Kauli huumba! Je, ni kweli Magufuli ni dikiteta? Kama ni kweli, ni kosa la nani kati yake na aliyetoa kauli hii?

Kauli huumba! Je, ni kweli Magufuli ni dikiteta? Kama ni kweli, ni kosa la nani kati yake na aliyetoa kauli hii?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,101
Reaction score
128,716
Wanabodi,

Kuna hoja kuwa kauli huumba. Yaani ukitoa kauli fulani, kauli hiyo inakuwa na nguvu za kuumba, hivyo huko mbele inakuja kukiumba kitu hicho kilichosemwa au kilichozungumzwa.

Hili likitokea, kosa ni la nani kati ya kilichotokea na aliyekiumba kwa kauli?.

Kama ni kweli kauli huwa zinaumba, kuna hii kauli kuwa Tanzania itatawaliwa na dikiteta, na kama rais Magufuli kweli ni dikiteta, then sio kosa lake kuwa dikiteta, kwa sababu huo udikiteta hakujiumbia yeye, bali uliumbwa kwa kauli kuwa tutatawaliwa na rais dikiteta!.

Sikiliza kwa makini clip hii, kisha ujibu maswali yafuatayo

Jee ni kweli Tanzania tuko under dictatorship?,
Kama ni kweli, jee kosa ni la nani?,
Ni la dikiteta aliyepo ambaye hakujiumba, bali aliumbwa, au ni kosa la kauli yenye nguvu, iliyotuumbia huo udikiteta?.

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade ...
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's ..
Mwito Kwa Wana JamiiForums Kuhusu Ukosoaji wa Rais Magufuli ..

Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...

Kufuatia hoja hii kuwa kauli huumba, hivyo kuna uwezekano mkubwa, kuwa rais Magufuli sio dikiteta, lakini kufuatia kauli zinazotolewa za kumuita dikiteta na kujirudia rudia, hivyo ndizo zimemuumbia udikiteta, hivyo Watanzania wote, tukibadili kauli zetu badala ya kumuita rais Magufuli ni dikiteta, sasa tumuite ni Malaika Magufuli, ili kauli hizi za malaika, zimuundie umalaika, rais Magufuli ageuke malaika, hivyo kuligeuza taifa letu kuwa ni peponi.

Mnaonaje hili?.

Nawatakia Jumatatu Njema.

Paskali
 
Nafikiria labda hiyo video nmesikia au kuelewa vby mwalim anasema tusiogope maana tukiogopa kumueleza ukweli kiongozi anavunja sheria za nchi tutatawaliwa kiongozi Dikiteta. Tayari wengi tulikuwa tunawategemea kusema mnaogopa ww mwenyewe unaogopa bunge letu mahakama zetu zinaogopa nchi inaendeshwa kwa mamuuzi ya muhimili moja tu kutoka magogoni...
 
Wanabodi,

Kuna hoja kuwa kauli huumba. Yaani ukitoa kauli fulani, kauli hiyo inakuwa na nguvu za kuumba, hivyo huko mbele inakuja kukiumba kitu hicho kilichosemwa au kilichozungumzwa.

Hili likitokea, kosa ni la nani kati ya kilichotokea na aliyekiumba kwa kauli?.

Kama ni kweli kauli huwa zinaumba, kuna hii kauli kuwa Tanzania itatawaliwa na dikiteta, na kama rais Magufuli kweli ni dikiteta, then sio kosa lake kuwa dikiteta, kwa sababu huo udikiteta hakujiumbia yeye, bali uliumbwa kwa kauli kuwa tutatawaliwa na rais dikiteta!.

Sikiliza kwa makini clip hii, kisha ujibu maswali yafuatayo

Jee ni kweli Tanzania tuko under dictatorship?,
Kama ni kweli, jee kosa ni la nani?,
Ni la dikiteta aliyepo ambaye hakujiumba, bali aliumbwa, au ni kosa la kauli yenye nguvu, iliyotuumbia huo udikiteta?.

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Jumatatu Njema.

Paskali

Ngoja niisikilize tena kwa sikio la rohoni labda nitaelewa!
 
Paskali ndugu yangu. Una uelewa wa mambo kiupana sana tena sana. Kwa kutambua hilo, naomba nikuulize kwanza maana ya dikteta ni nini? Hili neno liko kwenye kamusi zetu? Je, haiwezi kuwa rungu la wakubwa ambalo linatumika kusambaratisha umoja wa vinchi vidogo kama haka ka kwetu?

Ni kweli sisi tunaongozwa na dikteta? Kwa dalili au vipimo vipi? Ukiwa Baba wa familia na ukaamka na kumkuta mtoto wako hapo nyumbani hajaenda shule na anachezea midoli au anaumba ng'ombe wa udongo na angalau ukatata kufahamu kwa nini hajaenda shule na akakujibu hataki utafanyaje?

Nafahamu ni lazima utatumia nguvu kwa kuwa kama mzazi utakuwa unafahamu umhimu wa shule. Hapo hujawa dikteta? Ni dhahiri utakuwa dikteta japo dhamira yako itakuwa sahihi na ya kumuokoa mwanao ili asipate madhila huko mbeleni. Lakini pia kuna mifano mingi sana hapa ninaweza kuitoa ikiwemo ya viongozi waliopachikwa majina ya udikteta na mpaka wakaondoshwa madarakani na wengine kuuwawa kama wanyama. Tanzania hatuna dikteta wala hatujampata wa kufanana nae. Mwalimu pia aliwahi kuitwa dikteta na hao hao wanaojaribu kupenyeza hii kitu sasa.

Hakika si watu wema kwetu. Wana mbinu lukuki za kutuvuta mashati. Ukitaka mkeo akuheshimu ni lazima asiwe na uwezo wa kujipatia kipato chake Paskali. Akiwa na kazi yake na akajitosheleza wewe hutoweza kumwambia akupikie ugali usiku wa manane na kama huamini jaribu utakuja unioe mrejesho. Hizi ni propaganda kama demokrasia nk.

Tuziepuke tujenge nchi yetu. Tuna kiongizi mfia nchi tumuungee mkono. Hii ni bahati hatutaiona kirahisi naamini hivyo. Nyerere aliitwa dikteta lakini angalau yeye hakuwahi kukubali hayo na yawezekana hakuwa dikteta bali ni mzazi alietaka mtoto asichezee maboksi siku ya shule badala yake aende shule akasome ili kutengeneza maisha yake ya baadae.

Tusikubali msemo wa "wenzetu" UK au USA. Hao si wenzetu maana wana utamaduni tofauti na sisi na hawatakuja kuwa wenzetu milele.

Watakusifia ukishindwa na kamwe hawatakupenda ukiwa na dalili za kushinda. Ukijiweza maana yake hawatakunyonya tena.
 
Wanabodi,

Kuna hoja kuwa kauli huumba. Yaani ukitoa kauli fulani, kauli hiyo inakuwa na nguvu za kuumba, hivyo huko mbele inakuja kukiumba kitu hicho kilichosemwa au kilichozungumzwa.

Hili likitokea, kosa ni la nani kati ya kilichotokea na aliyekiumba kwa kauli?.

Kama ni kweli kauli huwa zinaumba, kuna hii kauli kuwa Tanzania itatawaliwa na dikiteta, na kama rais Magufuli kweli ni dikiteta, then sio kosa lake kuwa dikiteta, kwa sababu huo udikiteta hakujiumbia yeye, bali uliumbwa kwa kauli kuwa tutatawaliwa na rais dikiteta!.

Sikiliza kwa makini clip hii, kisha ujibu maswali yafuatayo

Jee ni kweli Tanzania tuko under dictatorship?,
Kama ni kweli, jee kosa ni la nani?,
Ni la dikiteta aliyepo ambaye hakujiumba, bali aliumbwa, au ni kosa la kauli yenye nguvu, iliyotuumbia huo udikiteta?.

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Jumatatu Njema.

Paskali

Mkuu Paskali, hiyo clip yako hapo Mwalimu Nyerere alikuwa ana state facts, hakuwa anafanya unabiii au kuchuria, he was merely stating the known facts.

Magufuli ni dikteta, na hilo ni tatizo la John Magufuli. NUKTA.

Upande wa pili kuna tatizo la mfumo (system) ambao ni dhaifu na butu haukufanya kazi ya vetting thoroughly. Hakuna namna Magufuli angeshika hata nafasi ya 10 kati ya wagombea 11, kwa sababu track record yake Wizara "alizotawala" ilikuwa mbaya na chafu. Hizo takwimu za kukariri ambazo zilimpa umaarufu zilipaswa kupitishwa kwenye tanuru ili dhahabu ijulikane na makinikia yajulikane.

Ukitaka kujua ubaya wake sikiliza kauli zake anapotafuta sympathy au ego-satisfaction hasa kwa kutumia zile cheap and stereo-typed popular slogans zake za uzalendo, upendo, tumbua nk nk. Ule ni unafiki wa kiwango cha Hollywood. Unafiki na chuki ni tabia zake Magufuli asisingiziwe mtu mwingine awaye yote. Anatakiwa akubali huo udhaifu kisha ajirekebishe (ni process) sio kusema aombewe. Udikteta wake alianzia kwenye familia yake na maisha yake yote amekuwa uchwara, hata kwenye Wizara alizotumikia.

Tunaomkosoa Magufuli, wengi tuna point kwenye hizo facts za Mwl. Nyerere tu. Wengi hatumkosoi kwa kumchukia bali kwa kuonyesha na kuianisha bayana madhaifu yake, ila kiburi chake kimemfanya ashindwe kusikia na kujirekebisha.
 
Mkuu Paskali, hiyo clip yako hapo Mwalimu Nyerere alikuwa ana state facts, hakuwa anafanya unabiii au kuchuria, he was merely stating the known facts.

Magufuli ni dikteta, na hilo ni tatizo ni la Magufuli. NUKTA.

Upande wa pili kuna tatizo la mfumo (system) ambao ni dhaifu na butu haukufanya kazi ya vetting thoroughly. Hakuna namna Magufuli angeshika hata nafasi ya 10 kati ya wagombea 11, kwa sababu track record yake Wizara "alizotawala" ilikuwa mbaya na chafu. Hizo takwimu za kukariri ambazo zilimpa maarufu zilipaswa kupitishwa kwenye tanuru ili dhahabu ijulikane na makinikia yajulikane.

Ukitaka kujua ubaya wake sikiliza kauli zake anapotafuta sympathy au ego-satisfaction hasa kwa kutumia zile cheap and stereo-type popular slogans zake za uzalendo, upendo, tumbua nk nk. Ule ni unafiki wa kiwango cha Hollywood. Unafiki na chuki ni tabia zake Magufuli asisingiziwe mtu mwingine awaye yote. Anatakiwa akubali huo udhaifu kisha ajirekebishe (ni process) sio kusema aombewe. Udikteta wake alianzia kwenye familia yake na maisha yake yote amekuwa uchwara, hata kwenye Wizara alizotumikia.

Tunaomkosoa Magufuli, wengi tuna point kwenye hizo facts za Mwl. Nyerere tu. Wengi hatumkosoi kwa kumchukia bali kwa kuonyesha na kuianisha bayana madhaifu yake, ila kiburi chake kimemfanya ashindwe kusikia na kujirekebisha.
Nimekuelewa
 
Sidhani kama kuna mtu anazuwiwa kusema. Watu wanatukana badala ya kusema. Si haki. Watu wajifunze kukosoa constructively na si destructively. Kuna tofauti kati ya "njoo hapa ya lugha ya ukali na njoo hapa hiyo hiyo ya lugha ya kistaarabu.
 
Kiongozi yeyote isipokuwa wa Kidini lazima awe Dictator.

Julius Kambarage Nyerere naye alikuwa Dictator mzuri tu.

Kama sio Dictator huwezi kuongoza watu.

Hata wewe Baba unayeongoza familia ni lazima awe Dictator la sivyo utaamshwa asubuhi na Hausegirl ili ukadeki chooni.

Kama Kiongozi lazima uwe na nguvu ya kufanya maamuzi magumu ili kuitetea Falsafa yako ya uongozi ambayo baadhi ya watu wataipinga au itawaumiza, lakini kama kiongozi utailazimisha ifanyike.

Ili kutetea Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, Mwalimu Nyerere alitaifisha kwa lazima miradi mikubwa ya watu binafsi na majengo yao ya thamani, na taasisi kama za elimu na afya na mashirika binafsi.

Nyerere alilazimisha watu kuyahama makazi yao na kwenda kuishi katika vijiji vya ujamaa na kuwafanyisha kazi kwa lazima katika mashamba ya ujamaa.

Hayo ni baadhi mambo machache aliyoyafanya ili ku Dictate siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

Kiongozi yeyote katika ngazi ya Uraisi ni lazima awe Dictator ndio maana lazima alaumiwe na watu wanaoathirika na maamuzi yake.

Wenyeviti wote wa vyama vya Siasa Tanzania ni Ma-Dictator pia.
Waangalie kwa umakini

Freeman Mbowe
Ibrahim Lipumba
John Cheyo
Agustine Mrema
James Mbatia

Wote ni Madictator

Kama sio Dictator huwezi kuongoza hata familia ya watu wawili. Yaani wewe na mkeo.
 
Kuna moja nimeisikia jana ITV baada ya taarifa ya habari katika kale ka kipengele ka "wosia wa baba wa taifa" nikaona yule mzee aliona mbali sana, was a real GREAT THINKER, sikushangaa niliposikia taarifa ya kurugenzi ya ikulu kuwa mheshimiwa hatahudhuria kumbukizi ya baba wa taifa!!
 
Wanabodi,

Kuna hoja kuwa kauli huumba. Yaani ukitoa kauli fulani, kauli hiyo inakuwa na nguvu za kuumba, hivyo huko mbele inakuja kukiumba kitu hicho kilichosemwa au kilichozungumzwa.

Hili likitokea, kosa ni la nani kati ya kilichotokea na aliyekiumba kwa kauli?.

Kama ni kweli kauli huwa zinaumba, kuna hii kauli kuwa Tanzania itatawaliwa na dikiteta, na kama rais Magufuli kweli ni dikiteta, then sio kosa lake kuwa dikiteta, kwa sababu huo udikiteta hakujiumbia yeye, bali uliumbwa kwa kauli kuwa tutatawaliwa na rais dikiteta!.

Sikiliza kwa makini clip hii, kisha ujibu maswali yafuatayo

Jee ni kweli Tanzania tuko under dictatorship?,
Kama ni kweli, jee kosa ni la nani?,
Ni la dikiteta aliyepo ambaye hakujiumba, bali aliumbwa, au ni kosa la kauli yenye nguvu, iliyotuumbia huo udikiteta?.

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Jumatatu Njema.

Paskali

Paskali, I do not see any philosophical arguments that can be raised in your proverb " Kauli huumba" with reference to Mwalimu's speech you have posted; and making a link with the so called udikiteita wa Magufuli.
Ronal Reagan, post #10 amekujibu vizuri.
 
Kuna moja nimeisikia jana ITV baada ya taarifa ya habari katika kale ka kipengele ka "wosia wa baba wa taifa" nikaona yule mzee aliona mbali sana, was a real GREAT THINKER, sikushangaa niliposikia taarifa ya kurugenzi ya ikulu kuwa mheshimiwa hatahudhuria kumbukizi ya baba wa taifa!!

Aisee kweli Mkuu Kivyako? Duh kweli tuna kazi kubwa sana mbele yetu
 
Back
Top Bottom