Kauli ya a.mrema juu ya baraza jipya la mawazili

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,711
2,224
“Yaani hawa mawaziri naona wangekuwa na barua za kujiuzuru mkononi ili watakapovurunda iwe ni kukabidhi barua hizo na kuachia ngazi.
Ni kweli baraza ni kubwa, lakini kama kutakuwa na uwajibikaji, sidhani kama kutakuwa na tatizo, ila kama wakilala, hapo ndio mambo yatakapoanza kuwaharibikia,” alisema Mrema.

Mrema alimpongeza Rais Kikwete kwa kuwateua Magufuli na Anna Tibaijuka akisema kuwa ni watendaji wazuri."


Mzee wa kilalacha nae hajaacha zile zama zake za kuwapa watu notice za ndani ya wiki
 
Limbukeni huyo, mwacheni hawezi "kuuma" hapa Tanzania tena.Anatafuta tu maslahi yake jamani
 
Hana mpya huyo keshapoteza muelekeo.tatizo kila siku anaongea pumba sasa hata kama siku nyingine akaweka mazuri,utapata shida ya kuchambua kwani pumba ndio nyingi
 
Mzee wa Kiraracha ni uzee unamsumbua ataongea sana kipindi hichi akijaribu kurudisha atention aliyokuwa nayo wakati akiwa Naibu waziri Mkuu. Mnaomsikiliza amani iwe kwenu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom