Katika kusoma kwangu sijawahi ongoza somo la Hisabati -Mathematics

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,563
3,708
Wakuu Salaam,

Katika kupata kwangu elimu ya dunia level mbalimbali za kusoma sijawai kuongoza katika somo la hisabu ata nikijitaidi vipi sijawai kuongoza kuwa kinara wa marks katika somo hili, lakini masomo mengine yalikuwa ni rahisi kwangu kuongoza kawaida.

Nilivyoona silielewi sana nikaamua kuachana nalo linaniumiza kichwa.

Nilipoenda chuo kusomea taaluma flani nikazikuta hesabu kama zote nikajuta kuliacha O-level yani nikajikuta narudia nyuma nilikokimbia lakini awamu hii sikufanya utani tena nilijua nikishindwa tena naangukia pua.

Wataalamu mahesabu hongereni sana ili somo yahitaji kipaji.
 
Moja ya talent Student basi ni mwanafunzi anae ijua Mathematics.(kujua Pysics sana au history au geography hakumpi mwanafunzi sifa ya talent student) hivyo ni namna gani Hicho nikipaji maalumu.

Japo wapo hukazana kuijua kwa kuisoma(kufanya) Ila ikiwa ni nje ya kipawa maalumu, hiyo itakuwa ngumu tu na kumsumbua wakati mwingine.
 
Advanced Physics ngumu kuliko Maths, O level Physics ngumu kuliko Maths. Kwa vipimo vya kibongo kwenye NECTA aliyefaulu P ni mzuri kuliko aliyefaulu M.
 
Nakubali kuelewa maths kibongobongo ni kapaji la sivyo nguvu kubwa inaitajika
 
Mimi shule ya msingi hili somo nilikuwa nalimudu sana, nimeshapiga 50/50 mara kadhaa. Kwenye pepa ya Taifa STD VIII nilipiga 47/50. Nilipokwenda sekondari form one hazikunisumbua maana topics nyingi zilikuwa ni marudio ya shule ya msingi.

Shida ilianzia form two kuanzia Quaratic equation,to make the subject, logarithm nikawa naona mapichapicha tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Advanced Physics ngumu kuliko Maths, O level Physics ngumu kuliko Maths. Kwa vipimo vya kibongo kwenye NECTA aliyefaulu P ni mzuri kuliko aliyefaulu M.

Hicho kipimo kiko wapi na nani kakiweka ??.

Ni lazima ujue kwamba hakuna physics bila Maths, Maths ni nyenzo ya kukusaidia kukokotoa Maswala ya Physics, ndiyo maana wapo "wanaojua Maths" lakini hawajui Physics lakini ni vigumu kukuta mtu anayejua Physics na asijue Maths.---- Maths ni baba Physics ni mtoto au Maths ni Jembe na Physics ni Shamba huwezi kulima shamba bila Jembe.

Marehemu Mwalimu wetu mmoja wa A level (Miongoni mwa mabingwa wa physics katika Tz) alipata kusema; "physics inahitaji ujue (1) Maths, (2) Logic, (3) English", hili la English alikuwa anamaanisha kwamba kwakuwa elimu ya Physics tuliyokuwa tunajifunza ilikuwa katika English na hivyo ilikuwa ni muhimu kuijua.
 
Mimi shule ya msingi hili somo nilikuwa nalimudu sana, nimeshapiga 50/50 mara kadhaa. Kwenye pepa ya Taifa STD VIII nilipiga 47/50. Nilipokwenda sekondari form one hazikunisumbua maana topics nyingi zilikuwa ni marudio ya shule ya msingi.
Shida ilianzia form two kuanzia Quaratic equation,to make the subject, logarithm nikawa naona mapichapicha tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
😂😂😂😂😂 form two hapo ndio wengi huwa ndio wanaacha hesabu form one inakuwa flashback,sasa umkute mwalimu mnoko anaependa kutoa Quiz yani duh.....
 
Kuna zingine hata kwenye maisha halisia hazitumiki
Ni nyingi sana hazitumiki nakumbuka Logalism wataalam wa 4 figure mpo!
Hakuna hesabu isiyotumika kwenye maisha wazee, sema nyie ktk maisha yenu ndo hamzitumii direct lkn mnazitumia indirectly, mfano hzo hesabu mnazosema hazitumiki watu wanatumia kujenga madaraja, kurusha ndege, kutengeneza mabomu n.k
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom