Katika hili watanzania tuwe wazalendo!

Katika hili watanzania tuwe wazalendo!

Status
Not open for further replies.

Kamanda Moshi

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
1,983
Reaction score
3,005
Ndugu wana Jukwaa, heshima kwenu wote.

Nimelazimika kuanzisha mada hii ili kujaribu kuwekana sawa katika vitu vidogo vidogo ambavyo tunakosea. Kwa muda sasa kumekuwa na chokochoke za mpakani kati ya Tanzania na Malawi. Ni kwa masikitiko makubwa ninawakilisha kilio changu kuona sisi wana JF ndio wa kwanza kupost post zinazoelekeza/kueleza nini jeshi letu linafanya, wapi kambi ya jeshi iliko nakadhalika. inawezekana hatujui madhara ya maneno yetu au kwa utoto/ujinga tunaona hizo ni habari za kujivunia.

WanaJF wenzangu, hatupaswi kwa namna yeyote kutaja mahali au movement za vyombo vyetu vya ulinzi, tunapotaja hakutusaiidi lolote zaidi ya kumpa faida adui. Mliopita jeshini naamini mnaelewa vizuri sana ninayoyasema. kufahamu location za vifaa/vikosi/commanding post za unayepigana naye ni kujifakikishia 60% ya ushindi.

Hivo basi ninawaomba kwa heshima na taadhima, muache kupost habari inayoelekeza mahali au movement za jeshi letu, huku ni kujisaliti wenyewe ndugu zangu.

mnapopanga vita kitu cha kwanza ni kutafuta/kufanya military intelligence, na katika hiyo intelligence ni mnaangalia commanding areas, rada station, launching station nakadhalika, sasa sisi wana JF ndio tunaokuwa wa kwanza kumpa adui faida kwa kumsaidia kujua wapi kuna nini na nini.

Nawaomba Mods mfute mara moja post zote zinazoelekeza/kueleza movement za Jeshi letu. Hii ni muhimu sana kwa national Security.

najichanganua kama mmoja wa wananchi watiifu kwa nchi yangu Tanzania, naamini katika Tanzania moja huru na inayoheshimika katika mipaka yake. kwangu mimi TANZANIA KWANZA NDIPO ZIFUATE SIASA ZA CHADEMA NA CCM.

BILA TANZANIA HAKUNA CHADEMA WALA CCM. TUIPENDE NCHI YETU TUWE WAZALENDO WA KUPIGA VITA RUSHWA, UMASKINI, UJINGA NA MARADHI.

TANZANIA KWANZA..mengine yatafuata.
Asanteni.

==========
Taarifa:
Kuna taarifa kwenye mitandao ya simu inayoendelea kutolewa kwenye message za simu kwamba kuna Mabomu zaidi ya 30 yenye uzito usiopungua tani 100 na kuwataka wananchi katika mikoa ya Tanzania iliyo jirani na Malawi kuwa waangalifu. Taarifa hiyo imetaka wenye wasiwasi kuhusu taarifa hiyo wapige simu 0756000042. Taarifa hiyo imedai kwamba imetolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Tunapenda kutoa taarifa kwamba taarifa hizo siyo za kweli na lengo lake haliwezi kuwa zuri kwa Watanzania. Wananchi wanashauriwa kutotuma taarifa zozote kwenye namba hiyo ama kuziamini taarifa za aina hiyo.


Assah Mwambene
Mkurugenzi, Idara ya Habari Maelezo.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
22 Oktoba, 2012

Zipo taarifa ambazo katika wiki hii zimetumwa kwa njia ya simu za mikononi (SMS) zikitahadharisha wananchi wasiokote kitu chochote ambacho wana mashaka nacho, kuwa kuna mabomu yamerushwa toka Malawi. Kwamba mabomu hayo yapo zaidi ya 30 na yenye uzito usiopungua tani 100. Aidha, imeelezwa kwamba taarifa hizi zimetolewa na JWTZ/L S 5 CAMRM.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linachukua fursa hii kuwaeleza wananchi wote wa Tanzania kuwa taarifa hizo ni za uzushi na wala hazikutumwa na JWTZ. Uzito wa mabomu ulioelezwa ni mkubwa sana kiasi ambacho ni vigumu kubebwa kwa ndege au kurushwa na mzinga wowote ule. Aidha, zebaki (Mercury) ndio madini nzito kuliko yoyote duniani.

Umbo la chupa ya chai ya madini haya hayawezi kufikia hata kilo 15 (lita yazebaki moja ni sawa na kilo 13.6). Hivyo, hata kama chupa zote 30 zikipimwa hazitazidi kilo 450, hiyo Tani 100 ni kitendawili.

Tunawaomba wananchi wote wazionetaarifa hizi kuwa ni za uzushi na wala hazikutolewa na JWTZ. Hatari ya mabomu haiwezi kutolewa na Jeshi kwa njia ya simu, zitatolewa kupitia Vyombo vya Habari vya Radio, Runinga na magazeti. Aidha, Serikali itatoa taarifa hiyo kwa wananchi kwa kutumia mfumo ulio rasmi zaidi na si kupitia SMS za simu za mikononi.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

SLP 9203, Simu: 0764-742161
 
Naunga mkono hoja, na ningeomba sana MODs waweke vidole vyao kwenye DELETE button saa zote. Unless is absolutely neccesary hata kama utaona ndege ya jeshi letu inapita tafadhali usiandike. Tofauti za kiitikadi ni humu ndani, nje ya mipaka sisi wote ni watanzania.
 
Tumekusoma Mkuu na uko sahihi. Hilo wote tumeliona ingawa yawezekana wachache tumeelewa.
 
Kwa ushauri wako wa busara naomba nisiendelee kuyataja majukumu ya jeshi katika thread yangu, "Vijue vyeo vya jeshi la polisi...viko 16" na wala sitauanzisha ule uzi kuhusu JWTZ. Kiukweli mtandao huu unapendwa sana hapa SA na imagine watu kila kona wanauangalia.........intelijensia ya waMalawi iko humu JF.
 
Naunga mkono hoja. Kuna wengine humu wanafikiri Jeshi letu likizidiwa na adui ni aiubu Kwa JK, Kumbe ni aibu yetu sote kama Taifa.

Amkeni............Uzalendo kwanza
 
Mkuu uko sahihi na nakubaliana na wewe kwa manufaa ya usalama wa nchi yetu...MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Ni kweli nakuunga mkono si mambo ya kutangaza tangaza haya. Hakuna jinsi nawaomba mkiona lolote msitupie hapa jamvini, maana JF ni dunia nzima kwa sasa cyber intelligence ya malawi inalala na kuamkia Jamiiforums na mnajua siku hizi google wanafanya translation ya lugha karibu zote duniani hakuna jinsi ukiona toa taarifa katika vyombio vya usalama kama ni tatizo. Mtoa mada ur 100% correct.
 
Safi sana maelezo uliyoyatoa ila kuna watu sijui kama watakuelewa kwani vyama vimewakaa kichwani kuliko hata mungu alie waumba
 
Mkuu, ile Marekani & Uingereza na washirika wao walipokuwa wanaipiga Iraq mbona tulikuwa tunaona live CNN na SKYNEWS!

Hawakuwa wanahatarisha kuruhusu camera kwenye chimbo zao?

Mimi naona kwa dunia ya sasa huwezi kuzuia hilo. Cha msingi uwe na mbinu nzuri za vita
 
Nakubaliana kabisa na mleta mada,watu wamejisahau sana
 
Mkuu, ile Marekani & Uingereza na washirika wao walipokuwa wanaipiga Iraq mbona tulikuwa tunaona live CNN na SKYNEWS!

Hawakuwa wanahatarisha kuruhusu camera kwenye chimbo zao?

Mimi naona kwa dunia ya sasa huwezi kuzuia hilo. Cha msingi uwe na mbinu nzuri za vita

Unachanganya habari hapo
 
Kwa ushauri wako wa busara naomba nisiendelee kuyataja majukumu ya jeshi katika thread yangu, "Vijue vyeo vya jeshi la polisi...viko 16" na wala sitauanzisha ule uzi kuhusu JWTZ. Kiukweli mtandao huu unapendwa sana hapa SA na imagine watu kila kona wanauangalia.........intelijensia ya waMalawi iko humu JF.

Kiongozi, unaweza kuwasiliana na MODs ili wauweke pembeni ule uzi unaohusu jeshi, walao kwa sasa?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom