Ni upumbavu kuwaza eti itaondolewa au haitachaguliwa.
Kwani una uhakika gani sasa hivi imechaguliwa?
Pili ni nani anaiondoa serikali iwapo vikwazo vinawaathiri wananchi wa kawaida?
Nani mwananchi wa kawaida ana uwezo wa kuiondoa serikali?
Hao wenye uwezo wa kuiondoa ndio hao wanaofaidika na hata kidogo kilichopo.Hata nchi ikiwekewa vikwazo vigumu kiasi gani,hao wanaoiweka serikali madarakani hawatakosa mkate wala maji.
Unadhani wakifa wananchi wa kawaida ndipo kuna mtu atashituka?Kwa nini hamuangalii mifano ya nchi nyingine kama Zimbabwe?
Yule Mzee Mugabe hadi kaingia miaka 90 anatawala...jaribu kumpa wa kwetu hata 85 tu!