Kauli ya Kikwete sasa yashtukiwa

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,380
911,169
*Ni kuhusu kuridhia mabadiliko ya katiba 2011
*CUF wahoji, ni kuweka viraka, au katiba mpya
?

Na Rabia Bakari

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuweka wazi msimamo wa kauli yake kuhusu mabadiliko ya katiba, endapo inawekewa viraka ama inaandikwa upya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Naibu Katibu Mkuu Bara, Bw. Julius Mtatiro, alisema kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa wakati wa kuukaribisha mwaka mpya, imejaa utata mkubwa, na haikuwa wazi kwa wananchi kiasi cha kuchanganya watu.

"CUF kinaunga mkono kauli ya Rais ya kuanzisha mchakato wa katiba lakini tunatilia mashaka aina ya katiba ambayo anaitaka kutokana na maneno ambayo aliyatumia katika hotuba yake.

"Nikimnukuu hapa anasema 'Jambo la nne ambalo tulikubaliana kufanya ni kuanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya nchi Yetu kwa lengo la kuihuisha ili hatimaye tuwe na katiba inayoendana na taifa lenye umri wa nusu karne'.

"Kauli hii ya rais ina utata mkubwa kwani hakutaka kusema wazi anasimamia lipo kati ya katiba mpya au kuweka viraka kwa katiba iliyopo," alisema Bw. Mtatiro.Aliongeza kuwa wanaitilia mashaka kauli hiyo kutokana na ukweli Rais Kikwete na watendaji wake wamekuwa wakitofautiana katika suala hilo.

Aliwataka watendaji hao kuwa ni Waziri wa Katiba na Sheria, Bi. Celina Kombani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, ambao wote kwa nyakati tofauti walisema katiba mpya kwa sasa haiwezekani, na hakuna umuhimu, bali kinachowezekana ni kuifanyia marekebisho hii ya sasa.

"Sote tunafahamu kuwa rais wetu hana utaalamu wa mambo ya kisheria, inapotokea watendaji wake wa karibu na wataalamu wa sheria wanatofautiana naye kimtazamo kiasi cha wao kusema hadharani misimamo yao, halafu rais naye anakuja na msimamo wake, inaleta mashaka," alidai.

Akitoa msimamo wa CUF katika hilo, Bw. Mtatiro aliitaka ikulu itoe ufafanuzi wa kauli ya rais ili wadau na Watanzania wote wajue rais anaangukia katika msimamo upi.

Alidai kuwa nia matatarajio ya CUF kuwa Rais Kikwete atakidhi matakwa ya Watanzania walio wengi ambao wanahitaji kwa dhati uwepo wa katiba mpya itakayoandikwa upya ili kukidhi kizazi cha sasa.

Aidha alisema CUF wanamtaka Rais Kikweta kuwapumzisha watendaji wake walioonekana kuropoka kwa madai kuwa watakuja kumtia aibu kama ya viongozi waliopita.

"CUF inawaomba Watanzania wakae tayari kuishinikiza serikali iwapo watatokea wajanja wanaotaka kutupatia katiba yenye viraka, iwapo tutaandika katiba mpya chini ya Rais Kikwete atakuwa rais wa pekee Tanzania katika kuimarisha mfumo wa demokrasia na atakumbukwa mno na vizazi vyote," alidai Bw. Mtatiro.

Sambamba na hayo, pia Bw. Mtatiro alisema CUF inaenda kuishtaki serikali kwa wananchi kwa njia mbalimbali kutokana na kuwapa gharama kubwa, kutokana na kupanda kwa gharama za umeme.

Alisema serikali ya CCM haina ubunifu wa vyanzo vya umeme, wakati vipo vingi na hivyo kusababisha mzigo mkubwa wa gharama kwa wananchi na kudidimiza uchumi.

Aliongeza kuwa japo rais alizungumzia suala la umeme katika hotuba yake lakini hajajibu maswali ya wananchi na wala hajatoa suluhisho litakaloleta unafuu wa maisha ya Mtanzania katika matumizi ya nishati hiyo.

"Wakati pakiwa na ongezeko kubwa la bei za umeme, lakini nishati hiyo haipatikani na hata pale inapopatikana haitoshi, na serikali ya CCM bado inajipa matumaini kuwa hali hii itaimarika lakini muda unavyozidi kwenda ndiyo matumizi ya umeme ambao haupo yanaongezeka kutokana na ongezeko la watu, wawekezaji nakadhalika," alisema Bw. Mtatiro.

Alidai kuwa kwa hali ya wazi Rais Kikwete ameaihidi utekelezaji wa miradi mingine kadhaa itakayotoa takriban megawati 1,130 katika kipindi cha 2011-2013, jambo ambalo litakuwa maajabu ya dunia."Yaani serikali iliyoweza kuongeza uzalishaji wa megawati 145 tu katika kipindi cha miaka mitano, itaweza vipi kuzalisha megawati 1,130 kwa kipindi cha miaka mitatu? Watanzania wanadanganywa mchana kweupee tena bila chembe ya aibu.

Katika kuungana na Watanzania kuishinikiza serikali isitafute unafuu wa mikataba feki na ya kifisadi kama Dowans na kadhalika kupitia migongo yao, CUF kinajiandaa kuishtaki serikali kwa Watanzania kupitia njia mbalimbali, ili tusaidiane kuishinikiza, kwa sababu hawakuichagua ili iwacharaze bakora kiasi hicho," alisisitiza.
 
CUF wasichoelewa hadi hivi sasa ni kuwa JK hajatofautiana na kauli za Werema na Celina Kombani..........................Celina na Werema wanapinga Katiba mpya na kwenye hilo Jk anawaunga mkono kwa kuteua Tume ambayo itafanya kazi kwa maelekezo ya Ikulu na wala siyo ya Bunge...........................

Uzoefu tulionao ni kuwa Tume ya Raisi ya marekebisho ya katiba mwishowe huzalisha viraka kwenye katiba ambavyo vinaridhisha kero za viongozi wa juu serikalini na wala siyo raia.................................

Sasa CUF badala ya kuunga mkono hoja ya JK kwa shingo upande wanapaswa kuikataa...........kwa sababu Tume hiyo haina nguvu ya kisheria na siyo shirikishi kwa sababu haikuchaguliwa na wabunge kutokana na sheria zilizopo ambazo zimeweka wazi ya kuwa kazi zote za serikalini zitatangazwa kwenye vyombo vya habari na kutoa fursa sawa kwa kila mtanzania kujitokeza na kupew nafasi sawa ya ushiriki..................................

Kwa kutofuata utaratibu huu wa kisheria ni kuwa Tume hiyo ni batili kwa sababu haikumshirikisha kila mtanzania katika kuiunda.........................Itakuwa ni Tume iliyochakachuliwa na kamwe haiwezi kutuandikia katiba mpya ila itapendekeza viraka kama serikali ya JK itakavyo..............................

Kubwa zaidi ambalo CUF na watanzania wote kwa ujumla wetu tunapaswa tusisahau ni kuwa CCM haikuwa na ajenda ya kuandika katiba mpya kwenye Ilani yake ya uchaguzi wao sasa iwaje leo tuiamini CCM na JK wake ya kuwa wana nia njema wakati hata utaratibu wa kuiandika katiba mpya hawataki kuufuata na wameanza kwa mikwara na kucheza faulo za waziwazi kabisa?


Wake up CUF and join the progressive forces clamouring for a new dawn in this nation, we gladly call home..................
 
MHE KIKWETE ALIAHIDI 'KUTAFUTA MAONI' JUU YA KATIBA MPYA, SI KUANDIKWA UPYA HUKO:

Mhe Juliasi, hata siku moja usitegemee Jemadari wa CCM kupoteza muda wake hadimu KUFANYIA KAZI JAMBO LA KULILETEA CUF MAFANIKIO hata siku moja usahau hili.

Pili, tangu lini serikali ya CCM imewahi kufanyia kazi jambo ambalo halimo katika ILANI yao ya uchaguzi? Sahau kabisa hilo. CCM wamekaa lini na kumpa baraka Kikwete kubadilisha Katiba inayowalea vizuri kula na kusaza??

Mwisho, Mhe Kikwete hakuwahi kuahidi popote KUPATIKANA KATIBA MPYA. Ndugu yetu aliahidi tu kutafuta MAONI juu ya nani anataka Katiba Mpya. Ukumbuke maoni ni maoni na jinsi gani Mafisadi watakavyowekeza hapo kupitisha maoni yanayoenzi zaidi UFALME WA KIFISANI katika taifa letu.

Mwenzetu huyu alichokitupa uwanjani CHEAP POLITICAL GAME (karata ya kisiasa ilioshindwa kufanya kazi hata kabla halijaanza) kwa kusema YEYE KIKWETE ANAKUSUDIA KUJIANZISHIA CHOMBO CHAKE KUKIDHI MATAKWA YAKE KUBAINI 'MAONI' KWAMBA NI WANGAPI WANANCHI TUNATAKA KATIBA mpya na jibu lake tayari alishaitoa Jaji Werema kwamba ni viraka vichache tu vya hapa na pale tu tosha.

Ukumbuke Mhe Kikwete, kama marais wa CCM waliomtangulia, atatumia ujanja ule ule wa kutawanya kwenye matawi yote ya CCM nchini aina ya Ujumbe ambayo sikio lake litapendezewa kulisikia kisha atawatuma wale wale vijana wake atakaowaingiza katika tume yake BINAFSI waende wakakusanye maoni yale yale atakayokua ametawanya tangu mwanzo na kuibuka na jibu kwamba ni Watanzania asilimia 0.2% ndio wanaotaka katiba mpya hivyo haina haja tuweke tu viraka maeneo machache na maisha yaendelee.

Hivyo basi, Mhe Mtatiro unalo jukumu kutumia nafasi yako katika chama kama kijana mwenzetu ili kuhakikisha ya kwamba vyama vyote vya upinzani vinaungana nguvu sasa hivi tu na kushirikiana na 'Wabunge Wapambanaji' wetu walioko ndani ya CCM kuleta Tume ya Taifa Kuratibu mambo ya katiba na wala tusitegemee hata kidogo Tume ya Kikwete itakayokua ikiamrishwa na VINARA WA UFISADI njia gani pa kupita.

Amka sasa hivi Mhe Julius Mtatiro na wengine wachache MLIOANZA KUDANGANYIKA.na tujue mambo yote ni kule Bungeni Dodoma. Kwa nini sasa hivi MAFISADI waogope Bunge juu ya hili????

MAFISADI wanaogopa kupambana kule bungeni kwa sababu hawana bajeti nyingine ya kugharamia hilo kwani walimaliza fedha zote kwenye kununua uchaguzi wetu mkuu basi wakajua baada ya hapo ni ule ule wimbo wa 'UTULIVU NA AMANI YETU' huku wakiendelea kutafuna nchi.

No more buying time. Tukutane Dodoma juu ya hatima ya KATIBA MPYA tujue kimoja tangu hapo.
 
We might reject JK’s Constitution plan: CUF

Sunday, 02 January 2011

mtatiro.jpg

Acting deputy CUF’s secretary general for Mainland, Mr Julius Mtatiro addresses the journalist during the press conference held at the party’s head office in Dar es Salaam yesterday. Photo/ Edwin Mjwahuzi


By Florence Mugarula
The Citizen Reporter

Dar es Salaam. President Jakaya Kikwete’s proposed Constitution Review Commission stands to be rejected by Civic United Front (CUF) if it will focus on areas to be amended in the current constitution instead of seeking views and opinions to write a new document.

According to CUF’s acting deputy secretary general for Mainland, Mr Julius Mtatiro, the President has failed to clearly state whether he firmly stood for a total rewrite of the Constitution or he preferred mere amendments to the existing one.

On Friday President Kikwete announced the formation of a commission that would review the current constitution and seek the people’s views on what should be changed or improved.

The commission, President Kikwete said, will be headed by a prominent lawyer and will comprise other members from both Zanzibar and the Mainland representing people of different levels and interests.

But CUF has insisted that the President’s statement was not clear and that, until now, it was not yet established if the government was resolute on having a new constitution for the country or not.

“I think President Kikwete is using political tact to pacify Tanzanians who are demanding a new constitution. CUF is aware of this game and we will never accept any commission that is aimed at fixing patches to the current constitution,” Mr Mtatiro emphasised.

He said the President was supposed to be straightforward in his statement to avoid ambiguity so that the people could get a clear sense of the direction this issue is taking.

According to Mr Mtatiro, President Kikwete and his assistants were not speaking the same language because each of them had a personal view of the matter.

A few days ago, Constitutional Affairs and Justice minister, Ms Celina Kombani said the government was willing to work on amendments to the current Constitution but not writing a new one.

The minister argued that there was no budget allocated for the process of re-writing the Constitution.

In addition, the Attorney General, Judge Fredrick Werema recently remarked that here was no need for re-writing the constitution but there was room for stakeholders to come together with the government to make amendments to the current constitution.

Judge Werema, however, was criticized by a cross section of political leaders for opposing a complete overhaul of the constitution.

In wide-ranging interviews, politicians, members of civil societies, lawyers and academics rejected Judge Werema’s remarks observing that he had no power to oppose the people’s will.

Most of his critics described his remarks as “unfortunate” and said that he had demonstrated disdain for the public. They charged that the public and those in government could not tolerate his statement if they cared about issues that are people-centered.

According to CUF, it was obvious President Kikwete’s government was not committed to form a new constitution if governmental officials could not speak the same language.

“It does not come to mind when the President’s advisors on legal issues decide to announce their personal stand on the big issue like this, otherwise that convinces us to believe this government is not intending to listen to the people,” said Mr Mtatiro.

He added: “CUF advises President Kikwete to fire the AG and Minister Kombani because they will tarnish his government’s image in and outside the country. These people have already shown a negative attitude against majority Tanzanians who want a new constitution.”

Commenting to the matter, a prominent Dar es Salaam-based lawyer, Mr Yonathan Mbuga said the President’s idea was good but it was not clear if the plan was to form a new constitution or to maintain the current one.

Mr Mbuga, who is an advocate of the High Court, said forming a team to review the constitution and seeking the people’s views was a heavy task that required ample time for implementation.

“I suppose Tanzanians, especially politicians, decide to give the commission time to work carefully without pressure so that they can deliver something tangible. It has taken Kenya more than seven years to come up with a good and understandable draft of a new constitution,” suggested Mr Mbuga.

Meanwhile, CUF has condemned the Tanzania Electric Supply Company and the government for increasing power tariffs by 18.5 percent.

According to the party, the increase of the rates was due to the poor performance of Tanesco and some government officials who were involved in running the company.

Mr Mtatiro said the country was facing a problem of electricity shortage because the government and Tanesco were not creative enough to establish new sources for power generation.

“We cannot keep on depending hydro-power. What would happen if there were prolonged drought? I think Tanzanians must think of who is capable to lead this country to a successful future,” said Mr Mtatiro.

Alluding to this party’s analysis of the situation, Mr Mtatiro said CUF foresees a Tanzanian who currently pays Sh 80,000 a month for electricity will have to double the amount for the same monthly bill by 2015 because the government would hike the tariffs every year.
 
LET CONSTITUTION TEAM BE broad and INCLUSIVE

Sunday, 02 January 2011

katiba.jpg

Some have called it the President's New Year gift to Tanzanians, while others have seen it as a victory to the people against hard-nosed, conservative elements within the ruling class.

We are talking about President Jakaya Kikwete's New Year announcement to the effect that he is forming a commission to undertake a review that will kick-start the process to rewrite Tanzania's Constitution.

The announcement, as expected, has been widely applauded by Tanzanians of all walks of life. It is a big plus for the President, who now stands out clearly as a "leader who listens".

Coming as it has from the holder of the country's topmost political seat, the move puts paid to those who, for some hard-to-fathom reasons, were rubbishing the calls for constitutional change.

The debate now is no longer whether or not Tanzania will have a new constitution, for it is shifting to how the document will be prepared and when it will be ready.

A constitution, as we all know or should know, is the supreme law of the land. It provides, on the overall, for people's rights and the limitations to the enjoyment of those rights so that they don't interfere with the rights of others.

In a word, the Constitution takes care of the various laws, rules and regulations that determine the dos and the don'ts amongst the citizenry.

Whenever there is conflict on how certain laws are implemented, a reference to the Constitution sorts that out. Indeed, there are various laws that are in our current statute books, which, according to experts, are provided by the Constitution, yet they are outright "immoral". People are hungering for a new constitution that will get rid of such discrepancies.

The founding Father of the Nation is on record as having noted that the Tanzanian Constitution gives so many powers to the presidency that he might as well have been a dictator "without breaking the law".

No wonder, Tanzanians have been saying they can't afford the risk of holding on to a constitution that puts them at the mercy of their leader's benevolence.

They have been agitating for one that puts checks to all, the led and the leaders, from the grassroots to the presidency. They have been pushing for a Constitution that provides for leaders as opposed to rulers. And from the look of things, they are soon going to get it.

What some among us tend to forget, more so those who happen to be among the "powers that be", is that a Constitution is not about a section of the citizenry; it is about each and every member of the society.

It is also about posterity. Why? Today's holders of power would be grossly misguided if they would knowingly embrace a faulty constitution with relish, simply because it is operating in their favour, forgetting that power comes and goes. The Constitution is enduring.

Since Tanzanians in their generality are keen on a new constitution, it is our expectation that the review team will be broadly representative.

People are looking forward to a team that won't give room to murmurs that it comprises members who may succumb to manipulations by those with a huge stake in the current Constitution and hence, keen on retention of status quo.

Only a review outfit that is broad-based and enjoying the full confidence of all, will lead us to the writing of a document that every Tanzanian will be able to hold up proudly and say: This is our Constitution, serving me as well as much as it serves well all my fellow citizens.

 
Only a review outfit that is broad-based and enjoying the full confidence of all, will lead us to the writing of a document that every Tanzanian will be able to hold up proudly and say: This is our Constitution, serving me as well as much as it serves well all my fellow citizens.

Hii makala ina blaa blaa kibao lakini haitoi mwanga wowote............Swali la msingi ni kujaribu kujibu maswali ya ni namna gani watanzania watashirikishwwa katika kuiandika katiba yao?

Utaratibu uwe wa kisheria kwa kulishirikisha Bunge kabla ya mchakato hauljaanza au Bunge lije kuwa ni msimamizi na mratibu wa zoezi zima badala ya madaraka yake ya kisheria kutekwa na Ikulu ambayo haitambuliwi na sheria zetu kabisa kama ni chombo cha kututungia sheria na hii katiba ni sheria mama........................na hivyo inabidi tuwe waangalifu zaidi hapo...................
 
CUF wasichoelewa hadi hivi sasa ni kuwa JK hajatofautiana na kauli za Werema na Celina Kombani..........................Celina na Werema wanapinga Katiba mpya na kwenye hilo Jk anawaunga mkono kwa kuteua Tume ambayo itafanya kazi kwa maelekezo ya Ikulu na wala siyo ya Bunge............................................

Nawe usichoelewa ni kuwa kwa kuwa CCM ina uwingi mkubwa wa Wabunge, hakutakuwa na tofauti yeyote kwa tume kufuata maelekezo ya Ikulu au ya Bunge!!
 
Hii makala ina blaa blaa kibao lakini haitoi mwanga wowote............Swali la msingi ni kujaribu kujibu maswali ya ni namna gani watanzania watashirikishwwa katika kuiandika katiba yao?

Utaratibu uwe wa kisheria kwa kulishirikisha Bunge kabla ya mchakato hauljaanza au Bunge lije kuwa ni msimamizi na mratibu wa zoezi zima badala ya madaraka yake ya kisheria kutekwa na Ikulu ambayo haitambuliwi na sheria zetu kabisa kama ni chombo cha kututungia sheria na hii katiba ni sheria mama........................na hivyo inabidi tuwe waangalifu zaidi hapo...................

Nashangaa sana, kwani Kikwete alisema anaunda tume ya kuunda katiba?
 
CUF wasichoelewa hadi hivi sasa ni kuwa JK hajatofautiana na kauli za Werema na Celina Kombani..........................Celina na Werema wanapinga Katiba mpya na kwenye hilo Jk anawaunga mkono kwa kuteua Tume ambayo itafanya kazi kwa maelekezo ya Ikulu na wala siyo ya Bunge...........................

Uzoefu tulionao ni kuwa Tume ya Raisi ya marekebisho ya katiba mwishowe huzalisha viraka kwenye katiba ambavyo vinaridhisha kero za viongozi wa juu serikalini na wala siyo raia.................................

Sasa CUF badala ya kuunga mkono hoja ya JK kwa shingo upande wanapaswa kuikataa...........kwa sababu Tume hiyo haina nguvu ya kisheria na siyo shirikishi kwa sababu haikuchaguliwa na wabunge kutokana na sheria zilizopo ambazo zimeweka wazi ya kuwa kazi zote za serikalini zitatangazwa kwenye vyombo vya habari na kutoa fursa sawa kwa kila mtanzania kujitokeza na kupew nafasi sawa ya ushiriki..................................

Kwa kutofuata utaratibu huu wa kisheria ni kuwa Tume hiyo ni batili kwa sababu haikumshirikisha kila mtanzania katika kuiunda.........................Itakuwa ni Tume iliyochakachuliwa na kamwe haiwezi kutuandikia katiba mpya ila itapendekeza viraka kama serikali ya JK itakavyo..............................

Kubwa zaidi ambalo CUF na watanzania wote kwa ujumla wetu tunapaswa tusisahau ni kuwa CCM haikuwa na ajenda ya kuandika katiba mpya kwenye Ilani yake ya uchaguzi wao sasa iwaje leo tuiamini CCM na JK wake ya kuwa wana nia njema wakati hata utaratibu wa kuiandika katiba mpya hawataki kuufuata na wameanza kwa mikwara na kucheza faulo za waziwazi kabisa?

Wake up CUF and join the progressive forces clamouring for a new dawn in this nation, we gladly call home..................

I certainly agree with you RUTA, HAPA TUNATAKIWA KUMPA KILA SUPPORT MNYIKA ASONGE MBELE NA HOJA BINAFSI.Hata hiyo wiki moja aliyosema Mnyika ya ku-study mwenendo wa JK ni bure haina haja kwani tayari tume yake imeonekana haitakuwa na nguvu ya kisheria
 
Mnyika, shika breki ya kwanza Bungeni Dodoma kwa swala hili la Katiba Mpya. Ukumbuke, hiyo hoja ni yetu na wala sio mali yako binafsi hivyo kaipeleke kunakohusika mara moja bila kuchelewesha zaidi.
 
HOJA YA KATIBA: JK atiliwa shaka

• Maswahiba wake wadai ametumia madaraka ya katiba mbovu

na Waandishi wetu

KAULI ya Rais Jakaya Kikwete na utaratibu aliotangaza juzi kuwa utatumika kuitazama upya katiba ya sasa na kuandika mpya, vimetiliwa shaka na makundi ya Watanzania, wakiwemo watu wake wa karibu.

Baadhi yao, wakiwamo mawaziri, wamemkosoa Rais Kikwete kuwa ametoa tamko kuridhisha matakwa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Wanadai ametekeleza sera ya CHADEMA, kwa kuwa CCM katika ilani yake, hakikuwatangazia Watanzania kurekebisha katiba au kuandika katiba mpya.

Wanadai Rais Kikwete ameonyesha woga dhidi ya CHADEMA, na kwamba hakupata baraka za Baraza la Mawaziri kabla ya kulitangazia taifa kuwa anakubali kuandikwa kwa katiba mpya, jambo ambalo ni sera ya CHADEMA.

Baadhi yao, wakidai wanamfahamu vema, walisema hata hivyo, hawaamini kama kauli yake hiyo ni ya dhati. Wanadai inawezekana ameitoa ili kupunguza makali mjadala wa katiba mpya ulioanzishwa na CHADEMA.

Wanasema hata mwaka 2005 Rais Kikwete alianzisha Chuo Kikuu cha Dodoma baada ya kusikia Freeman Mbowe akisema CHADEMA itaugeuza mji wa Dodoma kuwa kitovu cha wasomi, mji wa vyuo vikuu; wakidai kuwa Ilani ya CCM haikuwa na ajenda ya kujenga chuo hicho.

Hata hivyo, wengine wamedai kuwa kwa jinsi wanavyomjua, Rais Kikwete anaweza kupiga danadana suala la katiba mpya kama alivyolifanya la Ofisi ya Kadhi Mkuu kwa miaka mitano, ili hata kama litakuja kujadiliwa na kutekelezwa, awe ameshastaafu.

Katika hali ya kuonyesha kukata tamaa, badhi ya viongozi hao waandamizi ndani ya serikali yake walifika mahali pa kuhoji alikopata mamlaka ya kutangaza kuunda tume ya kurekebisha katiba, kama alivyosema juzi kuwa ataunda tume chini ya mwanasheria aliyebobea.

Hata hivyo, baadhi yao walidai kuwa ingawa amekosea kiutaratibu, katiba hii mbovu inampa mamlaka ya kuunda tume hiyo.

Mmoja alisema: "Rais hajavunja katiba, ametumia mamlaka yale yale aliyopewa kwenye katiba mbovu ya sasa inayolalamikiwa. Kinacholalamikiwa sawa ni utaratibu alioutumia wa kutumia Constitutional Review Commission lakini wangehoji amepata wapi mamlaka ya kufanya hivyo…utakuja kule kule kwamba mamlaka hayo amepata kwenye katiba ya sasa ambayo tunasema ni mbovu, haifai...

"Wengine wanasema utaratibu huo ni kiini macho, ninachoweza kukuambia kwa sasa subiri uone yatakayotokea."

Mbali na hao, wengine wanaokosoa utaratibu huo, wanarejea tume kama hizo zilizowahi kuundwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na ile ya Benjamin Mkapa ambazo hazikuleta tija na Katiba iliishia kuwekwa viraka.

Juzi Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, alikaririwa akishauri kuanzishwa kwa Baraza la Katiba ambalo litakuwa na wajibu wa kuratibu kura za maoni ya wananchi juu ya uundwaji wa katiba mpya.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kitendo cha rais kutangaza kuunda tume ni kiini macho na kinadhihirisha hana nia ya kutaka kuundwa kwa katiba mpya.

Naye Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amesema anasubiri ufafanuzi wa serikali kuhusu mchakato wa katiba mpya, ili kujua kwa kina muundo wa tume hiyo ya Rais.

Mnyika alisema katika mazingira hayo anasubiri ufafanuzi wa serikali kuhusu mchakato husika ikiwemo kujua kwa kina muundo wa tume, hadidu rejea na kama serikali itapeleka bungeni mapendekezo kuhusu mchakato kabla ya kutoa kauli kuhusu hatma ya hoja binafsi ambayo alitaka kuiwasilisha bungeni katika mkutano wa Februari.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, alisema katika kipindi hicho ataendelea na hatua ambazo alizitangaza pindi alipokwenda kuwasilisha taarifa ya hoja kwa Katibu wa Bunge Desemba 27, mwaka jana.

"Hata hivyo, kutokana na kauli ya Rais Kikwete na hatua za ziada ambazo natarajia kutoka kwa serikali, nitatumia wiki ya kwanza ya Januari kukutana ana kwa ana na baadhi ya viongozi wa asasi za kiraia, taasisi za dini na vyama vya siasa ikiwemo chama chake (CCM) na kushauriana hatua za ziada za kuchukua," alieleza Mnyika.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa hoja hiyo, licha ya kuitwa hoja binafsi kwa kanuni za bunge, bado ni hoja ya umma, kwani katiba mpya ni hitaji la wananchi wote.

Mbunge huyo alieleza kuwa hatua ya kuwa na katiba mpya ni ya msingi, lakini historia ya taifa inaonyesha kwamba tume zilizoundwa na marais kushughulika masuala yanayogusa Katiba hazikuweza kukidhi matakwa ya wananchi.

Alisema kauli ya Rais Kikwete inaashiria kwamba wananchi hawatahusishwa moja kwa moja kwenye kuamua, badala yake tume itachukua maoni na baadaye maamuzi yatafanywa na bunge kama ilivyo kwenye marekebisho ya kawaida ya katiba kwa mujibu wa ibara ya 98 ya katiba.

Alisema pamoja na Rais Kikwete kukubali kuandikwa kwa katiba mpya bado Watanzania wanahitaji kujadili kwa kina na kwa haraka kuhusu mchakato uliopendekezwa ili taifa liende katika mkondo sahihi wa kuanza kutoa maoni.

"Ni muhimu kwa wadau wote kufahamu muundo wa Tume hiyo pamoja na hadidu rejea kwa kina, ili kuepuka taifa kuanza mchakato kwa njia isiyo kamili, jambo ambalo tunaweza ‘kuuziwa mbuzi kwenye gunia," alisisitiza Mnyika.

Hata hivyo, alieleza kuwa jambo la muhimu analopaswa kufahamu Rais Kikwete si kupatikana kwa maoni tu, bali uamuzi wa maoni ambayo ndiyo yanatumika kama msingi wa katiba mpya na makubaliano ya pamoja kuhusu misingi ya muhimu ya katiba mpya.

"Katika mazingira kama hayo ndipo panapohitajika umuhimu wa kuwa na mkutano mkuu wa taifa kabla ya mapendekezo ya katiba kupelekwa kwenye mamlaka za kikatiba ambazo kwa mujibu wa katiba ya sasa ibara ya 98 ni Bunge pekee.

"Ni muhimu kwa mchakato wa sasa kufanyika kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na kuwekewa utaratibu bayana, ikiwemo kuitaka tume yoyote itayoundwa kutumia mfumo wa Green Paper, ili wananchi waanze kutoa maoni yao kuhusu masuala kipaumbele badala ya kuathiriwa kimsimamo na serikali au tume yenyewe," alisema.

Alieleza kuwa kwa sasa hatufanyi marekebisho ya katiba bali tunafanya mapitio (review) na hatimaye kuwa na katiba mpya, hivyo suala la ushirikishwaji wa umma si katika kutoa maoni bali kuamua misingi muhimu ya katiba ili kuwa na katiba inayokubalika na umma.

Katika hatua nyingine, Chama cha Wananchi (CUF) kimemshauri Rais Kikwete kuwapumzisha Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, kutokana na kauli zao za ‘kuropoka' kuhusu suala la kuundwa kwa katiba mpya iliyopingana na kauli yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Ofisi Kuu za chama hicho Buguruni Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu Bara, Julius Mtatiro, alisema Rais anatakiwa kuwapumzisha kwa kuwaondoa nyadhifa zao, ili wasiendelee kutia doa jeusi katika utawala wake uliojaa kila aina ya matatizo.

"Tunampa rais ushauri wa bure juu ya watendaji wake waliionekana ‘kuropoka' mambo ya kuwakatisha tamaa Watanzania juu ya katiba, ni muda muafaka sana kwa rais kuwapumzisha Selina Kombani na Jaji Werema wasiendelee kuongeza doa katika utendaji wake," alisema Mtatiro.

Hata hivyo, alisema CUF imeunga mkono kauli ya rais ya kuanzisha mchakato wa katiba lakini imetilia mashaka aina ya katiba ambayo rais anaitaka kutokana na maneno ambayo aliyatumia katika hotuba yake akinukuu kauli ya rais ' jambo la nne ambalo tulilokubaliana kufanya ni kuanzisha mchakato wa kuitazama upya katiba ya nchi yetu kwa lengo la kuihusisha ili hatimaye tuwe na katiba inayoendana na taifa lenye umri wa nusu karne'.

Alisema kutokana na kauli hiyo imewapa utata mkubwa kwa kuwa rais hakusema wazi anasimamia lipi kati ya katiba mpya na kuweka viraka kwa katiba iliyopo.

Mtatiro alisema mashaka makubwa yapo kwa rais mwenyewe kutofautiana na watendaji wake ambao wamekuwa wakitofautiana katika suala hilo akiwemo Kombani na Werema. "Sote tunajua kuwa rais wetu hana utaalamu na mambo ya kisheria, inapotokea watendaji wake wa karibu na wataalamu wa sheria wanatofautiana naye kimtazamo kiasi cha wao kusema hadharani misimamo yao halafu rais naye anakuja na msimamo wake, inaleta mashaka makubwa sana," alisema Mtatiro.

Alisema kauli iliyotolewa na Kombani ya kwamba katiba mpya kwa sasa haiwezekani kabisa, kwani si muhimu na kuwa serikali haina bajeti ya kushughulikia katiba mpya, imeonyesha udhaifu kiutendaji wa waziri huyo bila kujali kwamba serikali ina bajeti ya kununua mashangingi ya mawaziri kwa kutumia mabilioni ya pesa.

Alisema muda wa kuchezeana shere umepita, hivyo Ikulu itoe ufafanuzi wa kauli ya rais ili wadau na Watanzania wote wajue wataangukia kwenye kauli ipi kati ya Waziri Kombani au Werema.

"Ni mategemeo (matarajio) ya CUF kuwa rais atakidhi matakwa ya Watanzania walio wengi ambao wanahitaji kwa dhati pawepo na katiba mpya itakayoandikwa upya ili kukidhi kizazi cha sasa na tunamtahadharisha rais na watendaji wake kuwa CUF itapinga juhudi zozote za serikali kuunda kamati ya marekebisho ya katiba itakayoenda kufanya kazi ya kutia viraka katika katiba iliyopo, sisi tunahitaji mpya na si vinginevyo," alisema Mtatiro.
 
Butola kama hoja yako hii ingelikuwa na mashiko leo Edward Lowassa angeendelea kuwa Waziri Mkuu................
Nawe usichoelewa ni kuwa kwa kuwa CCM ina uwingi mkubwa wa Wabunge, hakutakuwa na tofauti yeyote kwa tume kufuata maelekezo ya Ikulu au ya Bunge!!


Wabunge wa CCM usifikiri ni sawasawa na sukuma wiki.......nao wanalitakia taifa hili mema...........................hawatakuwa tayari kuvunja sheria kama JK anavyoliekeza taifa hili................kuunda Tume ya kurekebisha sheria bila ya Bunge kutunga sheria ya kuruhusu mchakato mzima uwe umejikita kwenye sheria...........................
 
Wabunge wa CCM usifikiri ni sawasawa na sukuma wiki.......nao wanalitakia taifa hili mema...........................hawatakuwa tayari kuvunja sheria kama JK anavyoliekeza taifa hili................kuunda Tume ya kurekebisha sheria bila ya Bunge kutunga sheria ya kuruhusu mchakato mzima uwe umejikita kwenye sheria...........................

RUTASHUBANYUMA! USIWAAMINI SANA WABUNGE WA ccm!!! sisi tuendelee na mchakato kama vile hawapo! wakituunga mkono, tutashukuru, lasivyo, tutashukuru pia!

nilifadhaika sana walipopiga makofi wanachadema walivyotoka nje ya ukumbi wa bunge! nikajihisi sipaswi kuwa mwana ccm. ndipo nilipohama kuwa mshabiki wa chadema hadi kada wa chadema!
 
Ila ifike sehemu Rais awe anazungumza na waandishi wa habari/wananchi na kuulizwa maswali,hii lack of clarity inatupa tabu,then iwepo timeframe manake hashindwi kuanza kazi ya kuunda tume 2015,na hapo ndo tutakapoelewa pia kama yeye na Kombani na Werema wanatofautiana au la.Yeye hakusema ataunda tume ya kuunda katiba mpya bali kushughulikia mabadiliko katiba ambayo kwa maoni yangu haina tofauti na zilizokuwepo before zikaweka hivyo vinavyoitwa viraka.
Kwenye suala la wabunge wengi wa CCM,nguvu ya umma ikiwa kubwa na Civil Society na tukapata pia support ya international community na organs,hawatakuwa na la kufanya zaidi ya kupitisha mapendekezo ya walio wengi.Ni strategies tu zinatakiwa kwenye hili.
 
nafikiri JK alikuwa wazi kuwa haundi tume ya katiba mpya ila ya kufanyia marekebisho katiba ya sasa, hivyo bado ni viraka tu vinavyosubiriwa. landa tofauti na tume za nyalali na kisanga ni mfumo wa kukusanya maoni na wingi wa maeneo yanayotarajiwa kuwemo kwenye hadidu za refea amabazo bado hazijawekwa wazi na hali inaonekana most likely kwa zitakuwa na maeneo mengi zaid ya tume zilizopita. pia ikumbukwe pia kuwa katiba mpya si ajenda ya ccm na haikuwemo kwenye ilani yake so hayo ni madadiliko tu ya katiba na sio katiba mpya. binafsi sioni utata wa kuhitaji ufafanuzi kwani naona kla kitu kiko wazi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom