Kauli hii ya Rais ndiyo matokeo ya chaguzi hizi za hovyo

gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,485
18,045
"Mkurugenzi nimekuteua mimi gari nimekupa mimi, Mshahara nakulipa mimi, Nitakushangaa kumtangaza Mpinzani mshindi."- John Joseph Pombe Magufuli

Hii ndio kauli Rais aliwahi kutoa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali nchini kama agizo kwao wakati akiwaapisha ambayo ni kinyume kabisa na hadhi ya cheo chake kama mkuu wa nchi na kiongozi wa taifa, kauli ambayo ni ya kichochezi kwa taifa na inaweza kuleta madhara makubwa sana kwa jamii siku za usoni, kauli ile haikupaswa kutolewa na Rais wa nchi

Leo hii tunaona chaguzi za hovyo kabisa kuwahi kufanyika toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini 1992 baada ya uhuru, chaguzi ambazo tunaona ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na utawala bora ukifanyika waziwazi kabisa bila hofu kama kuna sheria zinazosimamia mchakato mzima wa uendeshaji wa zoezi la upigaji wa kura, Rais wa nchi yuko kimya kana kwamba yanayotenda yanatendeka nje ya mipaka ya Tanzania ambako hana mamlaka nako.

Kauli ile ya rais kimsingi inadharau haki ya wananchi kuamua kuchagua kiongozi wamuonaye wao anawafaa kuwatumikia, kauli ile ni tusi dhidi ya Watanzania wanaotumia haki yao kikatiba kuchagua kiongozi wao

Tafsiri ya kauli ile wananchi hawana haki ya kuchagua mwakilishi wao isipokuwa yeye na hao wakurugenzi ndio watawapa ushindi watu wawatakao wao na si wawatakao wananchi

Uzalendo anaosimama kwenye majukwaa ya kisiasa na kuaminisha wananchi kuwa anao ndio huu wa kutumikia maslahi ya chama zaidi kuliko maslahi ya taifa zima!!
 
"Tuliponunua Bombardier mliziita Pangaboi,msifikiri wananchi hawakuwasikia,waliwasikia wakanyamaza wakasema siku yenu ipo"
:
"Tumenunua Boeing mmepinga baadae mkazipanda,wananchi wakasema haina noma mtaingia 18 zetu"
:
"Tumesema tunahitaji kutumia masaa 7 Dar-Dodoma tukasema kwa kufanya hivo tuje na mradi wa reli ya kisasa mmepinga,wananchi wamewasikia na wamewashuhudia wamesema isiwe tabu mtajaa tu kwene kilengeo"
:
"Tukasema tuondoe watumishi hewa wa serekali kuondoa upotevu wa fedha ya umma nalo mkapinga,wananchi wakawanyamazia kama hawawaoni"
:
"Tumejenga fly over tazara kuwaondolea Wananchi Kero ya Folen,mmedhihaki sio fly over ile ni daraja,wananchi wakawachukulia poa"
:
"Tumetia saini uundaji wa meli kubwa kuwahi kutokea Africa mashariki na kati,tumeunda meli mpya Ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa za mizigo na abiria,tumeunda vivuko vipya kigamboni na busisi Mwanza,tumetia sign na serekali ya Korea kusini ujenzi wa daraja la coco-beach,fly over ya Ubungo jiwe la msingi limekwisha kuwekwa,tuna mradi wa umeme wa Stigler"
:
"Mambo haya yote Hakuna hata moja mlilounga mkono afu Mnataka Wananchi wawachague kwa kupiga kelele za kupinga tu afu wasiwachague watu ambao wamepitisha mambo haya na kusimamia utekelezaji wake,mnawafanya Wananchi mboya sio....?? "
:
"Kwa huu mwendo wa kupinga kila kitu 2020 mgombea wenu wa Urais hatafikisha hata kura laki moja,endeleeni
 
Etwege,
Hiyo dreamliner mlinunua mfanye safari za ndani?

Haya ni matokeo ya kufanya mambo bila kujipanga.

Na kwa jinsi tulivyojaa kesi na madeni yanayotokana na kuvunja mikata, subirini kuona hayo mandege yakikamatwa huko katika nchi za watu na mimi nasema wayakamate tu tulipe kuliko kulimbikiza mariba.
 
"Tuliponunua Bombardier mliziita Pangaboi,msifikiri wananchi hawakuwasikia,waliwasikia wakanyamaza wakasema siku yenu ipo"
:
"Tumenunua Boeing mmepinga baadae mkazipanda,wananchi wakasema haina noma mtaingia 18 zetu"

Tumenunua sio neno sahihi ,Ndege za bilioni 70 hizo ni asilimia 0.15 ya bajeti, hio flyover ni sawa na asilimia 1 ya kodi za wananchi tunazochochangia kwenye bajeti nzima, Tanzania ya walipa kodi tunahitaji zaidi ya vitu hivyo ambavyo hata Hashim Rungwe akishika madaraka ni jukumu lake kuvifanya na sio kujisifia kwa hili neno Tumenunua

Hali ya kifedha nchini ni mbaya toka nchi ipate uhuru hadi kufikia hatua bajeti ya bunge live inafinywa.

Kauli mbovu zinazokiuka katiba zimeshamiri kwa kasi tangu tupate uhuru mfano :"Mkurugenzi nimekuteua mimi gari nimekupa mimi, Mshahara nakulipa mimi, Nitakushangaa kumtangaza Mpinzani mshindi "

Kazi Ipo
 
Utasubiri sana, kwa sababu CCM itatawala milele!
P
Hakuna kitu kama hicho.Kwa sasa kinabaki kikundi kidogo tu cha watu ambao ni wanufuika wa huu utawala wa sasa ila wengi wako against.

Wanazidi kupoteza uungwaji mkono na kadri wengi wanavyoikataa ndio hatari ya wao kutoka madarakani inavyoongezeka.

Hata Mugabe kwa ule wa madaraka alifanya maamuzi ya hovyo yaliyofanya hata majeshi kutomtii tena.
 
Back
Top Bottom