Katto: Siwajui vigogo wauza Unga

Katto: Siwajui vigogo wauza Unga

calory

Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
31
Reaction score
6
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akidaiwa kukalia orodha ya mtandao wa vigogo wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya, Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege nchini, Deusdedit Katto, amewataka wanaowafahamu watuhumiwa hao watoe taarifa.

Katika mazungumzo yake na kituo cha televisheni cha Channel Ten juzi, Katto alisema hawafahamu vigogo hao wanaotuhumiwa na kwamba yeyote mwenye ushahidi akatoe taarifa.

"Wakati mwingine tunasema tu, kama tuna ushahidi kuhusu hilo utolewe. Mimi nalisikia neno hilo la vigogo hata kabla sijaja hapa," alisema Katto alipotakiwa kufafanua kuhusu uuzaji wa dawa hizo kuhusisha mtandao mkubwa.

Alisema hilo ni tatizo kubwa duniani na kwamba hakuna serikali yoyote ambayo inacheza nalo.

Alisema wanapambana na suala hilo kwa namna mbalimbali na kudai kuwa kuna baadhi ya nchi ndogo wafanyabiashara hiyo wamekuwa wakishindana na serikali zao.

Kuhusu uteketezaji wa dawa hizo kufanyika kwa siri, Katto alisema si kweli kwani taratibu zinafuatwa kwa kuwashirikisha watu wengi.

"Kuna vyombo vinatajwa lazima viwepo wakati wa kuteketeza, mfano jaji aliyesikiliza kesi, mawakili wa serikali na wale wa utetezi, Mkemia Mkuu wa Serikali ili athibitishe kama zilizoteketezwa ni dawa za kulevya," alisema.
 
.....anataka nani awataje, akamfuate JK ampe majina aliyokabidhiwa.
 
Kila mtu hajui.
Hata yeye hajui.
Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege nchini, Deusdedit Katto hajui kwanini yupo JKIA.
Hajui cheo chake kazi yake nini.
Hajui kwanini watu wanamuuliza majina ya vigogo ambao hawajui.
Hajui kwanini watu wanapitisha madawa ya kulevya kupitia JKIA,hajui, hajui,hajui....

Na mimi sijui kwanini watu wanapoteza muda kumuuliza mtu ambaye hajui wajibu wake.Sijui.
 
Niwataje nisiwataje............????
 
...kama bwana kato hawajui basi yeye na ofisi yake hawajui na hawana wanalofanya. Ukiachilia mbali uwezo waliopewa kupeleleza,zipo kesi nyingi za madawa ya kulevya ambapo kazi yao ni kufuatilia tu chain mpaka mtu wa mwisho. Naamini angepata angalau wahusika si chini ya 10. Wengine wametajwa live ! Sasa sishangai polisi kusimamisha mishipa ya shingo na taarifa za inteligensia zinaishia kwenye maandamano na mikutano tu. Mambo ya msingi mtu bila aibu anasema hajui na orodha iliyotajwa na wananchi wanayn. Ooops.. Tanganyika...!
 
Unataka awataje halafu kinuke???
hivi huyo mwandishi wa habari hakumuliza swali la kwa nini haendi kwa rais kuchukua list ya wauza madawa ya kulevya akizingatia kuwa rais aliwahi kusema anayo majina!
 
Hajui kweli,hata baba Riz 1 alinukuliwa vibaya,HAJUI pia,akili ndogo hizo,hivi na wale waliowakagua akina "masogange"mpaka kusema mizigo ipo clear ipakiwe kwenye ndege nao HAWAJUI!?.Na mitambo yote,camera za JNIA,usalama wa taifa JNIA,polisi wote HAWAJUI,NA kweli hawajui,hata me SIJUI PIA.
 
hivi huyo mwandishi wa habari hakumuliza swali la kwa nini haendi kwa rais kuchukua list ya wauza madawa ya kulevya akizingatia kuwa rais aliwahi kusema anayo majina!

Hakuna mwandishi wa Tz anaweza uliza swali hilo,labda kama kucha na meno yake ameyachoka,ukizingatia na BAHASHA YA KAKi ipo mezani!
 
Hivi ninyi wadanganyika mpaka leo hamjui kuwa fedha za CCM zinatokana na mapato ya madawa za kulevya? nin kimejificha? USHINDI NI LAZIMA maana yake ni nini? fedha za kusafirisha watu kwa fusso, bajaji, Hice, coster, fedha za sare plus pockt money mnafikiri zinatoka wapi? marehemu gulamali na akina dewji walikuwa wanaifadhili simba na yangu bure bure tu? so do Manji!...

Kihoro kikubwa ni pale ambapo mission za magharibi kujaribu kuharibu nchi za Asia thru mihadarati, wameifanya Dar kama njia ya kupitishia mizigo yao! Serikali inalifahamu hili na limepewa majukumu ya kuwalinda wasafirishaji! Ieleweke kuwa target hapa siyo Watanzania bali ni mataifa ya Asia yanayotishia ustawi wa kimagharibi... mpaka leo hamshangai hii mikataba ya kubadilishana wafungwa inavyofungwa kwa wingi... fumbueni macho ... wasimamizi ndiyo wasafirishaji wakubwa! ila katika misafara ya mamba kenge nao wamo!!..
 
..... Ieleweke kuwa target hapa siyo Watanzania bali ni mataifa ya Asia yanayotishia ustawi wa kimagharibi... mpaka leo hamshangai hii mikataba ya kubadilishana wafungwa inavyofungwa kwa wingi... fumbueni macho ... wasimamizi ndiyo wasafirishaji wakubwa! ila katika misafara ya mamba kenge nao wamo!!..

Mkuu utasemaje target siyo watanzania wakati watanzania ndiyo wamerundikana huko magerezani asia kwa madawa....

Katika kuthibitisha kuwa target ni watanzania kwani nchi za ulaya hawana vijana kama vijana wetu wa hapa ambao wanaweza kuwabebesha hayo madawa?
 
Atakubali anawajua tarehe October 2015 subiri maana hapo atakuwa anajua ajira yake ndio imeisha ....
 
Mkuu utasemaje target siyo watanzania wakati watanzania ndiyo wamerundikana huko magerezani asia kwa madawa....

Katika kuthibitisha kuwa target ni watanzania kwani nchi za ulaya hawana vijana kama vijana wetu wa hapa ambao wanaweza kuwabebesha hayo madawa?
Thanks kwa angalizo murua mkuu, walengwa wa hayo madawa ni vijana wa mataifa ya Asia hususan China...System yetu na Vijana wetu wanatumika katika usafirishaji...nchi kuwekwa mfukoni kuna madhara mengi sana, na hilo nalo ni mojawapo ya kutawaliwa kwa remote control ...Nyerere aliasa alionya lakini mwisho wake walimua...Ole wake Tanzania
 
Watu wa kutoa jibu ni wakina HAMY-D, kwani hawa wanajua mengi kuhusu haya Mambo!
 
Last edited by a moderator:
Watasema tu, kwanini madawa yanapita hapo kwetu, akamatwe huyo mlinzi mkuu hapo, afikishwe mahakamani kwa uzembe kazini harafu utaona shughuli yake thereafter
 
Simple. Muulize mkuu wa kaya. Alisema ana list:smile-big:
 
Back
Top Bottom