jakaya Kikwete hakuwa 'the favourite' candidate in 1995. Na Mwalimu alimtaka Ben Mkapa wakati ule awe Rais. Ilibidi Lowassa atoswe ki namna!

Mimi namfahamu Edward. Ninyi mnaujua huo utajiri wake au basi akitoa michango hapa na pale ni pesa zake? Kati yenu mna utajiri zaidi ya Edward. Edward alivumilia na kumsaidia mwenzake (nasita sasa hivi kutumia neno 'rafiki') Jakaya ashinde uteuzi wa mgombea wa CCM hapo 2005. Aliamua hivyo baada ya makubaliano ya 1995. Wapo wengi wa Tanzania waliyojitolea muhanda, wa hali na mali kuungana na Edward kumwezesha Jakaya Kikwete kuwa Rais 2005. Kati yao, ndiyo wamekuwa karibu na Edward katika kinyang'anyiro cha majuzi Dodoma. Imani yao ilikuwa kwamba pamoja na mkanganyiko wa Februari 2008 wa Richmond ambao hauna mashiko yoyote ya ufisadi kwa maana ya rushwa, Rais Kikwete angemfungulia mlango mwenzake Edward kuwa mgombea wa CCM. Badala yake Edward bado akajengewa mzengwe wa utajiri kama Baba wa Taifa alivyofanya 1995. Hivi leo tukichambua nani kati yetu ni tajiri zaidi ya Lowassa tutakuwa na viongozi wanao kidhi mategemeo yetu?

Kuhusu hili swala la Richmond: Hivi baada ya taarifa ya Tume ya Bunge ya Dr Mwakyembe, Serikali litoa majibu. Mbona kwenye tuhum aza Bunge kuhusu Tegeta Escrow imekuwapo taarifa toka kwa Chief Secretary kuhusu suala hilo? Nani aliyejaribu kutoa maelezo ambayo yangemfungisha Lowassa au kumkomboa kwa kitendo chahe cha kujiuzuru kisiasa? Badala yake, wanazuoni wenzangu ambao sidhani kama tunazo facts za kutosha tuanaendelea kumshutumu Lowassa na kuwmona kama vile ni corrupt na kiongozi asiyefaa. It is not fair.

Mimi simlaumu Lowassa kujitoa CCM. Ni haki yake na kajieleza vipasavyo kuhusu maamuzi yake. Je, ni uamuzi wa uroho kuhusu U-Rais? Jamani, wanazuoni, hivi kweli tumefia hatua ya kumwona mtu ana uroho wa Urais? Ili awe au afanye nini ambacho sisi tufunge macho, na siyo tu kutoona, bali pia kuto chukua hatua? Ikifikia hapo, basi hatuna Taifa tena!!

Taifa letu limebahatika kufika hapa lilipofika mwaka huu. Wengi hatukutarajia kwamba yale ambayo tumekuwa tukitafakari na hata kusalia ghafla yameibuka. Sidhani na siamini kwamba ramani ya siasa ya Jamhuri yetu itabaki ilivyo ifikapo Desemba 2015. Ni ishara ya kheri na mwelekeo mwafaka kwa demokrasia ya Taifa letu.Naamini kwa dhati kabisa kwamba Edward Lowassa atakuwa kiongozi ambaye atasaidia ramani hii kuwa na muono mpya.

JV Mwapachu.

Culled From Wanazuoni
hapo umetia chumvi lowassa hakupata kuwa waziri enzi za mwalimu
 
Wednesday, September 3, 2008


SERIKALI IACHE KUMLINDA LOWASSA

Siku chache zilizopita. Nilitoa taarifa hii kwa vyombo vya habari. Hata hivyo, kwa sababu ambazo sizifahamu, habari hii haikutoka katika magazeti mengi ya kila siku. Pengine inaweza ikawa ni njia iliyotumika kufikisha ujumbe(barua pepe) lakini kuna uwezekano mkubwa sababu ikawa ni kuwa Lowassa hakutajwa kuchukuliwa hatua kama hizi ambazo nimezieleza hapa katika yale Maazimio 23 ya Bunge.

Yeye aliambiwa tu atakafakari na kuchukua maamuzi ambayo ataona yanafaa. Yeye akaamua kujiuzulu. Lakini bado siridhiki sana na sababu hii kwa kuwa maazimio hayo 23 hayajasema Karamagi na Msabaha wachunguzwe kuhusu Rushwa kama serikali ilivyoamua. Kama imeamualiwa na Serikali hawa wachunguzwe, kwanini serikali haikumjumuisha na Lowassa? Hii inafanya niamini kwamba bado msimamo huu hapa chini ni mwafaka:

TAARIFA KWA UMMA

SERIKALI IACHE KUMLINDA LOWASSA

Ni mmoja wa mizizi ya ufisadi wa Richmond

Akamatwe, ahojiwiwe na achukuliwe hatua za kisheria.


Tarehe 25 Februari, 2008 Vijana wa CHADEMA tulitoa taarifa kwa umma tukikemea jitihada zilizokuwa zikiendelea za Lowassa kujisafisha na kusafishwa na tukahimiza achukuliwe hatua za haraka kutokana na tuhuma za ufisadi na/ama matumizi ya madaraka katika kashfa ya RICHMOND.

Pamoja na taarifa yetu hiyo kwa umma katika kipindi chote ambacho Serikali ilipewa na Bunge kutekeleza maazimio ya Bunge kuhusu suala hilo hatua tulizopendekeza hazikuchuliwa. Aidha tumefadhaishwa zaidi na Taarifa ambayo Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo ameiwasilisha Bungeni Alhamisi 28 Agosti, 2008 pamoja na kutaja hatua ambazo zimechukuliwa kuhusu watuhumiwa wengine ikiwemo kuandikiwa Barua za kujieleza na/ama kuanza kuchunguzwa na vyombo vya dola/usalama; Waziri Mkuu hakueleza hatua ambazo zimeaanza kuchukuliwa dhidi ya Bwana Lowassa.

Tunatambua kuwa Waziri Mkuu katika taarifa yake ameeleza kuhusu hatua ambazo serikali imeanza kuchukua ikiwemo za marekebisho ya Sheria ama mifumo ya uwajibikaji, ikiwemo ile ya manunuzi. Hata hivyo, tungependa kuweka bayana kwamba matatizo ya msingi ya taifa letu hayasababishwi na mapungufu katika sheria pekee, ila kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na kulegea kwa misingi ya utawala wa sheria na uwajibikaji miongoni mwa viongozi. Hivyo, tunapenda kuwajulisha Watanzania kuwa kama watuhumiwa wa ufisadi hawatachukuliwa hatua mapema, misingi ya utawala wa sheria itazidi kutetereka na matokeo yake ni kuwa mageuzi yoyote katika mifumo ya kiutawala hayatatekelezwa kikamilifu. Kwa ujumla tunaamini kwamba utamaduni huu wa kulindana katika serikali unatoa mfano mbaya kwa vijana wa kitanzania kuhusu uongozi na utawala bora.

Tungependa kusisitiza kuwa Bwana Lowassa, akiwa Waziri Mkuu wa nchi yetu wakati huo alikuwa mmoja wa mizizi mikuu ya ufisadi wa RICHMOND. Hivyo, tunaona kuwa Taarifa ya Utekelezaji ya Waziri Mkuu Pinda imejikita katika kushughulikia matokeo badala ya mzizi wa tatizo lenyewe na hivyo kama hali hii ikiendelea itaporomosha nidhamu na uwajibikaji katika taifa letu. Tunaamini kwamba kama Bwana Lowassa aliyekuwa kinara wa Serikali wakati huo, ataweza kuchukuliwa hatua kikamilifu basi itakuwa rahisi kwa waliokuwa chini yake kuweza kuchukuliwa hatua za haraka na hatimaye kurejesha maadili katika utawala.

Lakini kama Serikali itaendelea kumlinda Bwana Lowassa na kuwatoa kafara maafisa wa chini, bado haitakuwa imetekeleza kikamilifu dhana ya uwajibikaji na utawala wa Sheria. Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu na mawaziri wenzake kadhaa ni hatua ndogo sana katika kashfa iliyohusisha uvunjaji wa Sheria za nchi yetu, mazingira ya ufisadi na hasara kubwa kwa taifa.


Sisi tunaona kutotajwa kikamilifu kwa hatua zilizochuliwa juu ya Bwana Lowassa ni mwendelezo wajitihada za miezi ya karibuni za Bwana Lowassa(Mb) kupita akijitetea kuanzia katika hotuba yake alipokwenda Jimboni Monduli na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari na hata mahojiano yake maalumu na Televeshioni ya Taifa(TVT).

Aidha, taarifa ya Waziri Mkuu Pinda imeakisi uamuzi wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bwana Edward Lowassa kujitokeza miezi ya karibuni kujitetea kuhusu kuhusika kwake katika kashfa ya Richmond ambayo kwa ujumla ni ishara ya unafiki wa kisiasa. Itakumbukwa kuwa baada ya Kamati Teule kuwasilisha taarifa yake, Bwana Lowassa alipata nafasi bungeni takribani mara mbili kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni wakati akiwa Waziri kuzungumzia suala hili lakini hakutoa utetezi ambao Mwezi Februari alijaribu kuutoa kwa umma. Waziri Mkuu Pinda inabidi auleze Umma kama uamuzi wa kumtomtaja katika Taarifa yake ya utekelezaji kuhusu hatua ambazo amechuliwa ni ishara kuwa serikali imekubaliana na utetezi wa Bwana Lowassa.

Itakumbukwa kuwa Vijana wa CHADEMA tulieleza wazi kwamba katika kujitetea kwake mwezi Mei, Bwana Lowassa alithibitisha wazi uzembe na matumizi mabaya ya madaraka ambayo aliyafanya alipokuwa Waziri Mkuu wakati wa sakata zima la Richmond.

Hivyo, tunarudia kutoa mwito kwa vyombo vya dola kuweza kumkamata, kumhoji na kumchukulia hatua za kisheria dhidi ya uzembe na matumizi hayo mabaya ya madaraka kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Badala ya Bwana Lowassa kuendelea kupita akijitetea kuwa Kamati Teule haikumuita kuweza kujieleza; vyombo vya dola vimkamate akatoe maelezo yake panapohusika.

Vyombo vya dola vimekuwa vikiwakamata raia wa kawaida wenye taarifa za uhalifu kuweza kuisadia polisi, inashangaza Bwana Lowassa amejieleza wazi kuwa alikuwa anafahamu uhalifu uliokuwa ukitendeka lakini bado yuko nje akijitetea na pia Taarifa za kiserikali zikielekea kumlinda.

Tunaamini akikamatwa yeye, atawezesha watuhumiwa wakuu wa kashfa ya Richmond kuweza kupatikana. Tulieza wazi katika tamko letu na Mwezi Februari kuwa , jitahada zozote za kumlinda na kumtetea zingeweza kuathiri mwekekeo wa hatua ambazo zitanatarajia kupendekezwa na Kamati ya Waziri Mkuu mpya Mheshimiwa Mizengo Pinda. Kutokana na Taarifa ya Waziri Mkuu Pinda aliyowasilisha Bungeni Alhamisi tarehe 28 Agosti, 2008 ni wazi kuwa kuna kila dalili kuwa mwelekeo huo umeanza kuathiriwa, hivyo tunarudia tena kutaka Bwana Lowassa achukuliwe hatua kabla ya Bunge la Mwezi Novemba, 2008.

Bwana Lowassa akiwa Waziri Mkuu amethibitisha kwamba maneno yake mwenyewe kuwa alikiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 na Sheria ya Makosa ya Udhibiti wa Uhujumu wa Uchumi wa nchi ya Mwaka 1984.

Bwana Lowassa alikiri kwamba alikuwa anafahamu kwamba Richmond ni kampuni ya kitapeli, lakini katika kipindi chote cha uongozi wake aliinyamazia hali hii na kwa kiasi kikubwa aliitetea kampuni hiyo mbele ya macho ya umma. Wakati wa Viongozi mbalimbali wa upinzani walipoweka bayana kwamba Richmond ni kampuni isiyo na uwezo, serikali ilitetea kampuni hiyo.

Vyombo mbalimbali vya habari vilimtuhumu Bwana Lowassa mwaka 2006 na 2007 kama kiongozi wa Shughuli za serikali bungeni, kwamba alishiriki ‘kuwaziba midomo’ wabunge wa CCM wasijadili suala hili. Pia, ni Bwana Lowassa huyo huyo, alinukuliwa akiwa Arusha akiwataka watanzania wasiijadili kampuni ya Richmond baada ya mvua kuanza kunyesha.

Kama Bwana Lowassa wakati wote huo alijua kama ni kampuni ya kitapeli kama anavyojaribu alivyojaribu kujitetea, uamuzi wake wa kuwaasa watanzania wasiijadili ulikuwa ni wa kulinda ufisadi ambao aliufahamu. Inashangaza pia ni Lowassa huyo huyo alisema alijua kuwa Richmond ni kampuni ya kitapeli; ni Lowassa huyo huyo alisema kwamba alishauriwa vibaya na watumishi wa umma aliowataja kuhusu uwezo wa Richmond; Ni Lowassa huyo huyo aliyesema kwamba alijua kuwa TANESCO chini ya Menejimenti ya Net Group Solution walitaka kuhujumu mchakato wa tenda na hivyo ‘kuwanyang’anya’. Lakini ni Lowassa huyo huyo aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye angeweza kuviagiza vyombo vya dola kumwezesha kuthibitisha ‘utapeli wa Richmond’; hivyo, maelezo ya sasa yanayotolewa kuhusu ushiriki wake yanaonyesha kuwa sasa kuna mwelekeo wa kumlinda.

Tunaendelea kushangazwa na Serikali na Bwana Lowassa kutumia utetezi wake kueleza tu nia yake ya kutaka mkataba wa Richmond usitishwe; nia ambayo kama ni kweli alikuwa na uwezo wa kuitekeleza na hakuitekeleza. Tunaitaka Serikali na Bwana Lowassa kuweka bayana ni kwa vipi Richmond ilipewa tenda hiyo na kwa shinikizo la nani. Bwana Lowassa anakwepa kuyazungumzia haya kwa kuwa anajua kabisa kwamba ni yeye aliyetumia madaraka yake vibaya alipokuwa Waziri Mkuu kwa kukiuka Sheria na Taratibu za Ununuzi kwa ‘kupora’ mchakato uliokuwa ukiendeshwa na TANESCO, ‘kuunda kamati yake’ na kuzisukuma mamlaka za ununuzi hali iliyopelekea Richmond kupewa tenda ili hali haikuwa na uwezo uliotakiwa.

Ni uzembe huu ambao umelisababishia hasara taifa kwa kulipa shilingi milioni 152 kila siku kwa kampuni ya Dowans iliyohamishiwa mkataba wa kitapeli wa Richmond; na takribani bilioni 172 kwa ujumla ambazo taifa linawajibika kuzilipa kutokana na kukodisha mitambo hiyo.

Hvyo tunarudia tena rai yetu ya kutaka fedha zilizozilipwa kizembe mpaka sasa kurejesghwa serikalini. Kwa vyovyote vile, jitihada za Bwana Lowassa za kuhamasisha ujenzi wa Sekondari Kata, na utumishi wake kama Waziri Mkuu katika kipindi cha miaka miwili, haviwezi kuzidi hasara aliyosababisha katika uchumi wetu kipindi chote tulichokosa umeme wa dharura na wala hailingani na hasara ambayo tunaendelea kuilipa kila siku iendayo kwa Mungu. Maamuzi haya ya Bwana Lowassa yanaendelea kuwaumiza wananchi wote ikiwemo wa Jimbo lake la Monduli ambao wanataabika kwa mzigo wa gharama za umeme.

Tunarudia tena kumkumbusha Rais Kikwete kwamba Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba taratibu zinatengenezwa zitakazojenga maadili na kuongeza imani ya wananchi kwa uadilifu wa viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi ndani ya Serikali na katika sekta ya umma. Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile imeweka kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa umma: kwamba wanapokuwa madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali.

Kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa maslahi ya umma. Hivyo, taarifa ya Waziri Mkuu Pinda kutokueleza bayana hatua ambazo Bwana Lowassa ameshachukuliwa au atachukuliwa ni ishara kuwa kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa wakati akizungumza na Wazee wa CCM mkoani Dar es Salaam kwamba Bwana Lowassa amepata tu ‘ajali ya kisiasa’, na kumsifu kwa utumishi wake imechangia kumlinda mhusika huyu mkubwa katika sakata zima la RICHMOND.

Vijana wa CHADEMA tulitarajia kuwa, baada ya Bwana Lowassa kukiri mwenyewe hadharani kuhusu uzembe wake na matumizi mabaya ya madaraka Rais Kikwete angelekeza hatua za kuchukuliwa dhidi yake badala ya kuendelea kumpamba kama “shujaa wa uwajibikaji’, kinyume na hayo tutaamini kwamba serikali yake inaendeshwa kwa ‘ubia wa kulindana’.

Aidha tunarudia kutoa rai kwamba Rais Kikwete kuwafukuza kazi watumishi wote wa umma waandamizi ambao wametajwa na Bwana Lowassa kushiriki uzembe na matumizi mabaya ya madaraka; watumishi ambao walitajwa pia na Kamati Teule ya Bunge lakini mpaka sasa wanaendelea kutumikia nafasi zao mbalimbali. Kwa kuwa Waziri Mkuu Pinda ameshatangaza kwamba kwa wale wateule wa Rais, Kamati yake imeshapeleka suala zima kwake, tunategemea Rais atachukua hatua za haraka ili kuonyesha mfano kwa viongozi wengine wa chini yake wanaotarajiwa kuchukua hatua kwa watumishi wa chini.

Kadhalika tunapenda kuvikumbusha tena vyombo vya dola kwamba Sheria ya Udhibiti wa Makosa ya Kuhujumu Uchumi ya mwaka 1984 inatamka makosa yafuatayo kuwa baadhi ya makosa ya kuhujumu uchumi ni pamoja na yale yote yenye kusababisha hasara kwa mamlaka ya Serikali. Pia Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 inatamka kuwa ubadhirifu na/au ufujaji wa mali ya umma unaofanywa na watumishi wa umma na Matumizi mabaya ya madaraka kwa ajili ya manufaa binafsi, ni sehemu ya ufisadi.

Bwana Lowassa alithibitisha kwamba maneno yake kwamba wapo viongozi waandamizi wa Serikali ambao amewataja kwa majina wamefanya maamuzi ya kifisadi, kitendo chake cha kunyamazia ufisadi huo- kinafanya iwe vigumu kwa yeye kutenganishwa na tuhuma za ufisadi zilizomo katika mchakato mzima wa kupewa tenda kwa kampuni ya Richmond na mambo yote yaliyotokea baada ya Mkataba huo kuhamishiwa kwa kampuni ya Dowans.

Aidha tumefadhaishwa na Taarifa ya Waziri Mkuu Pindi kwamba kujiuzulu kwa Waziri Mkuu na Baadhi ya Mawaziri ilikuwa ni ishara ya hatua ambazo serikali imechukua kutekeleza maazimio ya Bunge kuhusu suala husika. Tunarudia kukumbusha kwamba toka sakata la Richmond lilipoanza zaidi ya mwaka mmoja uliopita tulimtaka Bwana Lowassa kujiuzulu kulinda heshima yake lakini alikaidi na kuitetea kampuni ya Richmond. Uamuzi wa yeye kujiuzulu baada ya kashfa yote kuwa hadharani, umesaidia tu kuilinda serikali ya CCM lakini katu hauwezi kumpatia heshima ya uwajibikaji na wala hakuwezi kuwa ishara ya kwamba Maazimio ya Bunge yameshatekelezwa.

Kwa niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), kwa taarifa hii tunarudia kukemea jitihada zozote za kumlinda na kumtangaza Lowassa kuwa shujaa katika taifa letu kwani hali hii ikiachwa kuendelea inatoa mfano mbaya kwa vijana wa Tanzania. Tusingependa kwa namna yoyote katika taifa letu, mtuhumiwa wa ufisadi aliyetajwa pia katika orodha ya mafisadi(list of shame) kulindwa na kuenziwa kama shujaa wa Taifa letu kwani ni kuharibu maana nzima ya ushujaa katika uwajibikaji.

“Inasikitisha kwamba vijana wezi wadogo wadogo wakijazana magerezani. Vijana wamachinga kuendelea kukosa mitaji na maeneo ya kufanyia biashara; wanafunzi wa elimu ya juu wakipandishiwa ada na wengine kukosa mikopo- huku fedha za walipa kodi zikiendelea kuteketea kwa ufisadi na watuhumiwa wa ufisadi wakiendelea kutamba hadharani. Hali hii ikiachwa, itaharibu utawala wa sheria na kuleta matabaka katika taifa letu. Vijana tusingependa kuona nchi yetu inatumbukia kwenye migawanyiko kwa sababu ya kuwalinda watu wachache kwa kisingizio cha haki za binadamu”

Imetolewa tarehe 31 Agosti 2008 safirini Kenya na:

John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana
0754694553

Siasa za kisasa hazitaki ulaghai
 
Yaani Mwapachu anadiriki kusema Nyerere ni muongo ili tu ahalalishe kitendo cha Lowassa kununua nafasi ya kugombea urais Chadema na kumtosa Slaa. Yaani Edo kutoswa CCM kaonewa ila Slaa kutoswa Chadema ni sawa.Kweli pesa mwanaharamu...
Kwani Nyerere hawezi kuwa Mwongo?
 
Bukanga

Hata Mungu alimpenda sana ibilisi kabla hajaasi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom