Nimetengeneza App Kwa ajili ya kusaidia watoto katika somo la hisabati

southern boy

Member
Jan 12, 2016
59
121
Habari humu!! Hi post pia nitaiweka na kule kwenye jukwaa la elimu sababu pia inahusu masula ya elimu.


Ningependa kuanza moja kwa moja kwamba nimetengeneza app hii kwa ajil ya kumsaidia mzazi/mlezi/mwalimu/kaka/dada kumpa mtoto mazoezi kwenye somo la hisabati mda ambao upo busy na shughuli nyingine.
Kipindi fulani cha nyuma pia mpaka hivi sasa mzazi huandika maswali ya hesabu kwenye karatasi na kumpa mtoto afanye huku na yeye akiwa anatafuta/ametafuta majibu ya maswali hayo ili mtoto akimaliza amfanyie masahihisho baadae. Jambo hili sasa litaweza kufanyika kwenye simujanja (smartphone) yako.
Hii app inaitwa Mathematics Darasa. Invyofanya kazi ni kuwa mzazi atatakiwa achague aina ya hesabu anazotaka kumpa mtoto:-
  • Kujumlisha (plus)
  • Kutoa (minus)
  • Kuzidisha (multiplication)
  • Kugawanya (divisions)
Mfano akichagua kujumlisha, atatakiwa achague aina za maswali ya kujumlisha kutegemea na ‘level’ ya mtoto.
  • Type I (A+B), tarakimu 1 jumlisha tarakimu moja mf. 3+5=
  • Type II (AB+C), tarakimu 2 jumlisha tarakimu 1 mf. 67+8 =
  • Type III (AB+CD), tarakimu 2 jumlisha tarakimu 2 mf. 47+82 =
  • Type IV (ABC +CD), tarakimu 3 jumlisha tarakimu 2 mf. 823+82 =
  • Type V (ABC+DEF), tarakimu 3 jumlisha tarakimu 3 mf. 428+937 =
Vivo hivyo kwenye kutoa/kuzidisha/kugawanya.
Akishachagua aina ataletewa sehemu yakuweka idadi ya maswali pamoja muda (katika dakika) ambao atahitaji mtoto amalize, yaani mfano mzazi ataingiza labda maswali 50 muda dakika 60 (ambao ni lisaa).

Baada ya hapo app itamletea mtoto swali la kwanza akijibu litakuja la pili mpaka kufikia swali la 50. Akimaliza swali la mwisho (mf. 50) au muda ukiisha (mf. Dakika 60) yatakuja majibu amepata ngapi katika asilimia. Pia kuna sehemu (option) ya ’check corrections’, hapa mtoto ataletewa ‘list’ ya maswali yote aliyojibu, jibu alilojibu pamoja na jibu sahihi.
Hii app haitumii internet. Internet inatakiwa muda wa kudownload tu au pia kuna option ya kushea.
Kuna option imeongezwa inaitwa “3 seconds challenge”. Option hii inakuletea mfuatano wa maswali yasioisha mpaka utakapokosa mda wa kufikiria ni sekunde 3 tu. Hii ni kumfanya mtoto afikirie haraka kutoa jibu. Pia option hii kwa mtu mzima inafurahisha na iko “very exciting”.


Sasa ni muda wa mtu mzima kuweka ‘airplane mode’ simu yako (‘calls’ wala message haziwezi kuingia simu ikiwekwa ‘airplane mode’) ili ukishamuwekea mtoto mfano hesabu za kuzidisha maswali 50 amalize baada ya dakika 60 (lisaa) mtoto asiweze kusumbuliwa. Au mnunulie yake kwa ajili ya kusomea tuu ambapo utaweka mathematics darasa na badhi ya apps zingine kwa ajili ya kujifunza.

Click hapa ikupeleke playstore kupakua/download


Kwa maoni/ushauri au jambo lolote
E-mail: namsweatech@gmail.com
Instagram: mathematicsdarasa
Whatsapp: +255 692 320 855
 

Attachments

  • choose_.PNG
    choose_.PNG
    6.3 KB · Views: 38
  • plus.PNG
    plus.PNG
    9 KB · Views: 33
  • plus01.PNG
    plus01.PNG
    4.2 KB · Views: 36
  • qns.PNG
    qns.PNG
    6 KB · Views: 33
  • endless.PNG
    endless.PNG
    6.6 KB · Views: 35
Back
Top Bottom