Kauli ya Chiligati kuigharimu CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya Chiligati kuigharimu CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kibajaj, Jun 3, 2011.

 1. k

  kibajaj Senior Member

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vyombo mbalimbali vimekuwa vikiripoti vipaumbele vya bajeti ya mwaka mpya wa fedha. Suala ambalo limekuwa na mvuto zaidi ni kukatwa kwa posho za vikao kwa wabunge ambapo ni sehemu ya bajeti ya upinzani.

  Hapa hakika tumeona jinsi baadhi ya wanasiasa katika nchii walivyo walafi na ni namna gani wanasiasa hawa hawana utu kwa raia ambao ndiyo waliowaweka madarakani. Naibu katibu mkuu wa chama cha MAPINDUZI bwana JOHN CHILIGATI ametoa kauli inayoonyesha jinsi asivyo na utu na pia jinsi asivyo mzalendo.

  Kauli ya kwamba Zitto anataka umaarufu kwa vile sitting allowance zimepunguzwa na kusema wazi kuwa CCM watachukua posho hizo na kama wapinzani hawataki waache ni kauli mbovu sana kwa kiongozi wa ngazi ya juu kama yeye.

  Ikumbukwe kwamba mshahara wao uko palepale, posho nyingine ziko palepale na wakiwa bungeni wanalipiwa gharama zote muhimu. Kauli hii imedhihirisha wazi kuwa hata hii kampeni ya kujivua gamba ni danganya toto.

  Wenzetu Ulaya wanapunguza matumizi sisi tunaongeza kwa mambo yasiyo na msingi? Mtu alipwe milioni saba gari ya zaidi ya milioni sitini marupurupu kibao bado ashindwe kuwa na utu hata chembe moja? Jeuri ya pesa hizi ndiyo imewahamisha majimboni wako hapa mjini wakijivinjari.
  Jamani tembeeni Tanzania kuna umaskini mkubwa sana.

  Mbunge akilipwa milioni saba adundulize ajinununlie gari lake mwenyewe kwanza atakuwa na uchungu nalo na atalitunza.
  Kwa kauli hii ya Chiligati anazidi kuiweka CCM matatani.

  "AFRICA POLITICS IS AN INVESTIMENT JUSTFY"​
   
 2. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #2
  Jun 3, 2011
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  mmhu!!
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,669
  Trophy Points: 280
  Ccm ipo kwaajili ya kufilisi nchi,kwanza when it comes politics ya nchi hii huwa natamani kulia,imeoza na walioiozesha ni ccm!
   
 4. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kibajaj, sheikh wangu. Si kwamba Chiligati ametoa kauli ya kupinga wazo la kupunguzwa kwa posho kwa nguvu kubwa ki-hivyo kwa bahati mbaya.

  Kumbuka, Wabunge wengi wa CCM wana madeni makubwa sana wanayodaiwa kutokana na pesa waliyokopa wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi. Maana wengi walitumia pesa nyingi sana kutoa rushwa ili waweze kupata ubunge. Mategemeo yao makuu yapo kwenye hizo posho wanazolipwa ndizo zinazowasaidia kulipia madeni yao pamoja na mali waliyoweka dhamana wakati wanakopa.

  Kwa hiyo kumtegemea Mbunge wa CCM eti aunge mkono hilo wazo ni Ndoto ya Mchana.

  Hawa jamaa hawana ubinaadamu hata kidogo! Hata hali ya maisha ya Mtanzania iwe mbaya kivipi hawako tayari kujitoa ili kuokoa jahazi

  Lakini ndio watu mliowapigia kura hao!!

  Chiligati ana roho mbaya kama sura yake! Hana tofauti na Chenge!
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hawa wabunge wa ccm sijui wako kwa mslahi y a nani?:smow:
   
 6. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nampongenza Chiligati amekua muwazi kabisa! Tumeshudia unafiki wa Wabunge wa Upinzani kama aliofanya Dr Slaa aliwahi kusema mshahara ni mkubwa kwa wabunge lakini kaenda mtaani anataka alipwe vile vile! Pia wakati bunge hili lina anza kulikua na habari ya milioni 90 ya magari Wabunge wa upinzani walichukua hela hiyo! Naona ni kujitafutia umaarufu tu hakuna lolote ni unafiki!
   
 7. k

  kibajaj Senior Member

  #7
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "we need a TANZANIAN who will work for TANZANIA in TANZANIA for TANZANIA and TANZANIANS"
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,591
  Likes Received: 4,702
  Trophy Points: 280
  Hongera Mheshimiwa sana Chiligati, umesaidia saaaaaaaana wananchi wa Tanzania kukifahamu Chama Cha Maulaji.Hivi sasa picha ya jinsi CCM mulivyo inaonekana bila chenga.Well done Chilly.
   
 9. vunjo

  vunjo Member

  #9
  Jun 3, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  We mlengo wa kati hebu toa hilo GAMBA limebaki miguuni.Mi namuunga mkono zitto na kamati yake hizo posho hazina mana kabisa mana mshahara wanapata hicho ndio chanzo chakuweka vikao visivyo na misingi yoyote ili kula hizo posho.
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,184
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  kwani ni lazima kuchangia kila kitu
   
 11. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,591
  Likes Received: 4,702
  Trophy Points: 280
  Matumbo yao mkuu.
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280


  Chadema uzi ni ulele.Watanzania wote wameshaona ukweli nia yenu ni nini.Kwa wingi wao bungeni watawashinda kwa hoja hii,lakini siku zao zinahesabika.Bravo mbowe! Bravo Slaa ! Bravo Zitto!! Aluta continua.Tunaomba wakati wabunge wakiwa bungeni Dr Slaa na akina Marando na Mpendazoe wafanye ziara mikoani kuelezea bajeti ya upinzani na uzuri wake.Hongera Mbowe kwa kumteua Zitto kwenye nafasi ya waziri kivuli wa fedha,anafaa sana!!​
   
 13. delabuta

  delabuta Senior Member

  #13
  Jun 3, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha unafiki wako wewe mlengo wa kati hujui usemalo mnafiki ni wewe kwani unajua unayasema but unajifanya huelewi.nyie ndio serikali na maposho yote mlijiwekea nyie wezi ccm. sasa cdm tunasema muziondoe ila kama mkikataa tutazichukua kwani nyie ndio mlioweka huo wizi. sasa unafiki uko wapi? bora silaa aliyesema anapata Tshs. ngapi kwa mwezi mbona mukama amegoma kusema anapata ngapi kwa mwezi? sasa nakuuliza slaa na mukama fisadi nani? naona huna details tulia tu.
   
 14. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapa tunataka tuone wabunge wa chadema wakisusia hizo posho au wakidirect katika miradi ya maendeleo.
  Wasitupige changa la macho kama kwenye mishahara ya wabunge.
  Hatakama magamba watakaa hilo pendekezo, magwanda waonyeshe mfano!
   
 15. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  swali ni hili, sitting allowance ya nini? mbona hoja ipo clear,wewe mlengo wa kati? Mind, wanapata mshahara (7 Milioni/month) na posho zingine nono nne wakati wao wote wa ubunge sasa iweje wakienda Dodoma kwenye kikao wapate sitting allowance? au wakiwa Dodoma wanakuwa transformed from monogastric to ruminants (tumbo 1 hadi matumbo manne)?
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,325
  Likes Received: 19,492
  Trophy Points: 280
  Serikali inatarajia kutumia Sh. trilioni 12.8 kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, kati ya hizo Sh. trilioni 8.8 ni kwa matumizi ya kawaida, yaani posho na mishahara na ulaji mwingine, wakati fungu la maendeleo ni Sh. trilioni nne tu.

  Utaratibu wa kupitisha bajeti ya ulaji umekuwa ni utamaduni wa taifa hili, kwani hata mwaka huu wa fedha unaomalizika serikali ilipitisha bajeti ya Sh. trilioni 11.6, kati yake Sh. trilioni 7.7 zilikuwa kwa fungu la kawaida na Sh. trilioni 3.8 kwa ajili ya maendeleo.

  Soma maoni yetu ukurasa wa sita.
   
 17. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,184
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Nafikiri imeshaelezwa sana kuw akwa namna mfumo ulivyo wakisusia wao pesa zinazudishwa kwa mtoaji ambaye ni serikali na inaweza kuamua kufanya lolote

  Hii ni kama uko kweney kikao labda cha halmashauri na wengi wenu labda mkagomea posho na wengine wakapokea nyie mliokataa hamuwezi kuilazimisha halmashauri iwatengee mfuko maalum wa kuweka posho zenu ili zikafanye au kwenda kwenye mradi wowote pale halmashauri ndio yenye mamlaka ya kufanya lolote na zile posho mlizozikataa.

  So hata hapa wabunge wa upinzani wakisusia pesa zinarudishwa serikalini na wabunge hao hawatakuw ana uwezo wa kuamua lolote na hizo pesa
   
 18. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi kwani na huyu ni Mbunge wa CCM??........msidanganyike kwenye suala la Maslahi Wabunge Wote ni Wamoja, hayo mengine ni siasa tu.

   
 19. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,184
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  yaani ni upuuzi ambao haujapata kuonekana
  Trl 8.8 kwa ajili ya posho na mishahara na maendeleo ambayo ni barabara, kilimo, umeme, huduma za afya, elimu, na miundo mbinu yote kiujumla ya tanzania nzima ni trl 4 kweli tanzania zaidi ya uijuavyo
   
 20. k

  kibajaj Senior Member

  #20
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  mkuu tunomba utupatie amount kwa wabunge tu if possible.
   
Loading...