Kauli hii ya Rais Magufuli kuchaguliwa na masikini

mkubhi

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
2,211
3,317
"...Serikali ninayoiongoza, ilichaguliwa na masikini... Kama matajiri walifikiri nitakuwa upande wao basi wamenoa. Mimi nilichaguliwa na masikini na nitawatumikia masikini na si matajiri."

Hii kauli Magufuli amesikika Mara nyingi akiisema!!!! Tujiulize hii kauli anayotamba nayo PGM yuko Sawa!?

Na haina madhara kwa uchumi wa taifa!?
 
Kauli ya namna hii huwa inakuwa na maana wakati wa kampeni za uchaguzi kwa lengo la kuzoa kura za kundi kubwa la jamii pana ambayo ipo kwenye lindi la umaskini.

Baada ya kushinda uchaguzi, Rais anakuwa wa jamii nzima bila kujali maskini au tajiri. Kwa maoni yangu, Rais hawezi kutimiza ahadi zake nyingi ikiwemo ile ya kujenga uchumi wa viwanda bila kuwa na mahusiano mazuri na matajiri ambao kiukweli hao ndiyo walio na mtaji.

Rais mmoja wa Marekani aliwahi kusema kwamba HUWEZI KUWAFANYA MASKINI KUWA MATAJIRI KWA KUWAFANYA MATAJIRI KUWA MASKINI.

Jambo la msingi ambalo Rais anapaswa kusisitiza na kulisimamia ni matajiri kufanya biashara halali na kulipa kodi ipasavyo ili kodi hiyo isaidie maskini.
 
kama baba yako nae ni tajiri, mwambie zama zake zilisha pita. Tz ni nchi ya wakulima 80% na 18% ni wafanyakazi ni kama 2% ndo wafanyabiashara. Cha ajabu na kinacho sikitisha na kushangaza, kikundi cha wachache 2% ndo kinataka kitawale walio wengi kwa hira ya pesa. Hiki ndo Rais anapinga
hizo takwimu umezipata wapi kijana, wabongo sisi ujuaji mwingi
 
Hao matajiri ndo walipaji kodi inayoendesha serikali, na hao masikini ujira wao hutegemea matajiri kwa namna moja hau nyingine, kuwadhihaki matajiri tumsamehe tu hajui alitendalo.
Make matajiri akikutana nao anaomba walipe kodi.
masikini akikutana nao kwa kuwa hawana cha kumpa anawaabia atawapa msaada ambao kwa juhudi ya matajiri ndipo anapopatia hiyo misaada, tumsamehe tu ndivyo alivyo.
 
Ni kutafuta huruma na support na ni kauli iliyokosa ithibati kwakuwa kiuhalisia hakuchaguliwa na hao maskini bali wizi wa kura ndio uliomuweka madarakani
BTW maskini ndio wapiga kura lakini uwezeshaji hufanywa na hao matajiri
Naona mapovu yanakutoka mkuu
 
kwa kauli mbovu kama hizo hatuwezi kufika.
rais inabidi ajichunguze upya hizo sio kauli za kuongea kwa watu.
 
Ni kutafuta huruma na support na ni kauli iliyokosa ithibati kwakuwa kiuhalisia hakuchaguliwa na hao maskini bali wizi wa kura ndio uliomuweka madarakani
BTW maskini ndio wapiga kura lakini uwezeshaji hufanywa na hao matajiri
Ni kukosa subira katika kuchagua maneno ya kuzungumza. Ni kuwa na haraka ya kuzungumza isiyohitajika. Lakini ni hatari zaidi kucheza na wafanyabiashara. Wanaotambua nafasi yao katika nchi "wanawa handle with care", wala hakuna sababu ya kutamka kuwa hukuchaguliwa na matajiri wakati ukweli ni kwamba kuna matajiri wakubwa nyuma ya ushindi wa chama chako
 
Drama will never end na huyu jamaa, fine kweli sikukuchagua! So what ! Unataka ututenge kisa hatukukuchagua! Yaani sisi siyo wa tz au? Kuwa upande wako wala si lazima, fanya kazi kama watakupenda watakupenda tuu!!! Eish kwani lazima wote tukuchague! Tuna haki ya maamuzi
 
Back
Top Bottom