Katibu wa bunge na Spika wake wapimwe akili zao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu wa bunge na Spika wake wapimwe akili zao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mamaWILLE, Oct 27, 2011.

 1. mamaWILLE

  mamaWILLE Senior Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  leo katibu wa bunge ameutangazia umma kuwa Zitto kabwe yu mzima anaendelea vizuri na matibabu tucwe na wacwac.

  Hoja yangu ni kwamba ni kweli tanzania hatuwezi kumtibu mtu mwenye malaria kama ya Zitto? Kweli jamani hata malaria mpaka india? Yaani kweli muhimbili hawawezi kutibu malari? Agha khan hawawezi kutibu malaria? Daa tumekwisha

  Madai yangu Zitto haumwi malaria hapa kuna usanii mtupu. Katibu wa bunge na spika wake wakapimwe akili zao hawawezi kutudanganya kiasi hiki. Jamani inatosha sasa kudanganyana.

  Na ukiona serikali inalidanga taifa wazwaz basi kuna njama kali sana zimepangwa zidi ya Zitto Kabwe ikiwezekana atoweke duniani. katibu wa bunge akapimwe akili zake.

  Mimi kwa kutumia mawazo mazuri kutoka kwa Mungu zitto hasumbuliwi na malaria.

  Nina hasira, wapendwa.
   
 2. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,608
  Likes Received: 2,461
  Trophy Points: 280
  Aisee sikubaliani na ww hapo uliposema eti kuna njama nzito ikiwezekana Zitto atoweke duniani..
  Mi nadhani huu si muda muafaka wa kugeuka wanajimu na kuanza kutabiri yajayo.. La msingi hapa ni kumuombea ili Mungu amponye..
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Pole shusha pumzi upunguze hasira.

  Kama wanadanganya, ukweli utajulikana tu.

  Hatahivyo nimemsikia kaka yake redioni akisema zito anaumwa malaria na kwamba anaendelea vizuri. Je, na yeye anadanganya?
   
 4. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Tutajua tu, hasira za nini?
   
 5. only83

  only83 JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Nilikuwa naangalia habari hii nikiwa na mama yangu wakati inarushwa,mama yangu aliniuliza swali moja..ana malaria ya namna gani hiyo? Mimi nikasema sijui ila Muhimbili imeshindwa,yeye akasema sasa kama muhimbili imeshindwa kutibu malaria Je,zile hospital zetu za kata kule Same na kwingineko itakuwa habari gani? Kimsingi tukubali tukatae Kaka Zitto anaumwa....
   
 6. j

  jigoku JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ki uhalisia mambo haya yanachanganya, hapa bado ukweli halisi hata mimi sijau-grasp.

  Kama kweli issue ya Malaria mtu inabidi ahamishwe hospital.lakini huko nako akahifadhiwe ICU, na bado tunaelezwa kuwa ikilazimika atapelekwa India mwishoni mwa wiki au mwanzoni mwa next week.

  Je hivi hii ni Malaria tu au kuna malaria ya kisasa? hapa tunahitaji kuambiwa ukweli isije ikawa propaganda.

  Kikubwa tumuombe Mungu amponye haraka.
   
 7. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2011
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wewe mbona una lugha kali punguz hasiraa bana
   
 8. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  CCM wanaposema malaria hawana maana ile homa inayo sababishwa na vimelea vya aina ya Plasmodium falciparum, Plasmodium ovale, Plasmodium vivax ama Plasmodium malariae wanao sambazwa na m'mbu aina ya anophele. Malaria ya CCM ni ushirikina kuchanganya na interijensia ya kifisadi.

  Kama magamba yalikaa na kuazimia kuwa chama chao hakija anza kuua leo, basi huo ni muendelezo wa kukolimbana tena kwa kasi ya ajabu. Na kwa mtindo huu, LAZIMA WENGI WATAONDOKA kwani dalili za mvua ni mawingu!
   
 9. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Madaktari wamesema ni malaria wewe unapinga, hebu tuambie ugonjwa wake sasa.
   
 10. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,155
  Likes Received: 3,346
  Trophy Points: 280
  Wacwac ndio kitu gani?
   
 11. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Malaria India!
   
 12. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Msiwe na wasiwasi inawezekana Mhe. ana complication ya tu ya
  Malariaehivkisukarisis ugonjwa ambao Muhimbili umewashinda. Heri wampeleke India wasije mkata mguu au kichwa.
  Namtakia apone haraka
   
 13. J

  Joseph Isaack JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ni muhimu kuliangalia hili kwa umakini hasa ukihusianisha na mambo mengi ya kukanganya ya kisiasa yanayoendelea.
   
 14. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Siyo kila kitu utaambiwa sahihi, mbona ugonjwa wa Mwakyembe bado inabaki kuwa siri ya Dr wake na yeye mwenyewe, jiulize?
   
 15. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  inawezekana ili la kutaka kumpeleka india halina ulazima sana, lakini itabidi hiwe hivyo mradi tu serikali ijitoe kimasomaso
   
 16. OPTIMISTIC

  OPTIMISTIC Senior Member

  #16
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimeshindwa kuelewa pia, haiwezekani malaria ikashindikana aghakhani mgwonjwa awe reffered mnh. Kuna taarifa haijawekwa wazi
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Ah! Ushakiri mwenyewe una hasira, nilikuwa nina majibu makali sasa ngoja niweke pending!
   
 18. Nico1

  Nico1 JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  ndg ulichokiandika ni sahihi haiwezekani malaria impeleke mtu nchi za nje akapate matibabu kwa hiyo hata hz tiba tunazopewa wanatudanganya hazitibu nadhan hii inajidhilisha wazi..kwa mh zitto hapa ni suala la kilozi japo serikali inajifanya haitambui tena wakicheza watauana mpaka waishe kwa tamaa na uroho madaraka pamoja na wizi mali za wananchi.
   
 19. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kwani Ni Mara Ya Kwanza Zito Kuumwa, kuumwa sio kifo inatakiwa tumuombea apone kama kuna tatizo la ndani hatuwezi kujua mpaka aseme mwenyewe.
   
 20. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Kwa jinsi wahindi walivyo watu wa dili, usikute huko ndo kunageuzwa kuwa machinjio rasmi ya watu wenye uchungu na nchi hii. Yote haya yana mwisho. Wanaweza kumtoa mtu duniani lakini hoja zitabaki pale pale na kuendelea kujadiliwa siku zote mpaka kieleweke. Tutashinda tu!!!!!!!!!
   
Loading...