Kauli nzito za viongozi wa nchi

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Jikumbushe baadhi ya kauli nzito za viongozi wa nchi hii na utafakari aina ya viongozi wako.

1. "Ndege ya Rais lazima inunuliwe hata kama wananchi watakula nyasi"..... Mh. Basil Mramba akiwa Waziri wa fedha
2. "Pesa zilizopo katika account yangu nje ya nchi ni Vijisenti tu"................Mh Andrew Chenge akiwa waziri M/Mbinu
3. "Ukitaka biashara yako iende vizuri peperusha bendera ya CCM".............Mh. Fredrick Sumaye akiwa Waziri Mkuu
4. "kelele za wabunge kudai mawaziri wajiuzulu ni upepo wa siasa tu"........Mh. Jakaya Kikwete ( Rais)
5. "Asieweza kulipa nauli ya kivuko Kigamboni apige mbizi"........................Mh. John Magufuli (waziri Miundombinu)
6. "Kama madaktari hawatatii Mahakama, basi! Liwalo na liwe"....................Mh. Mizengo Pinda (Waziri Mkuu)
7. "Ulitaka nisiende bungeni ili posho hiyo apewe baba yako".....................Mh. Stephen Wasira (Waziri/Mbunge)

Unaweza kuongeza kauli kama hizo maana bado siamini kama waliozitoa walikusudia au waliropoka tu!

Je ni kweli tabia za viongozi inawakilisha tabia walizonazo wananchi?
 
Back
Top Bottom