Kauli hizi za Zitto zinatupa picha gani?

Mkandara.

...

Kusema Kikwete kashindwa si kweli hii ni dhana dhaifu kabisa ,nitakuwa nawe pamoja ukiniambia WATANZANIA tumefeli na kiongozi akiwa Kikwete.

Hii nafikiri ndiyo kauli mbiu sahihi.

Kulaumu watanzania kwa matatizo ya Kikwete, good but not that good kinda spin
 
MkamaP,
Mkuu unapotaka kuongoza watu amabo ni wagumu kuongozeka ni lazima uwe na mikakati inayoweza kuvunja hizo nguvu zao za ULIMBUKENI..kinyume cha hapo kwa nini uligombea uongozi ukijua fika haiwezekani. Bila shaka nawe unakuwa kundi moja na wao au sio?..
Nitakwambia kitu kimoja, matatizo yote ya Wadanganyika kama ulivyoyaorodhesha yapo kweli na sii makubwa kama unavyofikiria kwani ni rahisi kuongoza watu wa aina hiyo kuliko wale wanye mwanga tayari, meaning ni rahisi sana kuongoza Tanzania kuliko kuongoza Marekani au nchi yoyote siokuwa na matatizo hayo. reason behind hawa ni wasomi wanajua undani wa kila hoja yako na wanaweza kuiichambua hata kama ina mafao.. Tanzania ni nchi ya bora liende kama team ya Mpira..watu maskini unaweza kuwachezesha peku na mpira wa plastic lakini sii vinginevyo.. tatizo la viongozi wetu wanataka tucheze na njumu wakati wananchi wenyewe hawajawahi vaa viatu maishani mwao..

Kikwete alichotakiwa kuelewa ni kwamba mambo yote hayo uloandika yanatokana na UMASKINI wa Hali na MALI na hakuna njia pekee ya kuwaongoza watu hawa isip[okuwa kuweka mikakati ya kuwawezesha kisha kuwabebesha wao jukumu la maisha yao na nchi yao wenyewe. Ni sawa na baba mzazi mwanao anapokuwa anapotoka huwezi kumwacha ati dunia itamfunza na kuendelea kudai kwamba you have done everthing possible kumwezesha, ili hali hata siku moja hujakaa kitako na kujiuliza nini matatizo ya mwanao au hata kumuuliza yeye mwenyewe. Na kosa kubwa ni pale wazazi wanapofikiria kwamba wao ndio wanafahamu kulea and knows what a child need, he is what makes the family! na Haiwezekani kuwa kinyume.

Na hakika marais wote wa kiafrika hufanya wanavyofikiria wao badala ya wananchi wanavyotaka kuongozwa..Uongozi nchi zetu ni kutawaliwa na sii mawazo ya pamoja kufikia malengo tulokusudia kwani hata huyo rais na viongozi wote ni sehemu ya population ya nchi.
 
Mkuu haya ndio maswali yanayotakiwa... Na ajabu ni kwamba unasema all you can say now ni hivyo tu wakati kodi ya wananchi ilitumbuliwa. Mimi katika kumbukumbu yangu namkumbuka sana Mnyika alipokuwa akipiga vita swala la Zitto kuingia katika kamati ile, na kisiasa hata mimi niliunga mkono, Zitto mwenyewe hakuona makosa hata kidogo..Matokeo yake ndio haya, Zitto amejifunza nini kutokana na makosa yale ndilo swala la kuuliza.. imekwisha tokea.

Ameulizwa hilo swali hapa na hajawahi kutoa straight answer

Pili, nakuomba endeleza maswali ambayo yanajenga mjadala kwa manufaa ya umma hata kama wao watashindwa kujibu ama watakuja mbogo... Sisi wasomaji tutapima majibu yao nahwasa maadam wao wako huko juu ktk kamati ndio rahisi sana kuwaondolea points kama vile Invinsible anavyonilimba mimi kila siku ya Mungu!

Mkandara,

Tofauti yako na mimi ni kuwa, wewe unatumia lugha ya kistaarabu kwa kila jambo. Mimi ninajibu stupidity kwa stupidity. Yaani mimi siamini katika kugeuza shavu la kulia baada ya kusalabwa shavu la kushoto.

Mtu akija kwangu na upuuzi na yeye anapata upuuzi right away. Mtu akija hapa na kudai kuwa chadema ni chama cha kikatoliki au cha kikabila wakati ukweli unaonyesha vinginevyo, unategemea nimjibu nini?

Mtu akijadili issues (kama wewe hapa), atapata majibu mazuri toka kwangu. Lakini akileta pumba na udaku (kama ndugu yangu mkamaP), basi atapata tu pumba na udaku toka kwangu.

Mkuu wangu wewe au mimi hatuwezi kumwondolea Zitto umaarufu isipokuwa yeye mwenyewe.. Kama heshima ilivyo Zitto ndiye pekee anayeweza kujenga au kubomoa umaarufu wake.

Mkandara,

Naona umenunua pia propaganda ya kina Omar kuwa mimi namuonea wivu Zitto kwa umaarufu aliokuwa nao. Kwa taarifa yako, mimi nimewahi kuishi marekani na ulaya kwa muda. Nimejifunza jinsi wanasiasa wanavyoweza kuporomoka ndani ya muda mfupi sana.

Kuna kina Howard Dean (US), Gordon Brown na Tony Blair, Kuna Bush na hata kuna Kikwete wa Tanzania. Umaarufu wa wanasiasa sio kitu cha kuchezea kamari (bet on).

Unaweza kupotea muda wowote - na mara nyingi wanasiasa wanajimaliza wenyewe kama Obama alivyoanza kujimaliza mwenyewe. The same will be kwa Zitto - Buzwagi, Dowans, na kadhalika.

Ninampinga Zitto kama Zitto na wala sijali kama ana umaarufu or not maana Zitto sio MUNGU.
 
Tukiachana na matusi au kutokubaliana tatizo langu kwako MkamaP, ni hii hali ya kila wakati kuona CCM safi JK safi. Tangu lini ukawa na mtu wa aina hiyo au chama cha aina hiyo.

Jaribu ku-balance mambo na argument ili usionekana kama aliyekuwa mkuu wa Chuo Cha CCM kivukoni.

Mkuu safi sana.
Tatizo la kambi ile wao wanataka kukulazimisha ukubali mawazo yao,ukigoma kukubali mawazo yao basi umetumwa na RA na vinginevyo, kambi hiyo hiyo iko mstari wa mbele kuita watu mafisadi mwingine akiyatumia maneno hayo hayo kwa vipimo vile vile basi anaambiwa anatoa matusi na ahakikishe maneno yake maana mahakama haijaamua vile sasa nachoshindwa kuelewa siku hizi mahakama ni SLAA ama CHADEMA.? wao wakisema ndo tayari imethibitika .Inasikitisha sana.

Tukirudi ktk hoja yako
Si kweli kwamba mimi nimtazamo wangu kwamba ccm ni sawa na wala mie sio ccm ngoja nikuhakikishie,ila kambi ile ndo kwa vile wanaona natofautiana nao basi ili kuuwa hoja zangu wamenibatiza kuwa mie ni ccm, kwa kawaida hua sina taratibu ya kujitetea sana nikikwambia ukakubali sawa ukikataa sawa na ndio maana sijibu sana mtu anaponihusisha na ccm.Kifupi mkubwa ni propaganda zile zile chadema wanazotumia kuwamaliza akina Chacha,Kabouru,Zitto,na wengine ndivyo hivyo hivyo wanavyotumia kurusha hapa makobora kwa watu wanaopingana nao hapa.

Mie ni mtazamo wangu huru kwamba si ccm wala Kikwete waliofelisha Taifa hili ,ni sisi watanzania tumefeli tunatakiwa kutambua hilo badala ya kurusha matatizo kwa wengine.

Huko nyuma niliwahi kusema kwamba wakati wa Nyerere hakukua n ufisadi na kama ulikuwepo basi kwa kiwango cha chini sana ,still nchi ilikuwa masikini mno ,unakumbuka maduka ya ushirika?? kununua sukari na chumvi lazima kupanga mstari?? unazikumbuka sabuni za mangwanji??

Nyerere mwenyewe aling'atuka moja ya sababu ukiangalia kwa makini ni kushindwa kwake kunatokana na sisi na ujinga wetu.Maana kama sikosei kuna mwandishi wa BBC alimuuliza Nyerere umeng'atuka kwa sababu sera imefeli na wewe umefeli pia Nyerere alijibu hivi.

Yesu Mnazareti alikuja hapa Dunia akihubiri jamani msizini, Lakini leo hii watu wanazini sana na akamuuliza yule mwandishi je unaweza sema Yesu alifeli kwa sababu watu wanazini?

wewe unamwelewa je ? Nyerere kwa mfano huo.
 
Mwafrika,
Tofauti yako na mimi ni kuwa, wewe unatumia lugha ya kistaarabu kwa kila jambo. Mimi ninajibu stupidity kwa stupidity. Yaani mimi siamini katika kugeuza shavu la kulia baada ya kusalabwa shavu la kushoto.

Mtu akija kwangu na upuuzi na yeye anapata upuuzi right away. Mtu akija hapa na kudai kuwa chadema ni chama cha kikatoliki au cha kikabila wakati ukweli unaonyesha vinginevyo, unategemea nimjibu nini?

Mtu akijadili issues (kama wewe hapa), atapata majibu mazuri toka kwangu. Lakini akileta pumba na udaku (kama ndugu yangu mkamaP), basi atapata tu pumba na udaku toka kwangu.
Duh kumbe hunijui hivyo.... mimi mtu aje na upuuzi! mtumeeee amekwisha lakini siku zote sizungumzi personal life ya mtu.. matusi yangu huwa hayahusiani kabisa na maisha ya mhusika hata kama namjua vizuri. Nitasema vitu vya kufikirika tu!
 
MkamaP,
Mkuu unapotaka kuongoza watu amabo ni wagumu kuongozeka ni lazima uwe na mikakati inayoweza kuvunja hizo nguvu zao za ULIMBUKENI..kinyume cha hapo kwa nini uligombea uongozi ukijua fika haiwezekani. Bila shaka nawe unakuwa kundi moja na wao au sio?..
Nitakwambia kitu kimoja, matatizo yote ya Wadanganyika kama ulivyoyaorodhesha yapo kweli na sii makubwa kama unavyofikiria kwani ni rahisi kuongoza watu wa aina hiyo kuliko wale wanye mwanga tayari, meaning ni rahisi sana kuongoza Tanzania kuliko kuongoza Marekani au nchi yoyote siokuwa na matatizo hayo. reason behind hawa ni wasomi wanajua undani wa kila hoja yako na wanaweza kuiichambua hata kama ina mafao.. Tanzania ni nchi ya bora liende kama team ya Mpira..watu maskini unaweza kuwachezesha peku na mpira wa plastic lakini sii vinginevyo.. tatizo la viongozi wetu wanataka tucheze na njumu wakati wananchi wenyewe hawajawahi vaa viatu maishani mwao..

Kikwete alichotakiwa kuelewa ni kwamba mambo yote hayo uloandika yanatokana na UMASKINI wa Hali na MALI na hakuna njia pekee ya kuwaongoza watu hawa isip[okuwa kuweka mikakati ya kuwawezesha kisha kuwabebesha wao jukumu la maisha yao na nchi yao wenyewe. Ni sawa na baba mzazi mwanao anapokuwa anapotoka huwezi kumwacha ati dunia itamfunza na kuendelea kudai kwamba you have done everthing possible kumwezesha, ili hali hata siku moja hujakaa kitako na kujiuliza nini matatizo ya mwanao au hata kumuuliza yeye mwenyewe. Na kosa kubwa ni pale wazazi wanapofikiria kwamba wao ndio wanafahamu kulea and knows what a child need, he is what makes the family! na Haiwezekani kuwa kinyume.

Na hakika marais wote wa kiafrika hufanya wanavyofikiria wao badala ya wananchi wanavyotaka kuongozwa..Uongozi nchi zetu ni kutawaliwa na sii mawazo ya pamoja kufikia malengo tulokusudia kwani hata huyo rais na viongozi wote ni sehemu ya population ya nchi.

Mkuu
Kinadhalia nafikiri unaweza sema kama unavyosema
Lakini ki hali halisi kuongoza Marekani ni rahisi mno kuliko kuongoza mkoa mmoja tu watanzania.

1.Wamarekani wote wanatambua majukumu yao na nini wanakitaka yani hata wakifanya demostration mara nyingi wanafanya asubuhi kabla ya saa za kazi na mda wa kazi ukifika basi wote wamo makazini.Hawa watu wanafanya kazi.

2.Watanzania wanaamini Kikwete anaweza print fedha akawajaza mapesa mfukoni .Hii dhana pekee inatosha kabisa kufanya kuongoza wilaya moja ya Tanznia kuwa ngumu kuliko kuongoza nusu marekani.
 
Mwafrika,
Duh kumbe hunijui hivyo.... mimi mtu aje na upuuzi! mtumeeee amekwisha lakini siku zote sizungumzi personal life ya mtu.. matusi yangu huwa hayahusiani kabisa na maisha ya mhusika hata kama namjua vizuri. Nitasema vitu vya kufikirika tu!

Ha ha ha ha,

Nimekumbuka uliwahi kusema kuwa utamtumia mamba wa ukerewe mtu yeyote atakayekuletea upuuzi.
 
Wakuu Mjadala mzuri ukiacha hapa na pale ambapo watu wanaingiza mzaha.

Hivi kwanini Zitto, Zitto,Zitto? kwanini sio Halima, Halima, Halima au Owenya, Owenya, Owenya?

Jibu itakuwa kuwa Zitto ni maarufu kuliko hao wengine au zitto ana mawazo tofauti na viongozi wa chama.

Lakini kama ana mawazo tofauti (kama ni kweli) wameshindwa kuyamaliza kimya kimya?, jibu utaambiwa hapana hawajashindwa ila marafiki wa Zitto kisiasa wanatoa siri magazetini au utaambiwa Zitto anatumiwa na RA kuimaliza Chadema.

Mimi nionavyo tatizo sio Zitto, tatizo ni Viongozi na waasisi wa Chadema kutokuwa tayari kusikiliza mawazo mbadala ya Zitto, vilevile tatizo lingine ni marafiki wa Zitto kisiasa.

Ndivyo nionavyo
 
Wakuu Mjadala mzuri ukiacha hapa na pale ambapo watu wanaingiza mzaha.

Hivi kwanini Zitto, Zitto,Zitto? kwanini sio Halima, Halima, Halima au Owenya, Owenya, Owenya?

Subiri tu hao kina Owenya na Halima nao wakifanya aliyofanya Zitto basi utaona kinachotokea.

Jibu itakuwa kuwa Zitto ni maarufu kuliko hao wengine au zitto ana mawazo tofauti na viongozi wa chama.

Kama ingekuwa ni umaarufu wa Zitto, nadhani mjadala ungekuwa kwenye umaarufu wa Zitto na sio kwenye issue kama buzwagi au dowans.

Lakini kama ana mawazo tofauti (kama ni kweli) wameshindwa kuyamaliza kimya kimya?, jibu utaambiwa hapana hawajashindwa ila marafiki wa Zitto kisiasa wanatoa siri magazetini au utaambiwa Zitto anatumiwa na RA kuimaliza Chadema.

Ukishakuwa na mawazo kuwa kila anayempinga Zitto hapa ni kiongozi wa chadema, basi utakimbilia kwenye ushauri kuwa haya yajadiliwe kwenye vikao vya siri kama mnavyojaribu kufanya huko CCM.

Hayo ya wasaidizi wa Zitto, sidhani kama wamesema tofauti na alichosema Zitto hapa na kwenye vyombo vya habari kuhusu Chadema wakati wa huu uchaguzi uliopita.

Mimi nionavyo tatizo sio Zitto, tatizo ni Viongozi na waasisi wa Chadema kutokuwa tayari kusikiliza mawazo mbadala ya Zitto, vilevile tatizo lingine ni marafiki wa Zitto kisiasa.

Ndivyo nionavyo

Ni kweli ni maoni yako, mawazo mbadala ya Zitto hayo ni yapi yasiyotajwa? Kila mara nasikia kuwa kuna mawazo mbadala ya Zitto. Ni yapi? ya kununua na kisha kutaifisha dowans au yapi?
 
MkamaP,
Mkuu walimu Kiuchumi Alishindwa! Na huwezi kumfananisha kabisa na Yesu kwa sababu ya Uasherati ni kufur ya mtu mmoja mmoja katika matendo yake. Yesu alikuwa kutupa mwongozo ambao leo umepokelewa na zaidi ya watu billioni mbili. huo ni mshindi mkubwa sana.

Matatizo ya Tanzania yanaaza na Uongozi, watu ni sawa na wachezaji tu wa pira ambao inategemea na wamepata mazunzo kiasi gani kuweza kucheza Mpira huu tena basi katika maendeleo ya nchi hakuna kushinda hivyo kipimo cha maendeleo ya wananchi na nchi yao ni wananchi wenyewe.

Hivyo hata siku moja huwezi kuziweka lawama kwa kipimo.. Nchi itasemekana imeendelea ni kutonana na WATU wake..hivyo kaa ingekuwa sisi ndio tunaweza badilisha hali hiyo sidhani kama tungekuwa nyuma ya Marekani.

Mkuu wangu ni lazima tukubali makosa yetu yametokana na UONGOZI bora, China ambao majuzi tu walikuwa Makomunist wa kutupa leo hii wanapiga hatua kiasi kwamba hata Marekani wenyewe wanaogopa na amini maneno yangu Population kubwa ya China hawana elimu nje ya dunia yao wenyewe. Lakini hawa walitegeneza mazingira ambayo yaliweza kukaribisha resources toka nje kuingia nchini mwao.. WATU kama sehemu kubwa ya sababu ya maendeleo yao ni wachapa kazi pindi kazi zinapokuwepo tena kwa malipo hafifu kuliko sehemu yoyote dunani..Ukitazama Investment za Wageni China, sheria zilizopo na hata ushirika wao kwa nchi nyingine utasema haiwezekani kabisa China kuwa hapo ilipo na ndio maana wachumi wengi wa nchi za magharibi wanasema maendeleo ya China ni sawa na puto tu..

Sii kweli, policies sio msingi wa maendeleo yua China ina isipokuwa mazingira yake kwa kuzingatia pia watu wake ndio maana investment zinamiminika ndani kiasi kwamba China imekuwa the main exporter duniani with iembalance trade fareness to any country...
Lakini imefikia dunia haina choice nan hata hao Marekani wanaagiza mali toka China kuliko wao wanavyouza kwao..China wame set standard ya biashara kwa sababu wametambua vipaji, uwezo na maliasili zao wakaziweka ktk hali ya kuhitajika. Wananchi has nothing ktk kuiweka China hapom ilipo isipokuwa ni wajenzi waliowezesha mikakati ya Uongozi wao kufanikiwa.
 
Subiri tu hao kina Owenya na Halima nao wakifanya aliyofanya Zitto basi utaona kinachotokea.

Mwafrika, sidhani kama kwa Lucy Owenya itakuwa hivyo na nadhani hawezi kuwa na mawazo mbadala maana ni family member.

Kama ingekuwa ni umaarufu wa Zitto, nadhani mjadala ungekuwa kwenye umaarufu wa Zitto na sio kwenye issue kama buzwagi au dowans.?

Niambie ni wapi ulipoona watu wanamjadili Abdallah Mchafukoge yule msukuma mkokoteni pale Manzese, au watu wanamjadili FairPlayer mwenye duka la mbao hapa Mbagala.

Ukishakuwa na mawazo kuwa kila anayempinga Zitto hapa ni kiongozi wa chadema, basi utakimbilia kwenye ushauri kuwa haya yajadiliwe kwenye vikao vya siri kama mnavyojaribu kufanya huko CCM.?

U got it wrong buddy, mie ndio nimekusafisha kule kwenye thread ya Zitto na Dr Slaa kuwa wewe sio Halima, najua wewe sio kiongozi chadema na kama una maana ya viongozi Chadema halisi, basi ni kweli kuna ka msuguano kati yao na Zitto, hilo lipo wazi hata Abdalaah Mchafukoge ambaye wewe humjui anajua hilo

Hayo ya wasaidizi wa Zitto, sidhani kama wamesema tofauti na alichosema Zitto hapa na kwenye vyombo vya habari kuhusu Chadema wakati wa huu uchaguzi uliopita.?

Hapana marafiki wa Zitto kisiasa wanaROPOKA sana, Zitto haropoki kama wao hasa huyo Kafulila

Ni kweli ni maoni yako, mawazo mbadala ya Zitto hayo ni yapi yasiyotajwa? Kila mara nasikia kuwa kuna mawazo mbadala ya Zitto. Ni yapi? ya kununua na kisha kutaifisha dowans au yapi?

Naona hukuisoma ile thread ya Zitto kugombea Uenyekiti, kaisome tena Kitila Dr alielezea wazi kuwa kuna WANACHAMA wenye mrengo wa kulia na wenye mrengo wa kushoto chadema.

Karibu kama una lingine, leo UMEME UPO HAPA MBAGALA
 
Mkuu
Kinadhalia nafikiri unaweza sema kama unavyosema
Lakini ki hali halisi kuongoza Marekani ni rahisi mno kuliko kuongoza mkoa mmoja tu watanzania.

1.Wamarekani wote wanatambua majukumu yao na nini wanakitaka yani hata wakifanya demostration mara nyingi wanafanya asubuhi kabla ya saa za kazi na mda wa kazi ukifika basi wote wamo makazini.Hawa watu wanafanya kazi.

2.Watanzania wanaamini Kikwete anaweza print fedha akawajaza mapesa mfukoni .Hii dhana pekee inatosha kabisa kufanya kuongoza wilaya moja ya Tanznia kuwa ngumu kuliko kuongoza nusu marekani.
Basi wewe ndio hufahamu kitu..Toka Nyerere , Mwinyi, Mkapa, JK na viongoizi wote wa Kiafrika hakuna hata mmoja wao angeweza hata kushika madaraka ya County moja.
Mbali na kusema hivyo, huwezi kuongoza nchi yenye kuelewa mrengo ni kitu gani kwani huwezi hata kusema maneno yanayojichanganya. Tanznia unaweza sema wewe ni Mjamaa kama hao CCM na siasa za Ujamaa na Kujitegemea kisha wakafanya vinginevyo na wananchi bado wakakupa hongera kwa uongozi.
Mkuu wangu, usemayo wewe ndio ya kinadharia kwa sababu ikiwa JK ataongoza Marekani basi hizo demostration hazitakuwa za kupima tena itakuwa hadi mfanyakazi wa IKULU ana stage demo. Marekani unapoahidi kufanya jambo vyombo vyote vinajiandaa kutokana na sera zako.. huwezi kusema utaondoa tatizo la Umeme watu wakajenga kisha ukategemea wao wanunue generators, maji wakachimbe visima na kadhalika..Ukweli ni kwamba Watanzania wanafanya mengi kwa mikono yao kuliko serikali yao hali Marekani kila kitu kina msingi, unachotakiwa wewe ni kujenga ukitakacho.. Fikira kitu chochote Marekani, hata iwe kufyatua fedha basi mwananchi anaweza na sii kufikiria Kikwete.
Watanzania wanafikiria Kikwete anaweza chapisha fedha kwa sababu hakuna njia za kupata fedha zaidi ya KUIBA na KUCHAPISHWA..ni kutokana na umaskini wetu ndio unajenga mawazo hayo..Mkuu wangu binadamu tunaelemikika kutokana na mazingira yaliyowazunguka..Ndio kama wazungu kwa utajiri wao wanvyofikiria unaweza kumfuga Simba kama pet kwani ukali wake unatokana na kukosa mapenzi, ukampenda Simba kwa mapenzi yote kuliko mwanao, hawezi kukushambulia.
 
Mwafrika, sidhani kama kwa Lucy Owenya itakuwa hivyo na nadhani hawezi kuwa na mawazo mbadala maana ni family member.

Family member kwa wanaomjadili Zitto hapa au kwa kina nani hasa?

Niambie ni wapi ulipoona watu wanamjadili Abdallah Mchafukoge yule msukuma mkokoteni pale Manzese, au watu wanamjadili FairPlayer mwenye duka la mbao hapa Mbagala.

Hili ni jukwaa la siasa la JF. Huyo Mchafukoge angekuwa mwanasiasa Tanzania, basi angejadiliwa hapa.

Kumbuka kuwa Chenge anajadiliwa sana hapa, je Chenge anajadiliwa kwa sababu ya umaarufu?

U got it wrong buddy, mie ndio nimekusafisha kule kwenye thread ya Zitto na Dr Slaa kuwa wewe sio Halima, najua wewe sio kiongozi chadema na kama una maana ya viongozi Chadema halisi, basi ni kweli kuna ka msuguano kati yao na Zitto, hilo lipo wazi hata Abdalaah Mchafukoge ambaye wewe humjui anajua hilo

Nimeona kazi yako kule na nimekupa bonge ya THANKS. Nilichosema hapo ni kuwa, ukishakuwa (hapo kwenye u, weka mtu yeyote yule) na mawazo kuwa anayemjadili Zitto ni kiongozi wa chadema, basi objectivity inaisha.

Hapana marafiki wa Zitto kisiasa wanaROPOKA sana, Zitto haropoki kama wao hasa huyo Kafulila

Hapa nitaacha historia ya Zitto itoe evidence.

Naona hukuisoma ile thread ya Zitto kugombea Uenyekiti, kaisome tena Kitila Dr alielezea wazi kuwa kuna WANACHAMA wenye mrengo wa kulia na wenye mrengo wa kushoto chadema.

Niliisoma na nikaielewa, kutofautiana mtizamo ni kitu cha kawaida. Hivi karibuni kwenye uchaguzi wa US, Obama na Clinton walipingana kwa miezi sita. Je hii ilisababishwa na matatizo ndani ya Democratic Party au ilikuwa tu process ya kawaida?

Karibu kama una lingine, leo UMEME UPO HAPA MBAGALA

Nitakuwa Mbagala weekend hii. Jiandae twende Zanzibar wote tukawekeze sasa maana Karume na Hamad wameshikana mikono.
 
Nikianza na la maana,

Hata Pasco nimemwambia nitakuwa Zenji tarehe kumi na sita December, lengo ni kufungua duka la mbao huko pia. Karibu zenji

Soma PM yako

Back to Zitto, YES umaarufu wa Chenge ndo maana tunamjadili. Zitto ni maarufu.

Kuhusu Owenye hukunielewa, nina maana Owenye ni family member wa viongozi au waasisi wa chadema..

Tatizo la Tanzania (nahisi umekaa nje muda mrefu saana) ni kuwa ukiwa na mawazo mbadala ndugu yangu basi wewe SIO MWENZETU na UMETUMWA. Na hilo ndo tatizo la akina Zitto na Viongozi na waasisi wa Chadema.

Ndo siasa za bongo uliza utaambiwa.
 
Basi wewe ndio hufahamu kitu..Toka Nyerere , Mwinyi, Mkapa, JK na viongoizi wote wa Kiafrika hakuna hata mmoja wao angeweza hata kushika madaraka ya County moja.
Mbali na kusema hivyo, huwezi kuongoza nchi yenye kuelewa mrengo ni kitu gani kwani huwezi hata kusema maneno yanayojichanganya. Tanznia unaweza sema wewe ni Mjamaa kama hao CCM na siasa za Ujamaa na Kujitegemea kisha wakafanya vinginevyo na wananchi bado wakakupa hongera kwa uongozi.
Mkuu wangu, usemayo wewe ndio ya kinadharia kwa sababu ikiwa JK ataongoza Marekani basi hizo demostration hazitakuwa za kupima tena itakuwa hadi mfanyakazi wa IKULU ana stage demo. Marekani unapoahidi kufanya jambo vyombo vyote vinajiandaa kutokana na sera zako.. huwezi kusema utaondoa tatizo la Umeme watu wakajenga umeme kisha ukategemea wao wanunue generators, maji wakachimbe visima na kadhalika..Ukweli ni kwamba Watanzania wanafanya mengi kwa mikono yao kuliko serikali yao hali Marekani kila kitu kina msingi, unachotakiwa wewe ni kujenga ukitakacho.. Fikira kitu chochote Marekani, hata iwe kufyatua fedha basi mwananchi anaweza na sii kufikiria Kikwete.
Watanzania wanafikiria Kikwete anaweza chapisha fedha kwa sababu hakuna njia za kupata fedha zaidi ya KUIBA na KUCHAPISHWA..ni kutokana na umaskini wetu ndio unajenga mawazo hayo..Mkuu wangu binadamu tunaelemikika kutokana na mazingira yaliyowazunguka..Ndio kama wazungu kwa utajiri wao wanvyofikiria unaweza kumfuga Simba kama pet kwani ukali wake unatokana na kukosa mapenzi, ukampenda Simba kwa mapenzi yote kuliko mwanao, hawezi kukushambulia.

Mkuu
Nakubaliana na wewe kabisa lakini inabidi tuangalie misingi yake pia.
umeongelea China ni kweli cina ilikuwa hoehai nasikia alitokea Dikteta mmoja mstaarabu akawachapa sana viboko akawashikisha adamu namna ya kufanya kazi jamaa nasikia imekuwa desturi yao yani akikaa chini bila kufanya kazi mikono inamuwasha.

Ndivyo vivyo hivyo wamerekani kila mmoja anajua namba yake na position yake ktk situation fulani, kwa hiyo wana panua uwanja vizuri na kutimiza majukumu yao kila mmoja, hivo mmoja akifanya kosa lazima alalmikiwe hiyo ni sawa na ndio maana ni rahisi kuliongoza taife lile.

Tatizo la tanzania wachezaji tumejirundika sehemu moja na uwanja hakuna sehemu ya kujinafasi, tukiambiwa jipangane uwanjani wabishi kama nini, sasa hata kama Mkandara mimi namba kumi wako wa kutegemewa na kapteni wako nimekuhahidi goli nitalipata vipi kwa wachezaji waliolundikana na hawataki ushauri wa kapteni wao?? Hii timu ni ngumu mno .

Watu tunaambiwa kilimo kwanza bila hata kujaribu shuti nduki moja kuelekea golini umeshabeza na kudharau unafikiri utafunga goli?

Tatizo ya timu yetu ni timu isiyokuwa na daraja lakini inajinadi ni timu profefesheno na kibaya zaidi ikipigwa goli inasingizia refa na haitaki kujirekebisha wala kukubali japo refa aliuma kidogo lakini wenye makosa ni sisi mda wote kucheza offside trick.
 
In addition Mwafrika;

Hilo tatizo la ukitupinga sio mwenzetu sio kwa Chadema tu, ni kwa viongozi wote wa kiafrika waliopo madarakani, haijalishi ni upinzani au ni serikali au ni chama hata makampuni ya umma ni hivyo tu.

"Miafrika ndivyo ilivyo" - Nyani ngabu aka Julius
 
Mwafrika,
Mkuu wangu kuwepo na watu wenye mrengo wa kulia na wengine kushoto ndani ya Chadema ni tatizo kubwa sana ndani ya chama kuliko matatizo ya Obama na Clinton
 
Mwafrika,
Mkuu wangu kuwepo na watu wenye mrengo wa kulia na wengine kushoto ndani ya Chadema ni tatizo kubwa sana ndani ya chama kuliko matatizo ya Obama na Clinton

Mkandara I think you can merge the two ideas and come with a mixed vision.

Sijui labda tujadili hili kwenye thread maalum. Ila kama nilivyoandika kwa Africa mkitofautiana msimamo au mtazamo au mkigombea cheo kimoja wewe ni adui na sio mwenzetu na wewe UMETUMWA. Hili ni pote Africa kwenye makampuni mpaka serikali mpaka vyama.

Tujadililini hili kwenye thread mpya.
 
Kuna dhana ya kijinga ambayo imetufanya tuongozwe kama kondoo tusijue tunaelekea wapi kwa kushindwa kutambua kwamba Tanzania bila CCM yawezekana. Hivi sasa pia dhana hii ya kijinga inaanza kupenyeza na kujengeka miongoni mwa wapenzi wa Zitto kuwa umaarufu wa Chadema umepatikana kwa sababu ya Zitto na bila Zitto Chadema itaporomoka. Jamani watanzania how stupid and low can we get, Zuberi Zitto Kabwe kijana ambaye yaonekana hata hajui anataka nini maishani kulingana na quotes za hapo juu ambazo ni yeye mwenyewe aliziandika kwa mkono wake ! Tuache kuumauma maneno, tuliite koleo kwa jina lake.

Zitto is on his way out and the sooner wapenzi wake realize this, the better for everybody kwani kama anakwenda aende kwa amani - Chadema will live on. Hii ndiyo tofauti kubwa nadhani kati ya CCM na Chadema - hakuna aliye juu ya sheria na hakuna atakayeonewa haya akienda nje ya msitari. Hivi Zitto anapolalamika kwa hatua zilizochukuliwa na sekretariat ya Chama, anataka nini. Humu ana wapenzi wa ajabu kweli kweli na ni wa aina mbili - wengine wanamtaka aondoke aende CCM na wengine wanamtaka aiue Chadema kwanza. Well moja la kuondoka lawezekana lakini la kuiua Chadema haliwezekani ng'o - mkae mkijua.
 
Hawa watu kwa nini waonekani kuwa ni wakorofi siku hizi na sio hapo kabla????hii ni kwa kuwa Mbowe na wenzie wanawashughulikia sana na wao wanakuwa wanapmbana na matokeo yake ndio haya kwamba watu wanapambana kama vile palka unapokuwa umemfunia kwenye chumba kimoja na kuanza kumchapa ujue ni wazi atakurarua vibaya sana kwa kuwa hana pa kukimbia,ALIANZA DK KABOROU AKAFATA WANGWE NA SASA NI ZITO NA WENGINEO...............GAME LINAENDELEA.
 
Back
Top Bottom