Katibu wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, Raphael Mwaitege, ajiuzulu

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mbeya Mjini, Raphael Mwaitege, ametangaza kujivua wadhifa huo pamoja na nafasi zote alizokuwa anazishikilia ndani ya chama hicho pamoja na kujivua uanachama akidai kuwa anataka kupumzika siasa.

Akizungumza na wandishi wa Habari jijini hapa leo, Mwaitege amesema ameamua kuachana na chama hicho kikuu cha upinzani kutokana na vitisho alivyokuwa anavipata kutoka kwa wanachama wenzake waliokuwa wanamtishia maisha.

Hata hivyo ameweka wazi kuwa, pamoja na kutaka kupumzika siasa ili kunusuru maisha yake, anavutiwa na sera za Chama cha Mapinduzi (CCM).
Sababu ni vitisho au sera?
 
Kaelewa kazi inayofanywa na JPM kaona aondokane na genge la wahuni
 
Hata mtulia alisema hivyohivyo, yeye aende tu. Kasema ukweli Kuwa anapumzika siasa
Uchaguzi umekaribia, na huyo keshashikishwa chake. Wengine wengi wa aina hii bado wanakuja. Angalau muziki umebadilika kidogo, sasa hivi si kuunga mkono tena, bali ni kupumzika siasa. Cha ajabu mtu anapumzika siasa mpaka na uanachama anapumzika. Au waliokuwa wanatishia maisha walikuwa wanaitaka kadi yake ya uanachama nini, hali iliyomfanya aamue kuirudisha ili kunusuru maisha yake. Kweli vituko vya nchi hii haviishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ametoa wapi hela za kujenga ofisi nzuri namna hii jimboni kwake alafu hela za kujengea makao makuu ya chama hana?

Mbowe acha usanii hela za jimbo badala ya kuzipeleka kwa wanachi kama Sugu anavyofanya wewe unazijengea ofisi ya mbunge kana kwamba utakuwa mbunge wa milele??

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom