Kauli 'TATA' ya Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi ''Mimi ni mkristo Mkatoliki..., mtanizoea taratibu'

Kakumamoto

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2015
Posts
1,497
Reaction score
2,214
Your browser is not able to display this video.


Akitoa salam za pole Mh. Nchimbi alisema yeye ni Mkristo Mkatoliki hivyo watamzoea taratibu. Wakumzoea taratibu ni waombolezaji au wale wote wanaosema yuko kimya kwa yanayoendelea nchini kuanzia mauaji ya tarehe 29?

Alisema kwa taratibu za kanisa Katoliki Baba Askofu anapokuwepo Makamu wake hawezi kuzungumza, hivyo na yeye kwakuwa Rais yupo ataongea kidogo sana.

Lakini kwanini aseme yeye ni Mkristo Mkatoloki tutamzoea taratibu?

Tutamzoea taratibu katika lipi?!
 
Nchimbi ni kiongozi anayepaswa kukuta kila kitu kipo tayaria Halafu aambiwe endelea

Hana uwezo wa kuvuta vitu na kuvistahilisha ni mtu mwepesi kutumika vyovyote

Wao waliomkaimu pale wanajua vizuri tu kuwa hana madhara

Nyota yake ni kushikana na mazuri tu, ubaya hauwezi Labda wakuiga ni watu wanaochanganyikiwa wakifanya ubaya

Yupo pale kusafisha Nyota ya waovu
 
Vatican ndio inaongoza dunia
 
Hivi ukiwa mwanaume na watu wanakujua ukisema ''mimi ni mwanaume'' ni kauli tata?

Ukiwa mwanamke ukisema wewe ni mwanamke ni kauli tata?

Au ukiwa amiri jeshi mkuu ukisema wewe ni amiri jeshi mkuu ni kauli tata?

UKitafakari kwa utulivu ukiangalia utagundua Nchimbi na bosi wake wote ni wale wale wana insecurity ,tofauti yao ni ndogo sana sababu wapo chini ya mfumo mmoja.
 
Nimebahatika kusikia mahubiri ya Padre kuhusu ndoto yake nimewaza mengi.... Ila nimegundua kitu kuwa

Maisha na Imani hazikutaki uonekane kuwa wewe unastahili zaiiidi kuliko wengine, hapana! Bali inatufundisha kuwa wanyenyekevu siyo tu' kwa Muumba Bali hata kwa wanadamu tunao ishi na kukutana nao....

Nanukuu maneno yake, anasema alikaa kwenye kituo Cha huduma zaidi ya mwaka mzima lakini hakuwahi kufahamu mtu anayeomba Misa Kila Dominika ni nani lakini alipoulizia kumfahamu alielekezwa location anazopenda kukaa huyo muhusika mwishowe akaja kughundua kumbe muumini huyo ni JJM.

Wale wakuziba masikio na Kupayuka kama hamkuelewa mahubiri ya Paroko... Kamwe hata wangewalaza na kuwafunika na vitabu vya Dini kamwe hamtoelewa umuhimu wa unyenyekevu na kunyenyekeza kwa Mungu na kwa wanadamu.

Mfano wa unyenyekevu nimeuona pia kwa Mh. Vice

Mungu wa mbinguni awasimamie wote wanaoheshimu na kuupa thamani, UTU, UBINADAMU na UHAI wa wengine bila kujali wana nafasi gani hapo walipo.

Niwatakie Dominika Njema

Location

Kigali, Rwanda
 
Who are you JJM?
 
Ndivyo tafakuri yako inavyosoma juu ya hotuba ile?

Twaweza tofautiana kidogo.

Mimi nilitafsiri kama hotuba ile ni dongo kwa mashehe na wale wote wanaomuona kuwa ananyamazia kusemea mambo ya hovyo yanayofanyika nchini kwa sasa.

Jibu lake akawa kawajibu kwa mfumo huo: 'hawezi kupanua kinywa chake akiwa ni makamu wakati Rais yupo'.
 
Uko sahihi sana Maste👊
 
Nakubaliana na wewe mkuu.
Tafsiri yako ni sahihi hujakosea ila tujiulize madongo au mafumbo na mapisho kipindi hiki yanaliponya taifa? Madongo yanapunguza makali au yanaongeza chumvi kwenye kidonda?

Ndio maana nikasema tofauti yao na bosi wake ni ndogo sana wakiwa chini ya mwamvuli mmoja.

Ukatoliki pamoja na uislamu havipaswi kuwa gumzo kipindi hiki sababu watanzania hasa watanganyika wameumizwa bila kujalisha dini zao.

Tukifanikiwa kuwapuuza hao majamaa katika issue ya udini watarudi nyuma na kujitafakari upya.

Nchimbi Emmanuel muda unavyozidi kwenda atapoteza control na hao wa upande wa pili watakuwa wamefanikiwa kumvuta acheze ngoma na midundo yao bila kupenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…