Katika hili Dr. Slaa amedhihirisha Tundu Lissu alikurupuka na kuna mgongano ndani ya CHADEMA

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,210
42,072
Wasalaam wana jamvi!

Wana jamvi mtakumbuka baada ya hukumu ya mahama kuu juu ya swala la Mh Zitto na chadema..! Tundu Lissu kwa haraka aliitisha vyombo vya habari akiwa pembeni na Godbless J Lema sambamba na Dr.W.Slaa na kutangaza kuwa Zitto si mwanachama wa Chadema!

Baada ya hilo watu wengi walikuwa na maoni tofauti juu ya hatua ya Lissu na baadhi ya wabunge wachadema walionesha kuwa Tundu Lissu alikuwa amekurupuka na si mtulivu kabisa hawa walikuwa ni Mh Mdee na Mh Wenje!

Lakini hivi karibuni Dr Slaa amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari alipo ulizwa swala la kuwaandikia barua tume ya uchaguzi ya kuthibitisha kumvua ubunge Zitto kabwe ili nao wa muandikiea Spika lakini cha kushangaza Dr Slaa alinukuliwa akisema Swala la kumvua ubunge Zitto kwao si kipaumbe bali wana mambo mengi ya kufanya!

Hapa ndio wana jamvi mnaweza kujiuliza Chadema ni chama cha namna gani? Chadema ni chama cha wakurukupaji? Ni majuzi Lissu aliulizwa swala la kuwaandikia tume ya uchaguzi barua na akasema kuwa hiyo ni kazi ya Dr Slaa lakini mtu mnaweza kujiuliza Slaa na Chadema hawakufahamu kuwa wanatakiwa kuwaandikia tume ya uchaguzi barua ya kumvua uanachama Zitto? au wanafikiri ubunge huvuliwa kwa mdomo?

Pamoja na maneno ya Dr Slaa kuonesha Lissu alikurupuka lakini tusisahau wakati Lissu anatoa tamko Slaa na Lema walikuwa pembeni hivyo alikuwa anajua anacho takiwa kufanya.

Hivi ni kama ni kweli swala la Zitto halikuwa kipaumbele kwa Chadema zile mbwembwe za kuita waandishi wa habari zilitoka wapi?Ni kweli Slaa ameshindwa kuwaandikia NEC barua? Chadema na Slaa wanaogopa na wanakwamishwa na nini?

Katika hili ni wazi kuna mvutano ndani ya chadema juu ya swala la Zitto lasivyo Slaa ange shaiandikia barua NEC maana hiyo barua haihiitaji masaa mawili!

Ni lini viongozi wa chadema wataacha kukurupuka?wana tofauti gani na futuhi?
 
Last edited by a moderator:

Hii hadithi yako inatufundisha nini?
 
Last edited by a moderator:
Mansour alipofukuzwa CCM hawakumpa nafasi ili atoe hotuba ya mwisho lakini Leo msaliti aliyekuwa akitumiwa na CCM anapewa asante ya nafasi ya kukipaka matope chama kilichomfukuza, hii ni aibu.
 
You are too low!!!

Lissu hakutangaza uamuzi Wa chama kumvua uanachama Zitto alisoma na kufafanua katiba..

Unapoona umevunja katiba huna haja ya kuandikiwa barua uambiwe umevunja katiba....

Lissu alisema kwa mujibu Wa katiba Zitto kajifukuzisha uanachama sasa unataka mpaka aandikiwe barua yeye katiba haijui?

Rais akidhalilisha kiti cha urais anaandikiwa na nani barua kuambiwa ajiuzulu kwa mujibu Wa katiba?

Zitto kwanini anasubiri barua wakati kikatiba si mwanachama tena?

Acheni upuuzi....
 
Upepo wa zito umeondoa paa zote ufipa, zito balaa. Babu sukari yake imegeuka, ilikuwa ya kupanda sasa hivi inashuka ovyoovyo tu. Anahitaji maombi

.
 
Nakubaliana na Chadema...issue isiwe kumfukuza Zitto bungeni. Wamuache amalize muda wake ndio aende. Mwisho wa siku siasa na wana siasa ni wale wale...wote dugu moja
 
Ruttashobolwa

Mkuu nionavyo mimi ni kuwa Chadema hawana shida na "Ubunge" wa Zitto bali wana shida na "Uanachama wake Chadema". Hoja kwamba kuandika barua ya kumwachisha sio kipaumbele chao cha sasa inaleta tafsiri ya kuwa wanamtaka aamue mwenyewe kusuka ama kunyoa i.e abaki akielea au ajinyenyekeshe kuomba barua rasmi!
 
Last edited by a moderator:
Mbona CCM badala ya kushangilia upinzani umevurugana wao ndio wanaumia zaidi. Au ndio maana baada ya kuona kete yao ya mwisho imeshindwa ndio wakaanza kutoa unabii wa mgombe uraisi kufa kabla ya April 30 kupitia wale watumwa wao kama Shekhe Yahya alivyofanya 2010 kabla ya Makyembe kuufichuo ule mkakati wao na Wasomali?

Kwa kusoma mazingira ya MaCCM wanavyohangaika, huenda haya ndio yaliokuwa maamuzi bora kabisa bila kujali USAHIHI wa tuhuma zidi ya Zitto.

Nafikiri kwa tafsiri RAHISI kabisa, LISSU hajamfukuza uanachama Zitto kama inavyodaiwa na hana mamlaka hio, Bali alinukuliwa akisema ''Kulingana na KATIBA, Zitto sio Mwanachama Tena'' sasa hapa Lissu alaumiwe kwa kuinukuu katiba au kwa wananchi kujua katiba inachosema juu ya mwanachama wa CDM anayekwenda mahakamani kwa mambo ya chama?

Japo watu wana mahaba na vyama au watu, itoshe na ifike mahali nyuma ya keyboard zetu tutumie Ubongo walao kidogo sio kuja tu na porojo por0jo zisizoeleweka.
 
CDM, CDM ccm wanahaha uchaguzi huu ndio mgumu na hawana puppet ndani ya CHADEMA, wakati huo CDM ina zaidi ya intellejensia ndani ya CCM na serikali inayoiongoza.

Hiki kitu kinawanyima usingizi CCM, how can they create their root inside CDM, unajua kupigana na adui unaemjua ni RAhisi kuliko adui usiemjua, Hiki kinakitesa CHAMA CHA MAPINDUZI, maana awali ZZK alikuwapo kuvujisha siri za CHAMA sasa mmebaki ukiwa, ni propoganda tu juu ya CDM

Mbona hamuiandiki CUF kwani kuna amani huko? Lakn enzi izo mliisakama.

Mbona hamuiandiki CCK na kuna fukuto huko, joto hasira. CDM ndio mti wenye matunda, nasi tunalijua hilo

Then wafuasi wa ZZK wanahangaika hapa kwasababu sasa hawatakuwa na ajira, walilipwa kuiua CDM mfereji wa ajira umekatwa, where else to go zaidi ya kuja JF kuinanga CDM.
 
Ruttashobolwa kuna mambo hayaitaji ubongo mpana kuyang`amua,,unafahamu kitu kinaitwa official(rasmi)?..Kitu kuwa rasmi kinataratibu zake,technically Zitto si mwanachadema,hata kama taratibu rasmi hazijakamilishwa.Na hicho ndicho alichofanya T.L.kUTAFSIRI.Ni lini na wapi mtu alifukuzwa kwa kauli ya mdomo ndio ikawa rasmi.Sasa hii nayo ni rocket science?..Jiongeze mkuu
 
You are too low!!!

Lissu hakutangaza uamuzi Wa chama kumvua uanachama Zitto alisoma na kufafanua katiba..

Unapoona umevunja katiba huna haja ya kuandikiwa barua uambiwe umevunja katiba....

Lissu alisema kwa mujibu Wa katiba Zitto kajifukuzisha uanachama sasa unataka mpaka aandikiwe barua yeye katiba haijui?

Rais akidhalilisha kiti cha urais anaandikiwa na nani barua kuambiwa ajiuzulu kwa mujibu Wa katiba?

Zitto kwanini anasubiri barua wakati kikatiba si mwanachama tena?

Acheni upuuzi....

Hawa watu ni wapuuzi haina hata haja ya kuhangaika nao sana

Sasa huyu jamaa ambaye nasikia ni mwanasheria ameweka hoja gani hapa...Mkuu lusungo hawa watu ni wa kuwadharu tu

Anajua maana ya vipaumbele huyu?

Sio priority ya CHADEMA kwa sasa ku deal na barua za kina zito...Priority za msingi zipo hilo la barua litafanywa tu kwa wakati wake
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom