Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana uliofanyika Yombwe old kiomboi,katibu wa Chadema wilaya ya iramba bwana Jose Alfayo amesema,Mwigulu amefanya ziara jimboni iramba na kujikosha kwa wanairamba kwa kuwalipia michango ya maabara.
Akifafanua kauli yake katibu huyu wa chadema alitanabaisha kuwa mwezi june mwaka huu walimwandikia barua DC wa iramba wakimtaka asitishe uchangishasha wa kibabe wa michango ya maabara na chf,kwa kuwa hawakuwashirikisha wananchi kupanga viwango vya michango na hawakuwahi kuwasomea mapato na matumizi yaliyopita.Mwigulu aliungana na DC kwa kutoa gari yake ya matangazo izunguke wilaya yote kutisha watu na kuwasweka polisi wengine wakishitakiwa mahakamani.
Ajabu leo mwigulu anawalipia michango hiyo wakati ni yeye na DC walioishadidia na kuwatesa wananchi maskini.Katibu wa Chadema aliendelea kusema,mwigulu ni mnafiki,baada ya kuona zoezi lake la kuwanyonya wananchi kwa michango ya kibabe limeleta chuki kwa serikali ya ccm,na hivyo litawaweka katika wakati mgumu kwenye chaguzi.