Katika hili Dr. Slaa amedhihirisha Tundu Lissu alikurupuka na kuna mgongano ndani ya CHADEMA

Yes! Dokta alijibu vyema, swala la Zitto sio kipaumbele cha Chadema na haikuwa na haja ya Dokta Slaa kuandika barua sababu ni swala la kikatiba na LISSU kama M/sharia wa chama alielezea katiba inasemaje?

Kama chama kilitaka NEC, BUNGE na Zitto wajiongeze.. badala yake wakataka kuanzisha ligi, chama kikawapuuza, hatimaye Zitto aliyesema atakuwa wa mwisho, hajakuwa wa mwisho wala wa kwanza, alikuwepo Kabourou na alishika nyadhifa kubwa CHADEMA kuliko Zitto, ametoka na Chama hakijayumba kipo zaidi ya pale

NEC, BUNGE NA ZITTO wajiongeze kwa lipi? unafikiri sheria ni kujiongeza tuu?? inamaana tundu lisu alikuwa hajui sheria ya kumfuta mwanachama uwanachama inasema vipi?? WEWE NDO UNATAKIWA UJIONGEZE
 
CDM kama alivyo lissu na slaa, hatukurupuki. Tafuta hoja nyingine kibaraka wa ZZK. Kwani leo hujui kama kajiunga na ACT academia FM, maana ACT Chipolopolo ya LIMBU hata haimtambui
 
NEC, BUNGE NA ZITTO wajiongeze kwa lipi? unafikiri sheria ni kujiongeza tuu?? inamaana tundu lisu alikuwa hajui sheria ya kumfuta mwanachama uwanachama inasema vipi?? WEWE NDO UNATAKIWA UJIONGEZE

Wajiongeze, wajue Katiba ya nchi inasemaje, Zitto alipoteza sifa ya kuwa Mwanachama, hilo swala halikuhitaji Kamati Kuu ya Chadema kuketi, wala Baraza kuu, Makelele yaliyoanzishwa ni kutokana na ujinga wa kutoijua Katiba, No research no right to speak walisema bado ni mbunge kwa vigezo vipi?

Chadema hatushindani kwa ujinga, huwa tunawaacha wajinga wajazane ujinga
 
nini tafasiri ya usomi?wingi wa degree za kudesa.au uwezo wa kudadavua mambo kulingana na wakati na mazingira husika?
 
wajiongeze, wajue katiba ya nchi inasemaje, zitto alipoteza sifa ya kuwa mwanachama, hilo swala halikuhitaji kamati kuu ya chadema kuketi, wala baraza kuu, makelele yaliyoanzishwa ni kutokana na ujinga wa kutoijua katiba, no research no right to speak walisema bado ni mbunge kwa vigezo vipi?

Chadema hatushindani kwa ujinga, huwa tunawaacha wajinga wajazane ujinga

hakuna katiba mbovu na ya kidikteta duniani kama ya chadema.
 
hakuna katiba mbovu na ya kidikteta duniani kama ya chadema.

Katiba ya Chadema haikuandikwa kwa ajili ya watanzania wote, ila ni kwa ajili ya Wanachadema, na iliandikwa na wanachadema ikapitishwa na wanachadema na mwanachadema yeyote lazima aifuate

Ukijiunga na Chadema, unasisitizwa usome katiba, kama utakubaliana nayo then utajua likupasalo kufanya.

Mimi nimeisoma na kuikuabali katiba ya CHADEMA, na naiona Katiba ya CCM ni mbovu kuliko sababu haitumiki vile ilivyo
 
ni fikira zako, lakini kwa mtu ambae ameona mbali, zitto aliona mbali zaidi ya wewe unavyoona, na mpongeza sana zito, zitto chama alichoingia wewe umeona jana akichukua kadi adhalani lakini sisi tuliokuwa tunafatilia nyendo za zitto tangia zamani tunajua kabisa kuwa chama hiki ni cha zitto, ndie alieanzisha lengo kuu ndoto yake yakuwa mwenyekiti wa chama taifa, na kutokana na katiba ya chama hicho hivi karibuni wanafanya uchaguzi na zitto ndie atakae kuwa kiongozi wa chama hicho, wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa zito alifanya kampeni kubwa kigoma mjini, ngome zote za chadema kugeuka kuwa ngome ya ACT, na alifanikiwa kwa upande wa kigoma ujiji, ukifatilia utaona hata aliyekuwa mwenyekiti wa chadema kwa muda mrefu mzee kasisiko ndio walianza kuweka mazingira mazuri ndani ya chama hicho na penda kuwaambia kuwa chama hiki lengo kuu kuwa chama kinachowakilisha ukanda wa kigoma, mkakati mkubwa uliopo nikuchuka ngome ya NCCR MAGEUZI iliochukua nafasi kubwa mkoani kigoma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom