Katibu wa CHADEMA Iringa, Jackson Mnyawami akamatwa na Polisi kwa tuhuma ya kutoa lugha ya kuudhi dhidi ya DC Kilolo

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,524
2,000

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Juma Abdallah!

Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa Jackson Mnyawami, amekamatwa na Polisi jioni hii na kupelekwa Kituo cha Polisi Mazombe Wilayani Kilolo kwa kutuhuma ya kutoa lugha ya kuudhi mtandaoni dhidi ya Mkuu wa wilaya ya Kilolo.

Inadaiwa kwamba Mnyawami aliweka kwenye kundi la wana Kilolo video yenye nukuu ya majaji wakizungumzia uvunjwaji wa sheria unaofanywa na baadhi ya Wakuu wa Wilaya nchini na kuandika maneno yenye kuonesha kwamba ujumbe huo unamhusu pia Mkuu huyo wa Wilaya.

MUENDELEZO
-------------------
Bw. Mnyawami ameachiwa na Polisi muda mfupi uliopita kwa kujidhamini yeye Mwenyewe!!
 

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
22,920
2,000
Kipindi nikiwa kijana nilikuwa nasumbuliwa sana na wanawake ila nilipokuja kuwajua wanawake wanataka nini wala hawanisumbui tena.
 

Silverone

Senior Member
Jun 29, 2018
126
250
Demokrasia ni gharama, ninaamini ipo siku yatakwisha, hakuna marefu yasiyo na mwisho, makamanda tuvumilie yote safari yenye mafanikio si nyepesi
 

Barack Obama jr

JF-Expert Member
Dec 23, 2017
599
1,000
Ukitaka uyaepuke haya yanayotendeka kwa wakosoaji wa serikali hii na viongozi wake ujitie upuuzi tu wa kushangilia kila jambo toka kwao
 

gunz

JF-Expert Member
Jun 30, 2018
300
500
Hakuna aliye juu ya sheria. Hivi upuuzi anaoongea jiwe mara kwa mara na watu wanapiga makofi. Ukiongea mtu wa kawaida inakuwaje?au sheria ina matabaka?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom