singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
WAKATI umefika kwa Watanzania sasa kusema imetosha. Tunataka wenzetu waliokabidhiwa dhamana ya kuongoza mashirika, taasisi, idara na kampuni mbalimbali za umma na kuzitumia kwa manufaa yao binafsi badala ya kufikiria manufaa mapana ya wananchi wote wa Tanzania, walielewe hili.
Ripoti ya mwaka 2014/15 ya Mdhibiti na Mkuguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad iliyopewa nafasi inayostahiki na vyombo vya habari karibu vyote imebainisha wazi ni jinsi gani taasisi hizo za umma zilivyokuwa zinanyonywa kwa mabilioni ya shilingi na watu wachache bila chembe ya huruma.
Kati ya halmashauri 164 zilizokaguliwa mahesabu zake ni 47 tu ndizo zimepata hati safi huku nyinigine 117 zilizosalia zikiwa na hati zenye mashaka, zisizoridhisha na chafu. Ni mabilioni mangapi yametiwa mifukoni mwa wajanja wachache ndani ya halmashauri hizo?
Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa imebainika kuwepo kwa wafanyakazi hewa waliolipwa mishahara wakiwemo watoro na waliokufa na kiasi cha Sh bilioni 2.7 katika kipindi hicho zimechotwa.
Madudu mengine yaliyobainika na ripoti ya CAG ni pamoja na mikataba yenye kukiuka taratibu za manunuzi katika kampuni ya UDA na Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), misamaha ya kodi, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuingiza nchini bidhaa za Sh bilioni 4.6 bila kufanyiwa ukaguzi.
Nyingine ni mita za kupima mafuta katika Mamlaka ya Bandari (TPA) kutotumika na hivyo kushindikana kufanya udhibiti wa mapato ya serikali na dawa za thamani ya Sh bilioni 2 za Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ambazo hazikuwa kwenye kumbukumbu zikionesha tu kwamba bado ziko njiani kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili lakini hazijafika tangu mwaka 2012. Orodha ni ndefu.
Hakuna ubishi kwamba orodha ya tasisi hizo za umma zilizojikita katika kutafuta namna ya kufanya mavuno yao binafsi iko ndefu katika orodha ya CAG kiasi kwamba wakati mwingine ni vigumu kuamini kwamba hayo yote yamefanywa na watumishi wa umma walioaminika kutekeleza kazi za umma, lakini kwa makusudi kabisa wakajitengenezea njia nzuri ya ulaji wao binafsi.
Hakuna lugha nyingine nje ya kusema huo ni ufisadi wa hali ya juu. Tunapenda kuunga mkono hoja iliyotolewa na CAG kwamba wakati umefika sasa kwa mafisadi wathibitishe wenyewe mali zao badala ya kazi hiyo kufanywa na vyombo vya dola kama ilivyo hivi sasa ili kudhibiti au kumaliza kadhia hii ya kufuja mali za umma kwa maofisa waliopewa dhamana ya kuongoza taasisi hizo.
Safari bado ndefu lakini itoshe tu kusema kwamba wabunge wetu walione hili, walijadili na kuliwekea mkakati wa kuhakikisha kwamba linatekelezwa ili waliotufanya watanzania wote tuendelea kuishi katika umasikini zaidi kutokana na wenzetu kujinufaisha wao peke yao litokomezwe.
Vita bado ni changa lakini sote ni mashahidi jinsi majemedari wetu wakiongozwa na Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli wanavyotekeleza kwa vitendo vita dhidi ya mafisadi na bila shaka siku itafika kwa wahusika nao kupata wanachostahili mbele ya vyombo vya haki. Kamwe tusikate tamaa mpaka kieleweke.