Katu sitakula makombo hata yawe ya Biriani

Katu sitakula makombo hata yawe ya Biriani

Anold

ImageUploadedByJamiiForums1438249852.243188.jpg
 
Last edited by a moderator:
Nahisi shida ndizo zilizomfanya arudi. Msaidie kutafuta kazi apate halafu ujue msimamo wake. Lakini tena Usimgegede bila Kupima Aisee. Vyuoni huwa kuna cheni matata sana
 
Naimani ulishamsamehe kitambo tu na ni vyema ikawa hvyo ila ishu ya kurudisha mahusiano achana nalo,endelea na mipango yako naye aendelee na mipango yake
 
Anold

Great,....
Wanaume kamili tuko wachache sana siku hizi-wewe ni miongoni mwetu,
Tena mpige beat hata ghetto asiguse i,e kama salamu ni njiani au hata kama vip salamu yako asipate mpaka akuanze yeye na jibu ni-poa...!
 
Last edited by a moderator:
Anataka msaada uyo. Makosa katambua baada ya maisha kuwa magumu? Kama ulimpenda sana msaidie kumtafutia ajira ila muepuke kama kimbunga
 
Kwenye kesi hii usikilize sana moyo wako maana ndio wenye siri ya nn kilicho ndani ya nafsi. Kama ukimuacha mwambie kiungwana na uachane nae na wala usionyeshe umeumia kwa kumgharamia maana ataona kama nafasi yake bado ipo hivyo ukimuacha muache kwa kumweleza kuwa nafasi yake haipo tena moyoni mwako na umeamua kuendelea na maisha yako bila yeye.

Ila kama bado unampenda na unataka umrudie usikurupuke hata kidogo katika ili maana inatakiwa uwe mwangalifu sana kujua ana nia gani moyoni mwake (kumbuka moyo wa mtu ni kichaka kinaficha mengi) ukimsamehe mwambie kuwa umemsamehe ila mweke kwenye uangalizi mpk apate kazi uone trend yake baada ya kupata pesa maana anaweza kuwa ukata ndio unamrudisha na si mapenzi yake kwako.

Kingine usijiapize kuwa huwezi kula matapishi maana maisha haya yana mitihaninmingi sana usiishi kwa viapo huwezi kujua Mungu amekupangia nini. Kuna makosa uliyafanya kwa kumsomesha mtu ambaye haukuwa na commitment nae ilo ni kosa hata mke ukimsomesha chuoni atashawishiwa tu na wengi wanasaliti wenzi wao lakini maisha yanaendelea. Ukiweka sana moyoni haya mambo utakuja kuoa kwani hakuna mwanandoa aliye msafi ila ni uvumilivu ndio unaofanya ndoa zisonge mbele.

Pole sana kwa maumivu najua unaumia na kutueleza kwa kuwa bado yuko moyoni mwako ila hiyo ni mitihani ya dunia. Duniani hakuna msafi wote humu tunapitia mitihani migumu tena huwezi hata kuthubutu kuiandika humu lakini maisha yanaendelea tu.

Kwa maoni yangu binafsi kama mtu ametenda kosa na kuomba msamaha ( wa kweli) basi me ningemsamehe kama moyo wangu unamhitaji. Maana kuna msemo zimwi likujualo alikuli likakwisha. Pia kuna msemo unasema to err is human, to forgive is divine. Na nina imani kosa ni mtaji mkubwa sana kwenye maisha maana katika kosa kuna funzo kubwa sana unapata

Asante sana
 
tulishasema hapa kuwa mwanamke hasomeshwi...lakini pia mkuu naamini hili siyo swala lakuomba ushauri hata kidogo,maana kwa hekima zote hata zakuumba dunia ni kuwa HAKUNA kurudi nyuma,kugeuka nyuma nikuwa jiwe la chumvi...kaliwa watsap na kama haitoshi wazazi wake nao wamemsaidia wakuumize,sioni sababu ya wewe kurudi zaidi unaharakisha kifo chako kwa mawazo...huyo tabia zake zipo ndani ya damu yake maana hata wazazi wake ni mashahidi

Huyo hajagundua kosa ila amegundua kuwa alipoteza almasi kwa mng'ao wa chupa,yeye na wazazi wake...kajifunza basi asubiri mwanaume mwingine aje ila siyo wewe....
 
soory beo acha kuzingua unataka ushauri wa aina gani hapa ENDELEA NA MAISHA YAKO HATARI ITAKLUANGAMIZA..................usijishauri au huruma ya mshuma.....songa mbele bwana...mfa maj haishi kutapatapa.....mwisho utakiuja jiua bure,,...huyo si MKE...ila maamauz yako tusikushawishi sisi
 
Binti hana msimamo, wazazi wake hawana msimamo, hpo unaweza kurudiana nae na baadae yakatokea yale yale. Yale mafuta aloambiwa apake jamaa yalinunuliwa kwa hela yako...
 
ushasikia "geuka" "weka mafuta kwanza" hakuna usalama hapo mkuu... kimbia wala usigeuke nyuma
 
Kwa kauli hiyo ya weka mafuta kwanza, walishachana malinda.

Piga chini.
 
Hii dunia ina wanawake kama billion 4 hivi, huwa nashangaa inakuwaje mwanamke mmoja tu anamsumbua mtu akili. Piga chini tu!
 
Back
Top Bottom