Katika hili la Lugha ya Kiswahili, nakupongeza Rais wangu

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,997
20,329
Katika hili la Lugha ya Kiswahili nakupongeza Rais wangu Dokita John Pombe Magufuli...

Tulisubiri muda mrefu sana mtu atakayethubutu kuzungumza kiswahili mbele ya uso wa dunia, haijalishi mkalimani alishikwa butwaa ama laa, lengo kiswahili kimesikika...

Kwa haraka picha hii chini inaonyesha nchi zote zinazoongea kiingereza, marais wake wamevaa vitafsiri masikioni...

Hii inamaanisha muongeaji wakati huo alikuwa haongei kiingereza wala kifaransa, muhimu zaidi zingatia ambaye hana kitafsiri masikioni huyo anaelewa lugha inayozungumzwa muda huo...

Hongera sana rais Magufuli... Lugha ni alama moja wapo ya uzalendo na utaifa wa mtu.

Katika hili ninathubutu kukupongeza kwa dhati kabisha rais wangu, umeonyesha ukomavu na ujasiri wa hali ya juu kuwashinda hata watangulizi wako....

Picha ya pili ni Mwalimu Julius Nyerere akiwa kavaa kifaa cha kutafsiri lugha katika mkutano wa UN, hapa huenda lugha iliyokuwa inazungumzwa ni Kichina au kiarabu maana Mwalimu amefariki akiwa na ujuzi wa lugha sita... Sasa ukiona mwingine hajavaa katika mikutano ya Afrika ambao lugha kuu ni kiingereza, kifaransa, kiarabu, kiswahili na kireno tu basi huyu ni bora

IMG-20170130-WA0156.jpg
images.jpg
 
Mimi nauliza tu, hivi zaidi ya kisukuma na kiswahili kwenye mkutano ule rais alikuwa anaweza kuzungumza lugha gani nyingine?
 
Kazi kweli kweli!

Lakini mkuu hapo paragraph ya 3&4 nimeona waziri wa mambo ya nje amevaa,nafikiri atamjuza baadae!
 
Kuongea kwa kiswahili huku unajua Kiingereza lakini umekiacha ni uzalendo,,, lakini kuongea Kiswahili kwa kuwa haujui kiingereza sio uzalendo ni udhaifu.

Huku mnasifia kiswahili chake mnasahau kuwa watoto wake na watoto wenu wanasoma shule zinaitwa English medium. Speak Swahili by choice not by failure to speak English
 
Mimi pia nampongeza...
Ila tujiulize, Kiswahili kina maana gani katika dunia ya leo (practical world)
Umuhim wa lugha upo kwenye idadi ya watu wanaozungumza na nguvu ya uchumi wa nchi hiyo, sisi tupo wapi?
Ukiongea kiingereza kwa mfano, hapa Africa , more than 70% watakuelewa, then French alafu Kiarabu.
Huu uzalendo tunao uzungumzia usiishie kwenye lugha pekee... Tuwe wazalendo kwa umoja na mshikamano katika kujenga dola imara yenye uchumi imara.
 
Nadhani tujaribu kuwa na uelewa wa mambo hasa pale tunaposifia kitu fulani. Lengo la Magufuli kutumia Kiswahili lilikuwa nini? Kama analenga ku-promote lugha hii basi ile ni mbinu mbovu kabisa. Tujiulize waliokuwa wakimsikiliza ambao hawakielewi Kiswahili waliondoka na faida gani? Zaidi sana ukiangalia kwenye video they were simply bored.
Kama lengo ni ku-promote Kiswahili tunatakiwa kuandaa watu watakaokuwa na uwezo wa kuifundisha hii lugha barani Afrika na kisha kuweka utaratibu wa kuifundisha kama somo mashuleni na kwenye vyuo barani kote.
Tuanzishe pia Swahili Language Schools au cultural centres kwenye nchi nyingi iwezekanavyo kama Wachina walivyo na Confucius Institutes kwenye nchi zetu.
Hii ndiyo mbinu sahihi badala ya kuwakalisha watu na kuwalazimisha kusikiliza lugha ambayo hawaielewi wala hawatakaa waitumie.
Tuwe proactive kwanza badala ya kusifia tu kila kitu. Leo hii ukiuliza nini kimekuwa accomplished na Magufuli kuhutubia kwa Kiswahili ni kwamba hakuna kitu; tutengeneze mikakati ya kukuza lugha hii na si matukio ya dakika chache yasiyo na maana yoyote.
BAKITA ifutiliwe mbali halafu iundwe upya kwa kutumia wataalamu wa lugha watakaoivalisha sura mpya kuliko fedheha iliyopo sasa.
 
Back
Top Bottom