Katoliki: Kuvuja kwa nyaraka za siri za Papa

mwitaz

JF-Expert Member
Feb 19, 2012
315
93
Afisa mmoja wa ngazi ya
juu katika makao makuu
ya kanisa Katoliki mjini
Vatican, amesema kuvuja
kwa nyaraka za siri za
kiongozi wa kanisa hilo duniani ni kitendo cha
kikatili dhidi ya Papa
Benedict. Afisa huyo ambaye ni
naibu waziri wa mambo ya
nje wa Vatican Angelo
Becciu, amesema nyaraka
hizo ni pamoja na fikra
binafsi, na pia shutuma kali kutoka kwa watu
waliomwandikia Papa
barua za siri kutokana na
nafasi yake ya kipekee. Nyaraka hizo zinashutumu
vitendo vya rushwa na
kushindania madaraka
katika ngazi ya juu ya
Kanisa Katoliki. Mwandishi wa BBC mjini
Vatican amesema hii ni
kashfa kubwa kuliko zote
dhidi ya Papa Benedict
tangu apate wadhifa wake
huo miaka saba iliyopita, na ni tukio lililochafua
Kanisa Katoliki nyakati
hizi. Mhudumu mkuu wa Papa,
Paolo Gabriele,
amekamatwa na tume ya
Vatican inachunguza watu
wengine ambao
wamehusika katika kashfa hiyo.
 
Back
Top Bottom