Kauli ya Mwapachu Kuhusu Lowassa

Kauli ya Mwapachu Kuhusu Lowassa

Ilaumu CCM kama umetoka kapa. Haya ndio matuda yake baada ya miaka hamsini ya utawala wake. Kimombo ni sehemu ya lugha muhimu humu jamvini.
 
ccm cannot be a business venture but a political party. those who consider ccm as a business venture are the problem and members should not be afraid to get rid of them. the primary objective of a political party should be delivery of good governance that would lead to economic and social development of the general public and not to certain individuals or families in the country. those who want to turn political parties to corporate bodies are the enemies of the people.

No! The author used a business enterprise just as an analogue; not that he meant CCM to be one.
 
Huyu Marconi ni mtu mlaghai toka wakati ule aliposema kwamba amekuwa wa kwanza kupeleka sauti across the Atlantic. Wa kwanza alikuwa Nikola Tesla. Anavyosema Mwapachu ni sasa. Anatumia business analogy au allegory. Kwamba lolote unalotaka kufanya you must know what you are doing. Usifanye mambo kiholela. Kama Marconi haupingi hill basis hakuna unalobishana na Mwapachu.
 
It is sheer stupidity for an experienced person like Mwapachu to come up with such analogy at this early stage. It is a bit irrational and irrelevant to even suggest that without hard and compelling reasons.
 
Nitaongea Kiswahili, lugha ya taifa. Kwa lugha ya biashara, Mjumbe kakosea kutumia neno "divestiture" kwa sababu hilo hutumika unapobadili HULKA ya mfumo. Bila shaka Mzee Mwapachu kaazima lugha ya PSRC ambako divestiture likuwa inatumika ikiimanisha "privatisation", yaani ubinafsishaji.

CCM haibinafsishwi - ingawa kina Lowasa wangependa sana iwe mali binafsi kama ilivyo CHADEMA, yaani mali ya familia mbili tatu tu za Kichagga - CCM ilkuwa inajipanga upya kwa kuachiana madaraka, kumrithi Rais baada ya muda wake kuisha Kikatiba. Mzee Mwapachu angekuwa hodari angetumia neno "SUCCESSION" badala ya divestiture. Kwenye succession huwa hakuna kujivua, wala huoni "core business" na "non-core business": wote waliopo ni core business, shida tu ni kumpata yupi atafuata NYAYO vizuri zaidi.

Lowasa aliachwa precisely kwa sababu alitaka kuifanya CCM iwe biashara, to be taken by the highest bidder. Uamuzi haukuwa mgumu, walisaidia UKAWA wenyewe kwa kuiaminisha jamii kuwa Lowassa ni fisadi. "Baba" wa CHADEMA mpya, Padri W Slaa, ndiye aliyeasisis neno FISADI na kinara wake alimtaja kuwa ni Lowassa. Kama CCM walikosea, je na Father Slaa pia alikosea??

Mlio karibu naye tafadhali mshaurini Mzee Mwapachu asijivunjie heshima yake aliyojijengea siku nyingi. Pia ni ubinadamu na si vibaya tukimtaka awe na fadhila kwa CCM ambacho kama chama tawala ndiyo kilipelekea yeye awe international citizen of repute. Asijiunge na mafisadi, maadui wa wananchi wanaochumia matumbo. Mwapachu na Lowassa waambiwe kuwa Ikulu hainunuliki kwa mapesa.

Narudia: hii ni SUCCESSION, siyo DIVESTITURE, kwa hiyo hakuna haja ya kuangalia hoja zake.

William Marconi.

Asante sana William, nahisi ujumbe atakuwa kaupata. Hawa wazee wanafanya malipizi. Wanahisi Kikwete amewakosea kwa kuwanyima vyeo. Kwa kufanya hivi wao wanadhani wanamkomoa Kikwete. Jamani hawa wazee hawana uzalendo kabisa na hii nchi. Hawa na wengine wengi wanapigana vita kumkomoa Kikwete. Wala hawana sababu za msingi za kukimbilia kwa Lowassa. Na wengine ndo wanadandia treni kwa mbele wakijua hawa ni wenzao i.e WAZALENDO. Hawana dhamira ya ukombozi wala. Na hawa walikuwa wanufaika wakubwa na huo mfumo unaosemwa kuwa ni 'mbovu'. Kwa kupitia Lowassa wanajidanganya. Kama amewafata kwa njia hiyo AMEWADANGANYA.
 

Mapachu is visionary and transparent, and sadly enough, Your assumptions are odd, and would only be possible under the same same CCM and its corrupt systems downstream.
However, the guy [EL] joined a separate entity which is purely out of your mental parameters, specifically from 'mode operandi' to what would be 'state machinery' of which you have no clues of how the 'machinery' will and how those 'businessmen and drug barons would step their feet in! Please wait a minute, EL would never 'walk a free way' as you pre-empty, but rather work withing the Party's and coalition baselines!
...thus don't panic, stay well tuned for better then!


How can you call someone a visionary on the basis of a prophesy that has not yet come to bear? If you will be patient enough until after October then you can come back and propound Mwapachu's vision!!! I believe Juma Mwapachu is just hedging his bets so that in the event EL succeeds to go to Magogoni then he wants also to be counted as one of the people who stood up for him.

It is foolhardy to even think that EL is a MOSES who will deliver this country from bondage because EL and Kikwete are of the same mind-set. To me Dr. Slaa was our Moses [ mostly using Nyerere's policies to expound issues] who unfortunately has been sidelined by people who put their personal interests at the expense of wananchi interests.

CCM on the other hand has the best policies amongst all political parties because they are human centered; the problem with ccm is the current leadership that has managed to highjack the party and morgarged it to persons masquerading as businesspeople including drug barons!! Get rid of Kikwete and his gang in party leadership positions and replace them with people with integrity, ccm as a party will prosper again!!
 
How can you call someone a visionary on the basis of a prophesy that has not yet come to bear? If you will be patient enough until after October then you can come back and propound Mwapachu,s vision!!! I believe Juma Mwapachu is just hedging his bets so that in the event EL succeeds to go to Magogoni then he wants also to be counted as one of the people who stood up for him.

It is foolhardy to even think that EL is a MOSES who will deliver this country from bondage because EL and Kikwete are of the same mind-set. To me Dr. Slaa was our Moses [ mostly using Nyerere's policies to expound issues] who unfortunately has been sidelined by people who put their personal interests at the expense of wananchi interests.

CCM on the other hand has the best policies amongst all political parties because they are human centered; the problem with ccm is the current leadership that has managed to highjack the party and morgaged it to businesspeople including drug barons!! Get rid of Kikwete and his gang in party leadership positions and replace them with people with integrity, ccm as a party will prosper again!!

For fifty years they have ruled the country and here we are very poor country with ccm slogan nchi bado changa untill when itakomaa its not about kikwete gang its about economic policy failure of the ccm for past five decade so its time we put them aside and give opportunity to other party with different policy.
 
Kauli ya Juma Volter Mwapachu Kuhusu Lowassa

Ndugu zangu,
Nimekuwa kimya kwa muda mrefu katika mabadilishano ya fikra kwenye mtandao huu ambao kwa hakika, kwa maoni yangu, haubidi kuwa ni wa fikra pevu zisizo shawishika na misimamo ya 'kimalaya ya siasa'.

Kama tutaserereka katika msingi huu, basi ni bora Chambi ukafunga virago na kusitish huu mtandao. Nimesoma mabadilishano na mabishano ya fikra kuhusu hali ya siasa nchini mwetu na hususa ni baada ya Mhe Lowassa kuamua kujiunga na Chadema na kuwa mwakilishi wa UKAWA katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano. Sijui nyie wenzangu mmesimamia wapi katika suala hili.

Naomba niseme mwanzoni kabisa kwamba nchi yetu hii leo imefikia mahali ambapo wasomi, wanazuoni kama sisi katika mtandao huu, Hatuna budi kujitokeza na kuhesabika tunamuunga nani mkono katika uchaguzi ujao wa Rais wa Tanzania. Tuwe wakweli na siyo kuendelea kuegemea katika kificho cha 'uhuru' wa wanazuoni katika kutoa maomi na fikra kama vile sisi si wapiga kura au wananchi wanaothamini umuhimu kuhusu uongozi wa nchi yetu. Wakati huo umepitwa na hali halisi ya itikadi na maana muhimu ya uongozi wa Taifa.

Sasa, Mimi binafsi, namuuunga mkono Edward Ngoyai Lowassa. Yako mengi ambayo kazuliwa huyu ndugu yetu; tunaambiwa tangu 1995 wakati Mwalimu Julius Nyerere alipotamka kwamba 'huyu kijana ninalo faili lake, ana utajiri usiyoelezeka. Ana nyumba kadhaa.' Lakini huyo huyo Baba wa Taifa alimpenda sana Edward na kumpa madaraka ndani ya CCM na baraza la mawaziri.

Kama Edward alikuwa 'corrupt' swali ni kwanini Baba wa Taifa hakumchukulia hatua za kisiasa na kisheria? Kwanini aseme hayo aliyoyasema mwaka 1995 wakati Edward Lowassa alikuwa akiongoza kupendwa dani ya CCM, ngazi zote na akitarajiwa ndiye angependekezwa kuwa mgombea wa Urais?

Jamani, wanazuoni, lazima mtafakari historia na hali halisi ilivyokuwa. Mhe Jakaya Kikwete hakuwa 'the favourite' candidate in 1995. Na Mwalimu alimtaka Ben Mkapa wakati ule awe Rais. Ilibidi Lowassa atoswe kinamna!

Mimi namfahamu Edward, Ninyi mnaujua huo utajiri wake au basi akitoa michango hapa na pale ni pesa zake? Kati yenu mna utajiri zaidi ya Edward. Edward alivumilia na kumsaidia mwenzake (nasita sasa hivi kutumia neno 'rafiki') Jakaya ashinde uteuzi wa mgombea wa CCM hapo 2005. Aliamua hivyo baada ya makubaliano ya 1995.

Wapo wengi wa Tanzania waliyojitolea muhanda, wa hali na mali kuungana na Edward kumwezesha Jakaya Kikwete kuwa Rais 2005. Kati yao, ndiyo wamekuwa karibu na Edward katika kinyang'anyiro cha majuzi Dodoma.

Imani yao ilikuwa kwamba pamoja na mkanganyiko wa Februari 2008 wa Richmond ambao hauna mashiko yoyote ya ufisadi kwa maana ya rushwa, Rais Kikwete angemfungulia mlango mwenzake Edward kuwa mgombea wa CCM. Badala yake Edward bado akajengewa mzengwe wa utajiri kama Baba wa Taifa alivyofanya 1995.

Hivi leo tukichambua nani kati yetu ni tajiri zaidi ya Lowassa tutakuwa na viongozi wanao kidhi mategemeo yetu?

Kuhusu hili swala la Richmond: Hivi baada ya taarifa ya Tume ya Bunge ya Dr Mwakyembe, Serikali ilitoa majibu. Mbona kwenye tuhuma za Bunge kuhusu Tegeta Escrow imekuwapo taarifa toka kwa Chief Secretary kuhusu suala hilo?

Nani aliyejaribu kutoa maelezo ambayo yangemfungisha Lowassa au kumkomboa kwa kitendo chake cha kujiuzuru kisiasa? Badala yake, wanazuoni wenzangu ambao sidhani kama tunazo facts za kutosha tunaendelea kumshutumu Lowassa na kumwona kama vile ni corrupt na kiongozi asiyefaa. It is not fair.

Mimi simlaumu Lowassa kujitoa CCM. Ni haki yake na kajieleza vipasavyo kuhusu maamuzi yake. Je, ni uamuzi wa uroho kuhusu Urais? Jamani, wanazuoni, hivi kweli tumefikia hatua ya kumwona mtu ana uroho wa Urais? Ili awe au afanye nini ambacho sisi tufunge macho, na siyo tu kutoona, bali pia kuto chukua hatua? Ikifikia hapo, basi hatuna Taifa tena!!

Taifa letu limebahatika kufika hapa lilipofika mwaka huu. Wengi hatukutarajia kwamba yale ambayo tumekuwa tukitafakari na hata kusali ghafla yameibuka. Sidhani na siamini kwamba ramani ya siasa ya Jamhuri yetu itabaki ilivyo ifikapo Desemba 2015.

Ni ishara ya kheri na mwelekeo mwafaka kwa demokrasia ya Taifa letu.Naamini kwa dhati kabisa kwamba Edward Lowassa atakuwa kiongozi ambaye atasaidia ramani hii kuwba na muono mpya.

Juma Volter Mwapachu..
 
Back
Top Bottom