Katika mzingira ya ushabiki vya vyama je ni haki spika kuwa na chama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katika mzingira ya ushabiki vya vyama je ni haki spika kuwa na chama?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mghaka, Jul 29, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ukianzia kwenye mizengwe ya kuteua spika mpaka namna bunge linavyoongozwa katika Tanzania unatambua kuwa kama ni timu zinacheza mpira wa miguu basi timu ya ccm ina golikipa wawili. Licha ya kuwa timu hii inawachezaji wengi lakini pia kwa njia isiyo stahili imemchukua referee ili kudakia katika goli lake ili kusaidiana na golikipa wao. Mimi sishangai kwani misuguano ya ndani kwa ndani ya chama wakati wa kumpata spika ilikuwa inalenga kumpata golikipa bora wa kusaidia kudaka kwenye lango lao mipira inayompita mlinda mlango wao.

  Bahati mbaya kwao, golikipa huyu alikuwa anatakiwa kudaka mipira ya kichwa ambayo inampita golikipa wao, lakini kwa sababu ya upendo wa timu yake na kwa sababu ya ukali wa fowadi ya timu pinzani mipira yote inayopigwa golini kwao ni kwa miguu magoli yanaingia kila wakati na sasa uzalendo umemshinda amejitosa kuokoa mipira yote na filimbi aliyopewa ndiyo silaha anayotumia kuzuia magori. Nasema ni bahati mbaya kwao kwa sababu mechi kamishina ameona na ametangaza mechi hiyo ni batili.

  Viongozi wa Bunge letu spika na wenyeviti wake wamechemsha, filimbi zao hazipunguzi spidi ya fowadi ya timu pinzani bali zinaongeza, kibaya zaidi ni pale ambapo hata maana ya filimbi yenyewe inaendelea kupuuzwa. Nahisi mwishoe wapulizaji wataacha wenyewe kwa sababu umma unawadharau. Huwezi kuacha timu pinzani icheze kwa faulo nyingi hata kukamata mipira wewe upete timu pinzani isilalamike eti kwa sababu wakifanya hivyo wataonekanana wanaenda kinyume na kanuni. Unatengeza mizingira ya unyang'anyi wa haki eti kwa sababu sheria inawakataza. hii si kweli na si haki janja yake paka panya kesha jua hapati mtu hapa mnatupeleka katika nchi ya 'hapatakalika' na ile ya 'hapatatawalika'. Chonde sana lindeni haki nchi yenu, watu wenu na mioyo yenu. Tunajua wengi wenu mlishadunduliza kwa kuibia nchi hii kwa hivyo nchi ya 'hapatakalika' itakuwa yetu na nyinyi mtakuwa hampo. chonde chonde wabunge wa ccm na viongozi wa bunge muogopeni Mungu.


  A L U T A C O N T I N U A ! V I V A U M K H O N T O W E S I N Z WE
   
Loading...