Katibu wa CCM Kata ya Mwaruguru auwawa kwa kuchinjwa kama kuku

Nilisema ule wakati wa kuwa wao hawafi umepitwa na wakati ,wajue kuwa wanaongoza binadamu sio ng'ombe ,kwamba utapowavuta ndio hukohuko.

Hata kama wameuwana wenyewe kwa wenyewe ndio vizuri zaidi,ila wao sio wa mwanzo kwani pale bungeni wangapi wamepata vifo vya gafula,kuna kesi zinazopigiwa mfano "Kukolimbana" hii ni kitu gani ,kuna kesi ya Sokoine mpaka leo imefungika hakuna uwazi ,yaani kuna wengi tu ila sasa mambo yanatua mitaani huko ndiko atakakofungwa paka kengere ,maana usipoziba ufa utajenga ukuta ,miccm ikiambiwa nchi inaenda mrama wao wanakazana kujaza viroba na kuondosha hela nchini ,we wacha tu kuna waTz wananukia kupelekwa Hague ,mmemuona mwenzenu na uraisi wake kabwaga manyanga kwa hiari yeke kaelekea huko ,na nyinyi wekeni pamba masikioni dawa naamini ipo jikoni inachemka. Zibeni macho tu mkikodolea rasilimali za Taifa.
 
Kwani ccm nao wanajiita MAKAMANDA? watz tuendako ni kuzuri sana tena bado..ubabe wa ccm umefanya watz tufike hapo its good. halafu mleta uzi huu kwa sababu 1 au nyingine unahusika na mauaji haya coz ulijuaje kama kauliwa kwa mambo ya kisiasa? we ndo muuaji namba 1.

Poleni wafiwa
. Kwa hali mbaya ya kisiasa na mvuto ilivyo kwa pabde wa CCM nina mashaka kama kauwawa na watu nje ya CCM. Hapa kuna sababu nyingi baadhi ni kama zifuatazo:-
1. Inawezekana aliletewa fedha za kukisaidia chama kutoka katika chama chake, mfadhiri au mgombea ili zigawanywe kwa wapiga kura yeye akafanya zake.
2.Inawezekana mtu wa kundi lake hakupotishwa hivyo kuwageuka wenzake na wenzake wakaamua kumumaliza ili asiendelee kuumiza chama, haya ni maoni yangu tu .
 
Mtu hawezi kuuliwa bila sababu...hata kama ni ya kusingiziwa...tafuta chanzo cha kifo chake alafu uludi utuambie ukweli
 
Alivyo Chinjwa Mbwambo Kule USA River mkasema ana roho ya Plastic,
All in all,RIP katibu
Hivi mnataka kuifanya.Tanzania iweje?
Kwa ajili.Mbwambo alichinjwa basi ni ruksa kila mtu kufanyiwa unyama wa aina hiyo?
Ifike mahali tukemee huu ujinga. Ushabiki wa vyama usituondoe katika misingi ya ubinadamu.
TUNAUNGANA PAMOJA KULAANI UNYAMA KAMA HUU KWA BINADAMU WENZETU!
 
Ndani ya CCM wengi wamepoteza maisha... R.I.P Mbwambo, Mvungi, Mwangosi, Sokoine, Kolimba, Mgimwa, Nyerere, Malima, Peter Hassan, Karume, Mine, Akili, Tamim et al...
 
Ngumu sana kuingia akilini maana Watanzania wengi sana WAMECHINJWA mahospitalini baada ya kukosa madawa kuliko sababishwa na sakata la ESCROW!!!! Grrrrrrr Magamba yaadabishwe tu TUMECHOKA.... R.I.P Wahanga waliokosa madawa

Hivi mnataka kuifanya.Tanzania iweje?
Kwa ajili.Mbwambo alichinjwa basi ni ruksa kila mtu kufanyiwa unyama wa aina hiyo?
Ifike mahali tukemee huu ujinga. Ushabiki wa vyama usituondoe katika misingi ya ubinadamu.
TUNAUNGANA PAMOJA KULAANI UNYAMA KAMA HUU KWA BINADAMU WENZETU!
 
Usisahau diwani wa Kata ya Bugarama Kahama kabla ya wilaya mpya ya Msalala alivyouawa kama huyo unayemsema kisa kamshinda kura za maoni diwani aliyekuwepo wote chama kimoja.
Iweke vizuri taarifa yako tupate pa kuanzia maana haya magamba hayachelewi kuhusisha kifo hiki na ukawa. R.I.P fisadi
 
Natamani Kuiweka Picha ya Mwili wa Katibu AlieChinjwa APA lakini Naona Sio Sahihi.
Amechinjwa akiwa Kavalia Shati LA CCM akiwa Kazini kukijenga Chama.

Weka kama huna acha kutusumbua hapa watu tuna machungu kweli,nimepiga simu kwa katibu wa kata yangu CCM ,kasema ni kweli na walikuwa wote Kahama kwenye mkutano wa makatibu wote.
 
Hivi mnataka kuifanya.Tanzania iweje?
Kwa ajili.Mbwambo alichinjwa basi ni ruksa kila mtu kufanyiwa unyama wa aina hiyo?
Ifike mahali tukemee huu ujinga. Ushabiki wa vyama usituondoe katika misingi ya ubinadamu.
TUNAUNGANA PAMOJA KULAANI UNYAMA KAMA HUU KWA BINADAMU WENZETU!

Nani hao wanataka kuifanya Tanzania iweje ? Hivi wewe unaishi nchi gani ,huyaoni,huyasikii au huyapendi ,huyu si Mtz wa mwanzo kuuliwa wapo wengie mbali ya waliomwagiwa acid ,mbali ya waliookotwa mabwepande, Mlikuwa wapi ,au kisu kimegusa mfupa ,ndio kwa macho yenu mnaona Tanzania inataka kupelekwa kwengine,hapana ndugu ,njia mnayowapelekea WaTz sasa wanaamua kuipita hiyohiyo.
 
Rest in Hell Gamba,

Kule motoni wewe utaenda kua KUNI, yaani bottom kabisa ya lile shimo!!
 
Hivi mnataka kuifanya.Tanzania iweje?
Kwa ajili.Mbwambo alichinjwa basi ni ruksa kila mtu kufanyiwa unyama wa aina hiyo?
Ifike mahali tukemee huu ujinga. Ushabiki wa vyama usituondoe katika misingi ya ubinadamu.
TUNAUNGANA PAMOJA KULAANI UNYAMA KAMA HUU KWA BINADAMU WENZETU!

Kaanze kulaani kwanza Mauaji ya Mbwambo na wale waliolipiuliwa na Bomu kwenye mikutano ya CHADEMA then njoo na hizi ngonjera zako
 
TULIKOFIKIA WATANZANIA NIKUBAYA SANA.

Nalaani Kwa Nguvu Zote Kwa Wanasiasa wanaofanya unyama wa Namna hii.
Siasa za Tanzania Zimekuwa Siasa za Ajabu sana sana kwani Mauwaji, Villema, Wanaongezeka Kisa tu Uroho wa Madaraka.
Timama hii....
Huu ni mwili wa Katibu wa ccm kata ya mwaruguru aliyechinjwa Jana usiku
Maeneo ya Kagongwa Kahama Shinyanga.

Tumefikia Hatua yakuuwana Kisa Vyeo vya Serikali za Mitaa !!?
Kweli Mtanzania Unaejitambua Ulieshida Imani ya Dini Na Hofu ya Mungu unamuuwa Mwenzio Kisa Cheo cha Kisiasa?

Nimeumizwa sana Na Kitendo hiki cha Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Kuuwawa Kinyama Kwa Kuchinjwa kama Kuku kisha Kutelekezwa.

Hakika Duniani Tunapita tu !
Hukumu iko Kwa Mungu wale wote watendao Madhambi haya kisa Madaraka Mungu atalipa Kwa Imani yetu tunaoamini.
But Seikali Na Jeshi LA Police Tunaliomba Lifanye kazi yake Kwa Ufasaha kabisa likishirikiana Na Raia wema kuwafichua watu Hawa waovu, Mimi Naamini Watendaji wa Matukio haya tunaishi nao Mitaani ivo tunauwezo mkubwa wakuwasemea ktk Vyombo Vya Usalama Wawajibishwe.

Samahani Kwa Picha hii najua sio Ethical Kwa Haki za Kibinadamu pia Media Ethics haziruhusu imenilazimu Kufanya Kwa Maumivu ninayoyapata hapa.

RIP Ndugu yetu Kamanda Na Kada wa Chama Cha Mapinduzi.
Naamini umekufa kishujaa kite tea Chama chako Na Haki yako yakimsingi Umechinjwa Na uniform ya Chama Cha Mapinduzi .
Hakika Umekifia Chama.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Amen......!!
Mleta mada pamoja na kuonyesha unyama huo kwa uchungu mkubwa lakini maandishi yako ni ya kichochezi. Umetoa hitimisho linalolenga kuonyesha mauaji ni ya kisiasa wakati yawezekana kuwa ni sababu tofauti kabisa. Kisha umeonekana kufikiria kuwa atakuwa kauawa na mahasimu wa kisiasa wa chama chake ambayo pia yawezekana isiwe na ukweli. Tumwombee marehemu na wakati huo huo tujiadhari kusambaza chuku kwa taarifa zisizo sahihi.
 
Back
Top Bottom