#COVID19 Katika hili la Covid-19, nimejifunza sisi Watanzania ni wakushikiliwa akili

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,690
1,942
Watu tumekaa kumlaumu Rais wetu eti hajasema kuwa Corona ipo. Huu ni ujinga uliyopitiliza kwa kweli.Matendo Huwa yanasema kuliko maneno.

Mfano, Mzuri ni huu: Waziri Jafo alipotangaza Siku saba za kujifukiza, nyie watanzania wa kushikiliwa akili mlifikiri tafsiri yake nini? Ok tuache hili.

Taarifa zilisambaa zikionyesha Hayati Maalim Seif ameambukizwa corona, yani na hili hamkuamini kuwa Corona ipo mpaka Rais au waziri atangaze?

Akili za kushikiliwa hizi. Walipotangaza kuwa kuna dawa za Nimcaf na Covidol zinatibu mafua makali hapo Akili zenu ziliwambia nini? Akili za kushikiliwa

Wasomi wengi wamejaa Tanzania. Usomi wenu umesaidia nini. hamsomi updates za Corona mpaka Rais au waziri aseme kwamba vaeni barakoa?

Nimeona Mtu kama mwenyekiti wa chama anahamasisha watanzania waorodheshe idadi ya ndungu zao waliyokufa eti hapo baadae watakuja Kumdai JPM kwa nini hakusema Corona ipo. Akili hizi za kushikiliwa hizi.

Hawaambii wanachama wake wajikinge au kufuata health standards ili wasiambukizwe. Nimemuona mtu aitwaye Hilda akihamasisha wapinzani ambao ni tishio kwa serikali eti wakiumwa corona wasiende kutibiwa kwa hospitali za serikali.

Ningekuwa mimi ndiye Rais, nakutafuta nakutia ndani for the remaining five years maana mtu wa namna hii ni Muuaji kabisa.

Rais alichokisema ni kwamba hata lock down wananchi wake (nitajie nchi kwa sasa imelock down wananchi wake) lakini hakukataza Kuvaa barakoa, hakukataza kunawa mikono, hakataza social distancing (at least 2 Meters from one another) etc.

Sasa mnaomtukana sijui kosa lake liko wapi? Akili zenu za kushikilwa tu. Watanzania wengi tuko kama makinda ambayo hayajajua kujitafutia chakula.

Rais ametangaza siku tatu za Maombi. Bado liko kundi la watu ambao hata kanisani au msikitini hawaendi wanamdhihaki Rais kwa hili. Hizi ni akili za kushikikiwa.

Hamsomi Biblia au Quran lakini mnachojua ni kutukana tu. Mkatoliki mwaminifu ukimpa dawa ameze anapiga sala ya msalaba kwanza ndipo anameza dawa. Sasa kama Tukimwomba Muumba wetu, tukanawa mikono,tukavaa barakoa, tukajiepusha misongamano hapo kosa la Rais wetu kumtanguliza Mungu katika yote liko wapi jamani?

Mnakataa kumuomba Mungu lakini mkifiwa mnawita Padri au sheikh au mchungaji awasalie kwa Muumba yupi?

Lakini Dunia ifahamu ya kuwa Mungu yupo. Yule aliyemtetea Eliah, aliyewatetea Shadrack na ndugu zake, aliyemponya Daniel midomoni mwa Simba ndiye atayemtetea Rais wetu na wananchi wake.Mungu hajikani. Wewe unayetukana na kuamini sayansi tu haulazimishwi kushikiliwa akili.

Sabato njema
 
Waangalie hao wateule wanaongoza kushikiliwa akili ,boss akivaa tu wote watavaa
JamiiForums-780430982.jpg
 
Waangalie hao wateule wanaongoza kushikiliwa akili ,boss akivaa tu wote watavaaView attachment 1707016
Je kuna mahala amesema wakivaa atawatimua? Sikia eeh Mtanzania,watu waliyostarabika akisikia mafua anavaa barakoa au kitambaa kuzuia maambikizi kwa wenzake. Afu barakoa inafaa kuwalipa na mwenye dalili za kikohozi au mafua au ukivaa uvae na mawani au watu wakivaa wote
 
sayansi isifundishwe mashuleni, siyo muhimu kwa nchi yetu.
Mkatoliki mwaminifu ukimpa dawa ameze anapiga sala ya msalaba kwanza ndipo anameza dawa.......

Hapo unaona kuna mwanasayansi ametengeneza dawa,mtumiaji anaiombea kwanza ifanye kazi vizuri
 
Watu wengine naturally akili zao zinategemea wengine haziko matured hivyo wanahitaji kuongozwa tusiwalaumu .Na huyo nutcase wetu inamgharimu kiasi gani kukuri uwepo wa tatizo huoni kuwa anain confuse society
 
Yani umeandika utopolo mtupu, yaani hata ujui Rais ni nani, Yule ni amiri jeshi mkuu ndugu na nchi ni kama ipo vitani.

Maamiri jeshi wa nchi zinazojitambua wanaongoza mapambano katika janga hili,kuhusu kutumia akili basi si Watanzania tu ambao hawatumii Mbona yeye havai barakoa Hakuna sacial distance hata yeye halipo cabinet yake yote pia aina akili kwa sababu nao tunawaona wanapuyanga tu,acha kuropoka Kiongozi, tafakari.
 
''...Akili za kuambiwa changanya na zako...'' Alisika jamaa mmoja mweupe
 
Mi nawashangaa watu San..! Kam mnajidanganya kuvaa barakoa ndo unajikinga Basi US watu wasingekufa kama kuku kwa mazingira ya nchi yetu kuvaa barakoa haisadii peke yake...!
 
Back
Top Bottom