Katika hili watanzania tuwe wazalendo!

Status
Not open for further replies.
we can use jf to mislead adui zetu.hivyo nashauri mtanzania anayepost humu jf atambue athari za post yake.

Tukumbuke pia kuna uwezekano wa 'vijana' wa usalama wa malawi wanafanya kazi yao ndani ya jf,tusisahau hilo.

Mwisho kabisa tuwe tayari kupambana na adui yoyote mipakani mwetu bila kujali mifarakano yetu kisiasa au kidini.

MPAKA WA TANZANIA NA MALAWI NI KATIKATI YA ZIWA NYASA NA SI VINGINEVYO-HUO NDIO MSIMAMO WA TANZANIA,TUNAWAJIBIKA KUULINDA NA KUUSIMAMIA KWA GHARAMA YOYOTE ILE.MAJIRANI,WAHISANI NA JUMUIYA YA KIMATAIFA WANAPASWA KUTAMBUA NA KUHESHIMU MSIMAMO HUU.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.

Imetolewa na mwanadada mzalendo.
UDA
 
Naunga mkono hoja. Kuna wengine humu wanafikiri Jeshi letu likizidiwa na adui ni aiubu Kwa JK, Kumbe ni aibu yetu sote kama Taifa.

Amkeni............Uzalendo kwanza

Mkuu na wewe unapata muda wa kuingia humu? Mi nilifikiri tupo wote huku Mbeya tunapiga jaramba?
 
we can use jf to mislead adui zetu.hivyo nashauri mtanzania anayepost humu jf atambue athari za post yake.

Tukumbuke pia kuna uwezekano wa 'vijana' wa usalama wa malawi wanafanya kazi yao ndani ya jf,tusisahau hilo.

Mwisho kabisa tuwe tayari kupambana na adui yoyote mipakani mwetu bila kujali mifarakano yetu kisiasa au kidini.

MPAKA WA TANZANIA NA MALAWI NI KATIKATI YA ZIWA NYASA NA SI VINGINEVYO-HUO NDIO MSIMAMO WA TANZANIA,TUNAWAJIBIKA KUULINDA NA KUUSIMAMIA KWA GHARAMA YOYOTE ILE.MAJIRANI,WAHISANI NA JUMUIYA YA KIMATAIFA WANAPASWA KUTAMBUA NA KUHESHIMU MSIMAMO HUU.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.

Imetolewa na mwanadada mzalendo.
UDA

Aiseee shemeji amebahatika kupata mdada mwenye busara kama wewe nimeipenda hiyo idea ya kuitumia JF kuwamislead Wamalawi
 
kamanda moshi

Mkuu, ulichoongea ni sahihi kabisa katika zama zile! lakini zama hizi za globe positioning na google ni kupoteza wakati, kwanza wamalawi hapa wapo kibao!

Ila niseme kitu kwamba USHINDI ktk VITA una be dertamined katika mambo matatu tu!

1 UCHUMI WENU! Unaweza kuhimili VITA?

2 WATU; Jee umewaandaa watu wako kisaikolojia, pia wameshikamana kitaifa na kuwa wamoja kwa jukumu hilo? mf vita ya kagera!

3 SILAHA; Jee unazo za kutosha na kisasa? sio za kupepea!

Hayo kila moja lina mlolongo wake na mzunguko ukitimia USHINDI NI LAZIMA!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, ile Marekani & Uingereza na washirika wao walipokuwa wanaipiga Iraq mbona tulikuwa tunaona live CNN na SKYNEWS!

Hawakuwa wanahatarisha kuruhusu camera kwenye chimbo zao?

Mimi naona kwa dunia ya sasa huwezi kuzuia hilo. Cha msingi uwe na mbinu nzuri za vita

Jaribu kujiuliza kati ya vita na military intelligence kipi huwa kinatangulia kwanza? nadhani ulichokuwa unakiona cnn na sky news ilikuwa ni vita tayari!!
 
Nakuunga mkono kwa kila hali! Tusiyachukulie mambo haya kimzaha mzaha kama kwamba tunapambana na wanauamsho, au CDM! Hiki ni kitu kingine na nawaomba ma-mod wasisite kuzifunga thred zenye mwelekeo mbaya!
 
Unachanganya habari hapo

Duh! Ukieleza kwaufupi namna hii hueleweki, mkuu

Mimi nikiwa na habari nitapost tu hapa JF. Tuna uhuru wa habari. Kwanza mimi naona hizi habari ndo zinawafanya Wamalawi watugwae. Tunaweza hata tusiingie vitani tukawa tumeshinda kwa mkwara wa movement ya vifaa tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom