Katika Mapenzi...

Tetra

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
1,526
Reaction score
771
::
Tuwapendao sana
Ndio watuumizao sana.
::
Tuwapao siri zetu kwa kudhani ndio msaada wetu
Ndio watumiao siri zetu kuja dhidh ya upendo wetu.
::
Tuwaaminio sana ndio watuangushao sana nyakati tusizotazamia.
::
Tuamuapo kuwa serious na maisha yetu
Ndio nyakati majaribu ya mapenzi hutuandama.
::
Tupewapo hadhari sana kujiepusha na mapenzi,
Ndio nyakati ambapo tuanzapo kupenda.
::
Tupatapo fahamu baada ya kutendwa na kuamua kusimama imara
Ndio wakati huwa tumechelewa sana.
::
KATIKA MAPENZI....mwingine aendelee
=
 
tatizo la mapenzi sio shule huseme utafeli uachane nayo
ubaya wa mapenzi ni kutokutazama nyakati au wakati

hitaji la mapenzi ni uaminifu na uadilifu ambao ni udhaifu wa binadamu
mapenzi hayadanganyi lakini hulka ya binadamu kudanganya

tazama mapenzi yalivyokutesa, yalivyomtesa na yanavyonitesa
sio masikini fukara tu hata tajiri bill gates mfano mapenzi yanawakwida

kamwe husiseme hutakaa hupende maana ni kupambana na kiza kizito
Swali nauliza nani aliumba mapenzi? Hivi ni Mungu au shetani?

Kama jibu ni Mungu nina swali, kwanini aliweka usaliti ndani yake?
Kama jibu ni shetani hapo sina swali, maana hila za shetani zafanana na matendo ya mapenzi

wadadavuzi nidadavulieni, undani wa mapenzi ni ufahamu
Tetra husiondoke mpaka mkagasiko utakaponiachia
 

::
Asante sana Mokoyo
Nimekupata vilivyo
Aliyeumba mapenzi
Simjui nasema wazi
Najua mie Tetra
Mapenzi tuliyakuta
Kama Miti na ndege
Yapo yenye miiba tele
Yapo yenye maua
Japo hayakawii nyauka
LITUPASALO TUPENDE TU,TUSITARAJIE MAKUBWA.
=
 
Last edited by a moderator:
Ni heri kutoa kuliko kupokea. when you are in love, jifunze kupenda, without expecting anything in return, you will much enjoy the relationship, than expecting so much from it!
 
na mara nyingi inakua tofauti
unampenda mtu kupita maelezo
thn yeye anakuumiza mbaya
mi siku hizi sipendi kwa kweli natamani tu!

 

Ndiyo yaliyonikuta!
 
Ndiyo yaliyonikuta!
Pona my dear....
usimruhusu mtu ambaye mmekutana naye akakufanya uwe depressed milele.....
yamepita, unajifunza kisha unasonga mbele.....
Inauma sana, nimeshakuwa kwenye hiyo situation once..... nimeshapona na nasonga mbele, hata sikumbuki nini kilitokea....
Na.......... sitaacha kupenda sana....... ndo kitu ninachoenjoy nikiwa na mtu.... KUMPENDA SANA
 

I will survive my dear, najua muda ni dawa!
 
Ndiyo yaliyonikuta!

Christ, my God has prepared a better man for you than what has excited you before. He will cherish you with all of his heart then you will know that My God, Christ Jesus had done it just for you! The only price you have to pay be4 you receive the said divinely blessing is trusting HIM and patiently wait for your appointed moment of reckoning and that moment is closer than you can possibly imagine...................Are u that strong and be patient? Permitting God of patience and comfort do His divinely work on you? That is the question you have to honestly answer in your soul not to me for I am a confessed sinner!
 
I will survive my dear, najua muda ni dawa!

The good news is the bad boy is gone forever and it is God who has chased him away before he can cause even more damage to that beautiful body of yours. Remember your body is worth more than food and clothing. You can always buy them but where can you replace that beauty of yours? No doctor can do it because he did not create you in the first place.
 
Kaunga
Pole sana,,
Tuna safari ndefu ya kujifunza ktk ulimwengu wa mapenzi.
Darasa hili halina mwisho ni jipya wakati wote.
Tunatakiwa kusimama imara na kujithamini kwanza wenyewe.
=

Rejoice with those who rejoice and sorrow with those who sorrow. It is a calling of God to do just that.
 
na mara nyingi inakua tofauti
unampenda mtu kupita maelezo
thn yeye anakuumiza mbaya
mi siku hizi sipendi kwa kweli natamani tu!


::
Passion Lady
Jihadhari maana kutamani kukizidi inakuwa kupenda
::
Kupenda kusingekuwa jambo linalokupa bila kujua.
Lenye nguvu kama usingizi wengi wetu mapenzi ingekuwa mtihani ambao kila mmoja anafaulu.
=
 
Last edited by a moderator:
::
Kaunga
Pole sana,,
Tuna safari ndefu ya kujifunza ktk ulimwengu wa mapenzi.
Darasa hili halina mwisho ni jipya wakati wote.
Tunatakiwa kusimama imara na kujithamini kwanza wenyewe.
=

Ni kweli, wanasemaje ...kisichoweza kuua kina kufanya uwe strong...


Thanks Rutashubanyuma kwa maneno ya faraja na ya kunivimbisha kichwa at the same time. Ubarikiwe.
 
Last edited by a moderator:
Nimetoka kusema kwenye thread nyingine kuwa,unapofanya jambo usitafute sababu kutoka nje yako,jikamilishe mwenyewe
'
Unapoamua kumwambia jambo ambalo wewe umeliona la husuni na kudhani ukimwambia atakuhurumia halafu ikatokea kinyume lazima utaumia
'
Kama umeamua kumwambia jambo hilo mwambie kwa kuwa umeamu na hauhitaji huruma yake
'
Tunapotarajiwa tukamilishwe na wengine hatujui nao wanatarajia sisi tuwakamilishe,tutaishia kudaiana vitu ambavyo hatuna mwishoe tunaishia kulaumiana!
 

Dadadeki!!!!!!!!!!!
 
Thanks Rutashubanyuma kwa maneno ya faraja na ya kunivimbisha kichwa at the same time. Ubarikiwe.

AMEN! However, the things I prophesy in your life will happen and then you will know that it is the LORD who did it not you or him, for that matter!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…