Kauli hizi za viongozi wetu vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli hizi za viongozi wetu vipi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mnyampaa, Jan 9, 2012.

 1. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kawaida kiongozi akitoa kauli au tamko jamii inafahamu kuwa anamaanisha. Hii ni kutokana na imani yetu kwamba kiongozi anapozungumza anakuwa well informed na kauli yake inatokana na taarifa sahihi. Kwa utafiti mdogo nilioufanya unaonyesha kuwa kwa Tanzania suala hili ni kinyume chake kwa mfano;
  1. Mwaka 2000 tuliambiwa na viongozi wetu kuwa baada ya miaka 5 kila Mtanzania atakuwa na maisha bora. Hivi sas ni mikaka 7 imepita na hali ni mbaya kuliko ilivyokuwa 2000.
  2. Mwaka 2006 tuliambiwa na Kiongozi wetu kuwa Mgao wa umeme utakuwa historia ifikapo oktoba 2006 lakini mwaka 2011 Tanzania imeshuhudia Mgao wa umeme wa kihistoria.
  3. Tangu Waziri Mkuu Pinda akatae kutumia 'shangingi' na serikali kutoa msimamo wa kuachana na kununua magari hayo, kumekuwa na ongezeko kubwa la magari hayo mapya yenye namba za serikali na DFP kuliko hapo ilivyokuwa hapo awali. Hii inamaanisha PM hakumaanisha alichokisema.
  4. Tangu Waziri Mkuu Pinda kutoa bei elekezi ya sukari kuwa sh. 1700 kumekuwa na ongezeko mara dufu la bei ya bidhaa hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.

  Haya ni machache tu ya mengi yanayosemwa na viongozi na kinachotokea ni kinyume chake.
   
 2. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tumethubutu, tumeweza na tunazidi kusonga mbele.
   
 3. p

  pilu JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Usiumize sana kichwa chako kwani kauli nyingine huwa ni za kutafuta umaarufu kisiasa tu, na kweli kwa hilo la umaarufu walifanikisha na wamepata madaraka, ilobaki ni mimi na wewe kufanya uchaguzi sahihi 2015.
   
 4. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  tatizo propaganda nyingi sana
   
 5. Bepari

  Bepari JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 813
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Yaani kutoka mwaka 2000 mpaka 2012 pamepita miaka 7?!!
  Ndiyo maana nilikimbia hisabati, kah!!
   
Loading...