Katibu wa ccm kuzunguka na mawaziri

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
8,548
8,691
Hili la katibu mkuu wa CCM kuzunguka na mawaziri kuelezea mafanikio ("anyway" na mikanganyiko) ya serikali inatokakana na mfumo wa katiba ipi?
Kwenye mihimili ya serikali kwa mujibu ya katiba ya sasa hili la katibu mkuu wa chama kuwasimamia mawaziri mbona halijaandikwa?Au ni utawala usio wa sheria?
Naomba wataalamu wa sheria wanisaidie kulielewa hili maana kuna jamii ambayo inatuzunguka tuielimishe kwa hili
 

katalina

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
262
52
Binafsi sioni tatizo kwa sababu mawaziri ni wanasiasa na wanakagua utekelezwaji wa ilani yao. Kwahiyo kutembea na katibu wa ccm naona ni sahihi. Tunachokataa ni watendaji au watumishi wa umma kama TANROADS, TANESCO, etc kwenda kutoa ufafanuzi wa wanayoyafanya kwenye mikutano ya siasa ya ccm. Aidha kwa upande wa mawaziri ndo maana wadau wanapiga kelele kwamba mawaziri wasiwe wabunge. Kama mawaziri wasingekuwa wanasiasa, then waziri kutembea na katibu wa ccm hapo kidogo ingekuwa na walakini. Haya ndo maoni yangu wakuu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom